Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe, Geofrey Kiliba, amesema kuwa mwezi wa Oktoba ni kipindi muhimu mno kwa Watanzania kuungana na kushikamana kwa dhati ili kuonesha mshikamano wa kitaifa na kuendeleza amani. Kiliba alisisitiza kuwa uchaguzi wa mwaka huu si tu tukio la kisiasa bali ni fursa ya kipekee kwa Watanzania kudhihirisha kwa Dunia nzima kuwa taifa letu ni timamu na linaelewa nini maana ya maendeleo na kuwa kuna watu wanataka kuvuruga watanzania ili kuharibu amani ya nchi
" Kuna watu wana amini ili kusudi waingie madarakani waongoze Taifa hili, wanapaswa kuwavuruga watanzania kwa mbinu zile za kishetani" Amesema Kiliba
" Kuna watu wana amini ili kusudi waingie madarakani waongoze Taifa hili, wanapaswa kuwavuruga watanzania kwa mbinu zile za kishetani" Amesema Kiliba