Kilango adaiwa kusambaza kadi feki za CCM Same | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilango adaiwa kusambaza kadi feki za CCM Same

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Babylon, Jun 5, 2010.

 1. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kilango adaiwa kusambaza kadi feki za CCM Same

  Saturday, 05 June 2010
  Elias Msuya


  MBUNGE wa Jimbo la Same Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Anne Kilango amedaiwa kusambaza kadi feki za CCM ili kumpa ushindi katika kura za maoni zinazotarajiwa kufanyika baadaye mapema mwaka huu.

  Kubainika kwa kadi hizo, kumekuja kufuatia uandikishaji wa wanachama katika daftari la wapiga kura la CCM, unaoendelea nchi nzima.


  Taarifa kutoka jimboni humo zinasema kuwa, kadi feki zimebainika katika matawi ambayo inasemekana ndiyo ngome ya Mbunge huyo ambayo ni pamoja na Tarafa za Mamba, Vunta, Mpinji na Kirangare.


  Taarifa hizo pia zinasema kuwa, mbunge huyo amekuwa akiwatumia viongozi wa CCM katika kata na tarafa hizo, wakiwemo wenyeviti, makatibu na madiwani wa CCM wilayani humo.


  "Makadi hayo ni feki ya CCM yaliletwa jimboni na Kilango mwenyewe na kuyakabidhi kwa watendaji wa CCM, madiwani, makatibu kata na matawi. Ni mradi wa Kilango," alisema diwani wa kata moja katika wilaya hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa ajili ya usalama wake.


  Diwani huyo pia alisema wahakiki walipokwenda jimboni humo, viongozi wa CCM wa kata zote waliitwa wakiwa na madaftari ya wanachama wao, na ilibainika kuwa kadi nyingi za wanachama wao, siyo halisi.


  "Walipoulizwa walikiri kuwa kadi hizo walipewa na madiwani ambao nao walipewa na Mbunge Anne Kilango" alisema


  Hata hivyo Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Sophia Kilingo aliyekuwa akiongoza uhakiki huo alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu madai hayo, alionyesha kushtuka na kusema kuwa ni mapema kuzungumzia madai hayo kwani bado uhakiki unaendelea.


  "Wewe nani kakwambia? Siyo kweli, kwanza bado tunaendelea na uhakiki," alisema.

  Alipoulizwa kuwa uhakiki huo utamalizika lini alizidi kuwa mkali.


  "Wewe nimeshakwambia kuwa tunaendelea na uhakiki, kwani una haraka gani? Tukimaliza nitakwambia," alisema Kilingo na kukata simu.


  Naye Anne Kilango alipoulizwa aliruka na kueleza kuwa hana sababu ya kufanya hivyo.


  "Mimi ndiyo nahusika? Huyo aliyekwambia ndiye akueleze yote, sina sababu ya kufanya hivyo. Kwa heri," Alisema Kilango na kukata simu yake.
   
 2. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  Tanzania ni nchi ya kipekee anayekemea uovu ndio unageuka kuwa public enemy no 1 kaza buti mama fisadi hana aibu, hana huruma!
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hawa CCM woooote mafisadi tu...wasitusumbue sijuwi kuchukuwa hatua unafiki mtupu...kwa taarifa yako tu baraza la mawaziri la serikali ijayo baada ya uchaguzi limeshapangwa miongoni mwao hawajatangaza hata nia ya kugombea ubunge, tusubiri tuone ila cha ajabu kwa mara ya kwanza Tanzani kutakuwa na Wizara inayoongozwa na mtu kutoka upinzani, sijuwi nani, haya kina Zitto ndo mjipendekeze tena...hakuna cha masilahi ya wanyonge wala nini kwa rangi hii ya kijani ni tumbo lako tu...!
   
 4. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Habari zingine ni za kuchekesha sana. Kadi za CCM ni ghali sana kupatikana mpaka zigawiwe feki? au kuna mlolongo mkubwa sana wa kuipata kadi ya CCM. Huu nadhani ni upuuzi tu wa kutafuta habari hata sehemu ambayo haipo. Hayo ndiyo yanayosababisha watu kwenda nje ya nchi kugombania uanachama wa CCM.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wala haipatyikani kwa shida lkn kwa taratibu walizojiwekea mwaka huu kwenye kura ya maoni kila atakayeshiriki ni lazima awe na kadi, hiyo ndo inasababisha vurugu hizi. In fact tatizo halipo huko tu, for the past three days hata Dar kuna taarifa nyingi tu kuhusu kadi za Cm kugawiwa kama njugu... watu wameshaingia kazini
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nauliza: Kwani Sophia Simba anahusika nini hapa? Kwa wadifa wake kama Waziri wa Utawala Bora au kama M'Kiti wa UWT? Nadhani haya masuala ni ya CCM -- chombo kinachosimamia uchaguzi (nadhani kipo) katika chama hicho. Mimi nadhani Babylon kaiweka topic hii kwa sababu tu Kilango na Simba wameshawahi kukwaruzana huko nyuma. Nitashangaa iwapo Simba, naye mwenyewe ana tuhuma kibao kuhusiana na nyadhifa zake zote hizo mbili alizo nazo ataliingilia suala hili.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nadhani Chenge, ambaye ndiye mzee wa maadili ndani ya CCM, ndiye anahitajika hapa
   
 8. K

  Keil JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Halafu tutegemee kwamba Chenge anyooshe kidole kwamba kuna makosa wakati yeye mwenyewe kazungukwa na kashfa kila kona?
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Zitakuwa kutoka China hizo!
   
Loading...