UNDENIABLE
JF-Expert Member
- Feb 26, 2013
- 2,326
- 1,314
NB: Akisi zaidi katika mtizamo wa mamlaka ya kisiasa:
Twende sasa:
Kuna wengi hawatanielewa. Enewei sijali sana. Naandika kwa ajili ya wachache sio kwa ajili ya wote.
Ipo hv.
Hv umewahi kuwaza wapi nguvu za utawala zilipo? Namaansha utawala wa kisiasa. Utawala wa kibiashara. Utawala wa kiimani. Aina yoyote ya utawala unaujua wewe.
Basi, leo nakwambia zipo kwa wanawake. Kama unabisha nenda kamuulize shetani maana nadhani ndo yeye pekee aliyebahatika kung'amua hio siri. Wapi Adam, Wapi Samson kwa kuwataja wachache tu.
Unaambiwa Adam alikuwa anaongea live na Mungu, lakini kupitia nguvu za Mwanamke Adam alikwenda kinyume na maagizo ya Mungu. Ardhi imelaani kwa ajili yetu na yeye atajifungua kwa uchungu. Duuuu! Enewei achana na hayo.
Mwanamke habebi vyuma kutunisha misuli. Wala hana mbio km Usain Bolt. Ila anaongea sana. Ana mdomo sana. Hahahahaha! Unajua nguvy ya ulimi wewe? Kawaulize watumishi watakwambia. Achana na hayo pia. Hebu tuendelee kidogo.
Unakumbuka wimbo wa No woman no cry? Usiniambie kaimba nani. Wewe tafakari tu hayo maneno wala sio content ya wimbo mzima.
Haijalishi wewe mwanamme una nguvu kiasi gani, bosi wako ni mwanamke. Hata mfalme, hata rais hata nani na nani bosi wake ni mwanamke. Ndo kusema mamlaka anayo mwanamke. Usibishane na mimi kabishane na aliyeumba.
Day in day out harakati zote za wanaume. Yaani zote. Nasema zote ni za kumtumikia mwanamke. Sikiliza nafsi na roho yako itakwambia hili. Ila akili yako itakubishia katakata. Hakuna mwanamme anaweza kuishi bila mwanamke na hakuna mwanamke anaweza kuishi bila mwanamme. Achana na maigizo tunayofanyiana. Oooohhh nipo single! Na ngonjera kibao. Roho, nafsi na mwili wote unawaza mwanamke na mwanamme. Jaribu kusikiliza nafsi yako itakwambia ukweli, achana na akili yako itakupotosha tu.
Fikiria kwa mfano wanawake wasingekuwepo, halafu tupo wanaume tu. Wala wanaume wasingehangaika na maisha haya. Tungekuwa tupo tupo na mambo yanaenda. Ila sasa uwepo wa wanawake unatuhangaisha sana maana ndio mabosi. Sisi ni watumwa by nature. Ok, achana na upande huu. Hebu twende upande wa siasa kisha biashara.
Kisiasa, mtaji wa mamlaka yoyote yale ni wanawake. Kawaulize CCM na CDM watakwambia. Kama kwa mfano wanawake nchi nzima wakachachamaa kuhusu Bashite na kweli anatoka kesho asubuhi.
Kama kwa mfano wanawake wakachachama nchi nzima ama dsm pekee kuhusu JPM na kweli kesho asubuhi jambo linatokea. Lakini wanaume wakichachamaa wala haistui sana watapigwa tu viboko vizuri na maisha yanasonga mbele. Lkn kwa wanawake Dunia nzima lazima ishutuke.
Fikiria kwa mfano. Wanawake wote wakagoma kupiga kura. Wote. Yaani wote. Nadhani matokeo yake yanafahamika. Maana hata wanaume nao hawatapiga kwa wingi sana kwa ushawishi wa wanawake pekee.
Kimsingi, wanawake wakiamua kusimamisha hii Dunia nakweli inasimama. Achana na hayo hebu twende biashara.
Kawaulize matajiri watakwambia wateja wao wengi ni nani. Kamuulize Bakheresa ama Dewji. Watakwambia. Kamuulize Mengi atakwambia. Wanaweza kuwa wateja direct ama indirect kutokana na ushawishi wao.
Wanawake wakiamua kumpinga mtu kanisani i mean mtumishi. Huyo lazima atoke. Haina mjadala. Makazini wanawake wakiamua kumng'ang'ania mtu huyo lazima aache kazi. Haina mjadala.
Nini kilichojificha. Hiki hapa. Mwanamke hafahamu nguvu zake alizo nazo juu ya Dunia hii na hata kwa mwanaume. Shetani anafahamu na anakula naye sahani moja. Maana ili shetani afanikishe mambo yake anahitaji kumtumia mwanamke.
Katika familia kwa mfano. Kama mwanamke amesimama imara hio familia itakuwa imara pia. Hata kama hamna baba. Lkn kama familia baba kasimama imara mama hajasimama imara hio familia itapoteza mwelekeo tu. Mbeba nguvu yaani mwanamke hajasimama imara.
Mwanamme anafahamu nguvu za mwanamke. Maana ni bosi wake naturally. Siku mwanamke akijua na kuamua kutumia nguvu zake basi maisha yatabadilika sana. Dunia itakuwa tamu mno. Maana wanaume watakuwa very responsible and disciplined. Wanawake watatunyoosha. Bahati mbaya sana hili halitatokea ktk picha kubwa bali kiduchu kiduchu hapa na pale.