Kila siku Okwi Okwi,ni kwel anahitajika?

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
859
1,000
Habar wadau,

Mimi ni mmoja Kati ya wasomaji WA magazeti waliobakia na hata nisiposoma bas angalau vichwa vya Habari vya siku havinipiti.
Nimegundua Kuna gazeti au magazeti fulani ambayo kama si kila yanapotoka bas kila baada ya siku chache lazima yawe na vichwa vya habar kama "okwi anarudi mwanangu","okwi uhakika msimbazi","narudi msimbazi-okwi" na vingine vingi vya kuashilia kurudi kwa okwi simba.

Pengine level yangu ya ufahamu ni ndogo ndio maana nimekuwa nikishangazwa na magazeti haya kujaribu kuliweka Jina LA okwi karibu Sana na vichwa vya mashabiki WA simba,najiuliza ni kwel okwi anahitajika bado na simba?kama anahitajika mbona hawamsajiri badala yake usajiri wake unafanyika kwenye magazeti kila siku.

Katika Hali halisi soka ya Sasa inahitaji vijana zaidi ili kutengeneza ushindani WA kweli na kwa mantiki hiyo nitashangaa Sana kama simba itamsajiri Tena mtu kama okwi ambaye anapaswa Sasa kuachwa kumalizia soka yake huko aliko.

Bado niko kizani kwann magazeti hayo bado yanaendelea kuweka vichwa vya habar vya okwi Mara kwa Mara,je Kuna uwezekano okwi anawalipa ili kutengeneza saikolojia ya kuhitajika kwa simba au Kuna viongozi wanamtaka kwa maslahi Yao na ndio wanaolipa waandishi ili akiletwa aje kwa kishindo na hivyo kuhalalisha malipi makubwa ya kumsajiri harafu watu wapige hela za simba kijanja?

Mwenye jibu LA hili anisaidie tafadhar.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom