Kila siku ni ukurasa mpya kwenye kitabu cha maisha yako

Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
4,726
5,442
Ndugu zangu wa JF, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila fursa anayotupatia kila siku ya kuendelea kuishi hapa duniani. Wapo ndugu zetu, majirani, tuliofanya kazi au biashara pamoja, jamaa na marafiki ambao hatunao tena duniani. Lakini wametangulia kuondoka kabla yetu.

Kila siku Mungu anayotupatia kuendelea kuishi duniani tujue, kuwa hiyo siku ni miongoni wa kurasa kadhaa ambazo tunaendelea kuziandika katika kitabu cha maisha yetu hapa duniani, tangu tulipozaliwa.

Swali la msingi la kujiuliza ni je, nina andika nini kwenye kurasa zilizomo katika kitabu hicho, ambacho kitaacha ukumbusho mwema hapa duniani, lakini pia kitaamua hatima ya MAISHA YETU YA MILELE BAADA YA KUONDOKA DUNIANI.

Mungu atuasidie kufanya uchaguzi sahihi wa kuishi maisha matakatifu hapa duniani ili vitabu vyetu viandikwe mambo mema yatakayotusaidia kupata hatima njema ya kuingia Mbinguni.

Jinsi ya kufanya ili kuishi maisha matakatifu hapa duniani:-

1. Kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha. Mithali 28:13....Afichaye dhambi zake hatafanikwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata
rehema

2. Kumkubali Yesu Kristo awe Bwana, mwokozi na mtawala wa maisha yetu, ili atusaidie kushinda dhambi, kwa sababu hatuwezi kushinda dhambi kwa nguvu zetu wenyewe.
WARUMI 10: 9-10.... " Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu".

MUNGU AKUBARIKI NA UWE NA JUMAPILI NJEMA.
 
Back
Top Bottom