Gerald Robert
JF-Expert Member
- Jan 2, 2013
- 337
- 219
Hakuna jambo lolote lililo jema ambalo utaweza kulipata au kulifanikisha bila ya kuwepo na upinzani,
kila njia ya mafanikio uiendeayo huwa haikosi upinzani wa kuzuia mafanikio hayo,
Kumbuka kwamba ili ufanikiwe ni lazina upambane kuvishinda vikwazo vinavyozuia mafanikio yako,
Ili urithi baraka za Mungu ni lazima upambane maana mafanikio huwa hayaji kirahisi rahisi tu
Kumbuka ya kwamba, mpango wa Mungu ni wewe ufanikiwe, lakini mpango wa shetani kuzuia mafanikio yako,
Usiku na mchana shetani na mawakala wake huwa wanapambana kuhakikisha wewe usifanikiwe katika jambo lolote lile
Usifanikiwe katika Kazi yako,
Katika ndoa yako,
Katika masomo yako,
Katika biashara zako, nk
Yawezekana Mambo yako katika eneo fulani la maisha yako hayaendi vizuri nikwasababu wewe umelala usingizi na hautaki kupambana kwaajili ya mafanikio yako, au yawezekana ukawa ubapambana lakini ni kwa kuzitumaini akili zako badala ya Mungu.
Shetani ndiye adui yetu mkubwa chini ya jua, akikushindwa rohoni huja hata mwilini.
Mshirikishe Mungu katika mambo yako yote maana Mungu ni Adui wa adui zetu, hakuba aliyeshindana na Mungu na akatoka salama,
Mbinu kubwa ya kumshinda adui yako ni wewe kutokukata tamaa na kutoruhusu hafu ikutawale kwa vitisho vya adui yako.
MUNGU AKUBARIKI
By Mtumishi Gerald Robert
Sent from my HUAWEI Y360-U82 using JamiiForums mobile app