Kila nikishusha Bei dhidi ya washindani wangu nao hushusha Zaidi yangu, nifanye nini kuongeza mauzo?

Kwahio unatuambia nini mkuu?! Ushauri...?
 
Excellent.
 
Sidhani kama nina jibu ila sio mbaya nikiweka ushauri wangu pia.
Kwanza kupunguza bei ni jambo jema, pale ambapo bado kuna faida reasonable. Anayepima faida ni reasonable ni wewe! Kwa hiyo nikushauri vitu vichache
1. Panua wigo wa soko lako. Jaribu kuwafikia watu wengine. Unasema ni duka la jumla. Ina maana unaweza ku supply kwa maduka ya reja reja. Badala ya kukaa hapo na kugombea wateja fanya kuwatafuta wateja wa reja reja huko waliko. Tumia mitandao na hata kutembelea maeneo mbalimbali na ujaribu kuwaomba uwe supplier wao. Ukiongeza wigo wa soko, unaongeza uwezo wa kushindana pia. Itakugharimu muda na nguvu, lakini ndio njia ya kuongezeka.

2. Offer Delivery. Wateja wengi huwa wanakuja kwa sababu hawana namna. Ukiwapa ofa ya kuwapelekea kwa gharama kidogo watapenda sana, haswa kama mtajenga uaminifu.

3. Punguza matumizi yasiyo ya lazima. Kama unashusha bei inabidi na matumizi yapungue ili kufidia punguzo.

Sio mtaalam wa hiyo aina ya biashara ila kutoa ushauri sio jambo baya!
 
Nyota naisafisha kwakutoa zaka ktk Mali yangu
Ushawahi kusikia chochote kuhusu ndumba kwenye biashara labda? Au kusikia figisufigusu za biashara maybe? Dawa za kuongeza mvuto? Kalumanzira je...Tawire tawire
Kuna wanaofanya hivyo na wanatusua


Japo nakwambia sio uende huko maana unaweza kukuta wenzio wanakupiga gap kutokana na hizo ishu

Ushauri wangu fuata hizo tips unazopewa na wadau za price, customer care,people,promotion, place n.k
Hakuna Cha nyota kufifia Wala nin....nichangamoto zakibiashara tu mkuu

Sent from my SM-J720F using JamiiForums mobile app
 
Kwahio unatuambia nini mkuu?! Ushauri...?

Ni kupambana tu ingawa unapambana na watu wa aina nyingi sana na wengine wanakuwa na bidhaa nyingi za wizi kwa hiyo hata akiuza cost bado ana faida maana kalipia hela kidogo sana

Mkuu nazijua biashara hizi na faida zake sio kubwa halafu mtu anauza mpaka cost

Ni mapato wanayajua haya kuwa wengi hawana elimu ya ulipaji wa kodi ndio maana wengi wanakadiriwa tu

Ushauri ni kuweka bidhaa zenye faida kubwa au kujitahidi kuwa na miradi mingi
Kuwa na biashara tatu au nne ni nzuri zaidi
 
Pole mkuu kwa changamoto hiyo
Kiukweli wewe unapitia changamoto Kama yangu
Ila Hebujaribu mbinu hizi
1 omba mungu kwa Iman yako Kila siku kabla na baada ya kufungua biashara yako
2 fungua mapema kuliko wenzako na funga kwa kuchelewa kuliko wao
3 kuwa msafi kwenye mwili, mdomo (kauli nzur kwa wateja) pia mpangilio mzuri wa bidhaa zako
Nk usisahau kuwa mcheshi na mchangamfu hasa kwa watoto heshima kwa wakubwa hasa wazee
4 jiongeze kwenye vitu ambavyo kwa namna yyte ile wapinzan wako hawawezi
Mfano
Tafuta maharage mazuri kuliko wao,
Choroko na karanga nzur kuliko wao
Uza Hadi vile vitu ambavyo watu weningine hawana mfano sindano za kushona nguo nk
5 tafuta Bango andika baadhi ya vitu na Bei zake Kisha liweke hapo njiani karibu na duka lako watu wakipita walione

6 tembelea mama ntilie waombe wawe wateja wako ukipata 5 wanaochukua angalau vitu vya 20000 Kila siku una uhakika w mauzo ila uwe nao makin ni warushi wazuri sana

Nakutakia Kila la kheri mdau mwenzangu
 
Baadhi siyo wateja ni watu wanajumua kwako wanapeleka kwa miongoni mwa washindani wako na wanarudi kwako kukupa pressure, uza bei yako utayopata faida wateja wa kweli utawapata tu pia ongeza thamani kwenye biashara yako kama lugha nzuri, kufanya delivery, nyongeza ya ziada.
 
Umemshauri vizuri sana mkuu.
 
Pole sana mkuu. Ushauri wangu unaweza kuhitaji muda kidogo ila ukisimama utakuletea matokeo ya muda mrefu sana

Wewe shida yako ni wateje na ushindani.

Binafsi naamini katika Nguvu ya Digital Marketing na kujenga uhusiano mzuri na wateja na kuwatumia kama mabalozi wangu.

Digital Marketing ni uwekezaji unaoukujengea brand na kupaisha biashara yako popote muda wowote.

Ila unahitaji muda (Kuanzia miezi 6)ili kupata matokeo mazuri.

Kufanya biashara locally kama zamani kwasasa ni changamoto.
 
Umewahi kufanya biashara?
 

Tafuta source ya uhakika na nafuu unapochukulia mzigo huenda wewe unachukua ghali ndomana wanajua wakishusha mpaka sehemu fulan we huwezi Mana itakula kwako.

Tafuta chanzo lingine cha kuchukulia mzigo pengine mpigie supply wako kwa namba nyingine jidai unataka mzigo alafu sema bei ya chini ili uone Mambo inakuaje!

Hyo n akili ya salesman nimekupa sababu tabia zetu tunazijua duka zinatengana kwa ukuta tuu au barabara lakini kila mmoja anabei yake
 
Huo ubinafsi wako ndo unakuponza, mda wote unawaza vita, wenzako wanataka amani, wewe ukiwasha moto wao wanakuja na maji wanauzima unabaki kupangusa majivu
 
Nina duka la jumla la dawa za binadamu mbinu ninayotumia ni ndogo sana nawapumbaza wateja wangu kwa kushusha bei bidhaa Fulani uku bidhaa nyingine napandisha bei zaidi..ile bidhaa niliyoshusha bei ndio inaficha bidhaa fulani niliyopandisha bei....
Iko hivi naangalia items zinazotoka sana ndio hizo hizo nashusha bei uku items nyingine napandisha bei kubwa sana...yaani wateja hawakauki wanasema nina bei ndogo kumbe nawazuzua kwa baadhi ya items nang'ata na kupuliza
 
Umetishaa
 
Ongeza muda wa kufungua na kufunga biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…