Kila nikishusha Bei dhidi ya washindani wangu nao hushusha Zaidi yangu, nifanye nini kuongeza mauzo?

malembeka18

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
2,780
2,706
Habari wakuu,

Nimekuja kwenu kutaka fikra na mawazo.. Niko ktkt biashara ya duka la jumla la vyakula kwa muda Sasa changamoto iliyopo kila mshindani wangu analenga kushika wateja soko kwa kushusha Bei chini Zaid nami nimekua nikishuka nao..

Sasa Basi Hali hii imepelekea kuzid kukupunguza faida ktk kila bidhaa matokeo yake unajikuta ktk bidhaa unayoiuza 56000 unabakiwa na faid200.

Na ukisema ubaki na bei juu tofaut na washindani wako Basi wateja wengi hukimbilia kwa wenye Bei ndogo Zaid maana soko ni dogo wateja niwale wale mnafanya kugawana wateja kwa mbinu ya kushusha Bei.

Wakuu nin nifanye nitoboe maana nawaza mbinu nyingi Zina feli.
 
Boresha ubora wa bidhaa zako kushinda washindani wako, then acha bei hiyo hiyo, usishushe.
Naboreshaje mkuu maana bidhaa za vyakula unavozijua ni bidhaa zinazozalishwa naviwanda vya humu humu nchini bidhaaa Kama ngano,sukar,mafuta,chumvi,juis,maji, Sasa hapo mkuu naboreshaje ubora wabidhaa Hali mim simzalishaji...napia namna soko lililivyo wateja wameshazoea Bei ndgo ukiweka Bei kubwa hautampata mteja hata mmoja utabaki unazishangaa bidhaa zako mwenyewe dukani
 
wake up
:unawateja wanao kutingisha kukuona uzaifu wako.

jibu zuri!
ukiona mtu hataki kufika bei zako mruhusu kwenda huko ana sema bei ni chini!

hizi code uwezi pata sehemu yoyote
Mkuu kila siku natafiti wapinzani wangu Bei wanazouza nna mashushu wangu wangu napia nimekua nikitumia mbinu yakununua bidhaa toka kwa washindani wangu kwakutumia mtu na anapewa kwa Bei ndogo nachenji inarud so
 
wake up
:unawateja wanao kutingisha kukuona uzaifu wako.

jibu zuri!
ukiona mtu hataki kufika bei zako mruhusu kwenda huko ana sema bei ni chini!

hizi code uwezi pata sehemu yoyote
Sjakuelewa unapisema nna wateja wanaonitingisha kwakuniona udhaifu wangu kivip hapo sjaelewa
 
Mkuu kila siku natafiti wapinzani wangu Bei wanazouza nna mashushu wangu wangu napia nimekua nikitumia mbinu yakununua bidhaa toka kwa washindani wangu kwakutumia mtu na anapewa kwa Bei ndogo nachenji inarud so

Unaendeshwa na wateja wanaokujua!
pili simama wewe na msimamo na uboreshaji wa biashara.

kuna wateja kujaribu,kuna wateja kuharibu kwenye biashara.

tatu punguza mazoea na wateja,wafanyabiashara wenzako mnaofanya biashara moja
 
Mkuu auboreshe vipi mchele na maharagwe
1. Kwa kuwa na kauli nzuri kwa wateja.

2. Kuweka mazingira ya duka lako safi.

3. Kutoa bonus mfano akinunua kilo moja ya mchele unampa na pakti ya chumvi free au kama ni mtoto unampa pipi kama zawadi.

4. Ukimpimia kilo moja ya mchele unamuwekea kanyongeza kadogo ka mchele (na una mwambia umeona nimekuongezea?)

5. Kwenda kununua mchele kwa bei ya jumla...

Nk nk nk...
 
Badili biashara iwapo hiyo Unayoifanya sasa Haikulipi...!
Kwenye kubadili biashara ndio naumiza kichwa maana walaji wahuku hupenda Bei cheee kipato Chao wengi nichachini nawakati Kias so kuivest biashara inayoendana mlnahali yakipato Cha watu ktkt eneo langu ndo mtihani naumiza kichwa
 
Biashara ni sayansi na inataka elimu au uzoefu wa mda mrefu sana
Tatizo kila mmoja anafanya biashara siku hizi na faida ndio hizo mnazopigania za 200
Mtu anafanya biashara ya faida 200 na anakuambia siachi hata 100 basi bora kutafuta kazi nyingine

Mlo wao wanalia hapohapo kwa maji ya kisima yaani maisha ya wengine ni duni sana kiasi unasema hivi huyu ni mfanyabiashara au anaganga njaa tu
Mwisho wa mwaka TRA wakija kudai chao hujawakusanyia kabisa maana wewe ulikuwa unaweka faida yako tu bila kuweka na VAT maana ukiweka na hiyo vat bei lazima iwe juu

Ndio hapo tunarudi na kusema biashara ni Elimu
Angalia Asians wanavyofanya biashara
Kesho akiendesha V8 unasema mwizi kumbe faida ya bidhaa zake ni zaidi ya nusu na VAT kakulima kiaina

Tutakalia kusema wakuja wanaiba sana ila hatujui kuwa biashara ni zaidi ya tunavyoiona
Wengi wanafuata mkumbo tu halafu msimu wa kulima usifika anaenda kulima na kumuacha wife anauza duka

Sasa unajiuliza huyu ni mfanyabiashara au mkulima?
Sifoki ila ukweli ndio huo na wengi wanafeli kwa sababu ya jirani kampiga bao anaenda kuchukua mkopo wa mamilioni ili ajaze duka ila bado anakuja kufeli vibaya na mwisho nyumba inapigwa mnada

Hitimisho naona kiwango cha biashara kwa wengi ni kuuza ubuyu na karanga tu
 
Naboreshaje mkuu maana bidhaa za vyakula unavozijua ni bidhaa zinazozalishwa naviwanda vya humu humu nchini bidhaaa Kama ngano,sukar,mafuta,chumvi,juis,maji, Sasa hapo mkuu naboreshaje ubora wabidhaa Hali mim simzalishaji...napia namna soko lililivyo wateja wameshazoea Bei ndgo ukiweka Bei kubwa hautampata mteja hata mmoja utabaki unazishangaa bidhaa zako mwenyewe dukani
Ongeza customer base..usitegemee wateja haohao sikuzote..Tumia mitandao kujitangaza zaidi..Ongeza huduma za ziada.(fanya deliveries,walipaji wazuri unaweza kuwapa kwa mikopo,)lugha nzuri, mwonekano wa bashasha huvutia watu, mazingira mazuri ya ofisi,branding....

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Battle lako nisawa na la diamond na harmonize. Be you
Mkuu nihatar mkuu biashara hizi nichangamoto hasa kwasisi tulio maeneo yenye soko limited kwa maana mji ni mdogo walaji niwalewale alafu supplier ndo wanaongezeka ktk same business yaaan nawaza mbinu gani nitumie
 
Biashara ni sayansi na inataka elimu au uzoefu wa mda mrefu sana
Tatizo kila mmoja anafanya biashara siku hizi na faida ndio hizo mnazopigania za 200
Mtu anafanya biashara ya faida 200 na anakuambia siachi hata 100 basi bora kutafuta kazi nyingine

Mlo wao wanalia hapohapo kwa maji ya kisima yaani maisha ya wengine ni duni sana kiasi unasema hivi huyu ni mfanyabiashara au anaganga njaa tu
Mwisho wa mwaka TRA wakija kudai chao hujawakusanyia kabisa maana wewe ulikuwa unaweka faida yako tu bila kuweka na VAT maana ukiweka na hiyo vat bei lazima iwe juu

Ndio hapo tunarudi na kusema biashara ni Elimu
Angalia Asians wanavyofanya biashara
Kesho akiendesha V8 unasema mwizi kumbe faida ya bidhaa zake ni zaidi ya nusu na VAT kakulima kiaina

Tutakalia kusema wakuja wanaiba sana ila hatujui kuwa biashara ni zaidi ya tunavyoiona
Wengi wanafuata mkumbo tu halafu msimu wa kulima usifika anaenda kulima na kumuacha wife anauza duka

Sasa unajiuliza huyu ni mfanyabiashara au mkulima?
Sifoki ila ukweli ndio huo na wengi wanafeli kwa sababu ya jirani kampiga bao anaenda kuchukua mkopo wa mamilioni ili ajaze duka ila bado anakuja kufeli vibaya na mwisho nyumba inapigwa mnada

Hitimisho naona kiwango cha biashara kwa wengi ni kuuza ubuyu na karanga tu
Mkuu bado hujatoa suluhu naona bado nawe unalalamika tu..
 
Back
Top Bottom