Kila nikikaa chini, nikigeuka nyuma nauona UKIMWI

Padri Mcharo

JF-Expert Member
Feb 28, 2015
1,899
3,687
kama mtanzania na mwana JF mwenye ubinadam nimeona leo niwakumbushe wenzangu kuhusu hili balaa japo najua mnajua.

wanasema ushuhuda ni moja ya mawaidha.. leo natoa ushuhuda:

1. Mwaka 2001 nikiwa darasa la nne, Dada alikufa kwa UKIMWI. aliacha watoto wawili. Nikasema aaaah, dada nae alikua mcharuko sana, kila mtoto na baba yake!!!!

2. Mwaka 2003 nikiwa darasa la sita, Baba yangu mdogo alikufa kwa UKIMWI. Aliacha mjane na mtoto mmoja. Nikasema tena aaaaaah, huyu nae tatizo machimboni Mwadui kule.. mzembe

3. Mungu si Athuman, mwaka 2009 nikiwa nasubiri selection niende 4m5 BABA YANGU mzazi alifariki kwa UKIMWI. Daaaaah, alituacha mie, mdogo wangu wa kike na mama yetu wa kambo (mama mzazi waliachana miaka 19 iliopita).
Mwaka 2013 (miaka 4 after father passed) mama wa kambo akatuaga nae kwa UKIMWI baada ya kuzembea matumizi ya ARV.
So sad kwa kweli. Ugonjwa nilokua nasema kuupata uzembe ukaja kuni prove wrong ndan ya familia yetu.

NDUGU ZANGU.. UKIMWI UPO NA UNAUA... TUWE MAKINI...
 
Asante mkuu umenikumbusha mbali sana. Mwaka 1996 niliomba baba anipeleke Sengerema hospital nikahasiwe (niwe kama ng'ombe maksai) ni baada ya kushuhudia mjomba akifariki nikiwa naishi nae kipindi hicho hata ARV tulikuwa tunazisikia Kenya. Ni zaidi ya wana ukoo 16 wameshaondoka ukiacha mbali marafiki niliosoma nao. Anyway asante kwa kutukumbusha japo ukimwi kwa sasa tunachukulia kama malaria tu.
 
  • Thanks
Reactions: THT
Pole sana mkuu na asante kwa kutukumbusha, UKIMWI naona umesahaulika ktk vichwa vya watu, watu wamekumbwa na siasa akilini mwao, utumbua msjipu na starehe.
 
  • Thanks
Reactions: THT
Naona ukimwi imekuwa mada kuu ya weekend.
¤ Kuwa na mpenzi mmoja, pimeni na muwe waaminifu.
¤ Acheni kufanya ngono kabisa, hadi baada ya kuwa kwenye ndoa.
¤ Tumieni kinga wakati wa kuingiliana kimwili.
 
  • Thanks
Reactions: THT
kama mtanzania na mwana JF mwenye ubinadam nimeona leo niwakumbushe wenzangu kuhusu hili balaa japo najua mnajua.

wanasema ushuhuda ni moja ya mawaidha.. leo natoa ushuhuda:

1. Mwaka 2001 nikiwa darasa la nne, Dada alikufa kwa UKIMWI. aliacha watoto wawili. Nikasema aaaah, dada nae alikua mcharuko sana, kila mtoto na baba yake!!!!

2. Mwaka 2003 nikiwa darasa la sita, Baba yangu mdogo alikufa kwa UKIMWI. Aliacha mjane na mtoto mmoja. Nikasema tena aaaaaah, huyu nae tatizo machimboni Mwadui kule.. mzembe

3. Mungu si Athuman, mwaka 2009 nikiwa nasubiri selection niende 4m5 BABA YANGU mzazi alifariki kwa UKIMWI. Daaaaah, alituacha mie, mdogo wangu wa kike na mama yetu wa kambo (mama mzazi waliachana miaka 19 iliopita).
Mwaka 2013 (miaka 4 after father passed) mama wa kambo akatuaga nae kwa UKIMWI baada ya kuzembea matumizi ya ARV.
So sad kwa kweli. Ugonjwa nilokua nasema kuupata uzembe ukaja kuni prove wrong ndan ya familia yetu.

NDUGU ZANGU.. UKIMWI UPO NA UNAUA... TUWE MAKINI...
mkuu nakuomba sana badilisha hilo jina. linakuathiri kisaikolojia. wengi. wamepatwa na hayo matatizp jiskie raha mustrehe shukuru Mungu kwa uzima naomba ubadilishe hilo jina plz. kwa amani ya moo wako
 
Naona ukimwi imekuwa mada kuu ya weekend.
¤ Kuwa na mpenzi mmoja, pimeni na muwe waaminifu.
¤ Acheni kufanya ngono kabisa, hadi baada ya kuwa kwenye ndoa.
¤ Tumieni kinga wakati wa kuingiliana kimwili.
mkuu kwenye ndoa nako kuna mauza uza still sio solution cha msingi kumkabidhi Mwenyezi-Mingu maisha yako tuu. wala hamna. kingine peke yako hitashinda.
 
mkuu kwa nini hutak watu wawe na tahadhari?
Nilikuwa chupa ya 6 nimesoma hii mada nimejikuta kama ndio naanza chupa ya kwanza...... Mnatukata stimu bhana weekend is about Enjoyment haya mambo ya Ukimwi anzeni kuyasema j3 Aghhhhh
 
starehe ya siku moja isikuponze ubwie madawa siku zako zote..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom