kheri ya mwaka mpya wana jamvi woote...mimi ni kaka ninaye anza kutimiza miaka thelathini tangu kuzaliwa kwangu ....sasa kiukweli nimebahatika kupata kakibarua sehemu fulani huku mjini....sasa naamini ni wakati muafaka wa mimi kutafuta mwenza wa maisha tho nimechelewa kidogo, tatizo linakuja pale ambapo najaribu kuwa fuata wasichana kila ninaye mueleza azma yangu ananiambia pole kaka nishawahiwa na wengine wanadiriki hata kunitolea matusi kiukweli ni idadi kubwa sana ya wasichana nimewafuata bila mafanikio sura yangu ni ya kawaida tu haitishi ingawa nina kovu kidogo kwenye paji la uso ....nimekuwa mpweke sana na hii imepelekea niwe mwanachama mzuri wa kimboka kona bar na sehemu zingine kama hizo....huwa naona ndoa kwenye vyombo vya habari wanandoa wana pendeza kweli kweli nimekija humu kuombaushauri wenu ninakosea wapi?