Kila mtu na fungu lake...

Kila mtu na fungu lake...

nameless girl

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Posts
4,195
Reaction score
2,685
Mnaendeleaje? 😛
Leo ninaomba tuongelee juu ya KILA MTU NA FUNGU LAKE.
Mara kwa mara nikipita kwenye jukwaa hili kunakuwa na mada nyingi sana tofautitofauti. Wengine wanaleta mada hizo kutokana na miemko fulani ambapo ninaamini kwa namna moja au nyingine zinawaathiri baadhi ya watu kwa namna moja au nyingine.

Mfano mtu anapokuja na mada ya "Kurudiana na ex ni ulimbukeni wa hali ya juu." Kuna watu ambao waliachana na sasa wapo kwenye ndoa na upendo mkubwa ukitawala.
Kuna mada kama "Kuoa single mother..." , "Kuoa bikra..." nakadhalika.

Hapa ndugu zangu tunapaswa kufahamu kuwa kila mmoja na FUNGU LAKE. Kwa kuwa mimi siwezi kurudiana na ex basi ipitishwe kuwa kurudiana na ex ni ujinga. Hii inatokana na kuwa maisha yangu mimi hayawezi kufanana na ya mtu mwingine.

Hakuna haja ya kusikitika au kujiona mnyonge kuwa umeoa mtu mwenye mtoto au asiye bikra. Huyo aliyeoa hivyo, hilo ndilo FUNGU LAKE.

Ni sawa na mama ambaye anawajua vema watoto wake. Anajua Mwajuma nikimpa hiki atakifurahia, Asha nikimpa kile, kitamsumbua nakadhalika.
Tufurahi tukiwa hai kwa kuheshimu MAFUNGU YA WATU.
Nawasilisha.
 
Kweli haukuwa fungu langu
 
Mimi huwa najiuliza...

Sisi wanaume ni Rahis sana KUOA Mwanamke mwenye mtoto/watoto na tukawapenda kwa moyo wote na kuwajali .

Lkn nyie wanawake ukiolewa una mtoto/watoto au huna, ili mradi umeolewa na MTU mwenye mtoto/watoto basi Utaishia kumnyanyasa huyo mtoto weeee.

Shida ninin?? Au ndo tuendelee kuamin ndio fungu lako
 
Kwa fikra zangu ni kwamba kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kumfanya mama wa kambo awe mbaya. Lakini ikumbukwe kuwa si wote ambao wanakuwa wabaya.
Mojawapo ya sababu inaweza kuwa ni baba mwenye mtoto mwenyewe. Toka anapomleta mtoto wake ndani ya nyumba, basi anakuwa na mawazo hasi kuwa mtoto wake atateswa. Hapo tatizo linaanzia hapo. Chochote mama atakachokifanya, ataonekana anamtesa.

Pili mtoto mwenyewe. Akiwa ameanza kuelewa mambo, anaingia ndani akiwa na akili ya "Sio mama yangu." Hata mama awe mzuri vipi, kwa mtoto mwenye mtazamo huu atasema anateswa.

Tatu unaweza ukakuta tatizo lipo kwa mama mwenyewe. Hapendi kusaidia watu, mchoyo nakadhalika. Unapomletea mtoto wa watu, atajikaza siku chache, baadaye ataonyesha wazi tabia yake.

Nne yaweza kuwa watu wa nje kama ndugu, mama mtoto, majirani nakadhalika ambao kila mmoja atatoa maneno yake. Mama mtoto ataanza kumjaza mtoto sumu, mashoga na majirani watamjaza mke sumu na ndugu pia wanaweza kuwa chanzo cha kuvunjika kwa amani na mtoto kuanza kupokea chuki toka kwa mama mlezi.

Nyingine utanisaidia, maana hapa nawaza kulala tu...
 
Mnaendeleaje? 😛
Leo ninaomba tuongelee juu ya KILA MTU NA FUNGU LAKE.
Mara kwa mara nikipita kwenye jukwaa hili kunakuwa na mada nyingi sana tofautitofauti. Wengine wanaleta mada hizo kutokana na miemko fulani ambapo ninaamini kwa namna moja au nyingine zinawaathiri baadhi ya watu kwa namna moja au nyingine.
Mfano mtu anapokuja na mada ya "Kurudiana na ex ni ulimbukeni wa hali ya juu." Kuna watu ambao waliachana na sasa wapo kwenye ndoa na upendo mkubwa ukitawala.
Kuna mada kama "Kuoa single mother..." , "Kuoa bikra..." nakadhalika.
Hapa ndugu zangu tunapaswa kufahamu kuwa kila mmoja na FUNGU LAKE. Kwa kuwa mimi siwezi kurudiana na ex basi ipitishwe kuwa kurudiana na ex ni ujinga. Hii inatokana na kuwa maisha yangu mimi hayawezi kufanana na ya mtu mwingine.
Hakuna haja ya kusikitika au kujiona mnyonge kuwa umeoa mtu mwenye mtoto au asiye bikra. Huyo aliyeoa hivyo, hilo ndilo FUNGU LAKE.
Ni sawa na mama ambaye anawajua vema watoto wake. Anajua Mwajuma nikimpa hiki atakifurahia, Asha nikimpa kile, kitamsumbua nakadhalika.
Tufurahi tukiwa hai kwa kuheshimu MAFUNGU YA WATU.
Nawasilisha.
Kwani nimekosea wapi hadi uandike maneno makali namna hii..?

Mwanamke kiguu na njia wewe fungu lako nimelikosa!
Umenitapakaza kwenye dimbwi la damu,nipo hoi bin taabani!
Au kwakuwa ulisema unajiskia kuua tena ndio maana ulisign mikataba ya kishetani..?
Toka ulivyonibadirikia dar es salaam usiku ule nilipata hofu kama ningelirudi na roho yangu!,na hakika hata wewe usingerudi nayo ningekuondosha kwa kono la malaika gibril ungerudi na salamu toka kuzimu!
 
Mkuu mnafahamiana?.
 
Back
Top Bottom