Kila mtu apate haki yake kulingana na alichokitenda!

mcrounmj

JF-Expert Member
Feb 26, 2016
380
885
Wasalaam ndugu zangu wanajf wote!

Siku zote mwanafunzi akifanya vizuri hupongezwa kwa kupigiwa makofi au kupewa zawadi. Vivyo hivyo kwa mwanafunzi akifanya ujinga huadhibiwa kwa viboko ama adhabu nyingine. Hii inaitwa stahiki au malipo ya alichokifanya, yaani ukitenda wema haki yako ni kulipwa wema na ukitenda ubaya haki yako ni kulipwa ubaya.

Nimeamua kulipiza kisasi cha marehemu mama yangu. Sasa miaka imesonga tangu marehemu mama yangu atangulie mbele za haki. Kipindi anaanza kuugua na mpaka kufariki mi nilikuwa bado mdogo japo siyo sana kwani ndo nilikuwa nimehitimu darasa la saba.

Nikiwa mtoto wa pili kwenye familia nilipitia wakati mgumu wa kumuuguza mama kwani kaka angu kipindi hicho alikuwa anasoma secondary, wadogo zangu nao walikuwa primary. Hivyo ni mimi mtoto pekee ambaye sikuwa nimebanwa na shule kwani ndo nilikuwa nasubiri matokeo ya darasa la saba.

Familia yetu ilikuwa ni masikini sana, mzee alikuwa wa mtungi ile mbaya, kwahiyo hatukuwa na kipato cha maana. Mama alianza kuugua taratibu akijiuguza nyumbani, nikawa ndo namhudumia kumpikia uji na huduma zingine. Kwa kuwa ndugu zangu walikuwa wanasoma day yaani kwenda na kurudi, waliporudi walinisaidia baadhi ya majukumu kama kuteka maji na kufua nguo za mgonjwa.

Kuna siku mama alizidiwa sana, baba akashauri tumpeleke kwa mganga wa kienyeji umbali unavuka vijiji vitatu. Tulimpeleka usiku kwa usafiri wa baiskeli yaani zaidi ya kilomita therathini. Huko kwa mganga ilibidi mimi nibaki na mgonjwa wakati baba akirudi kuwajulisha ndugu zake na mama kuwa amezidiwa na hivyo yuko kwa mganga. Nilibaki na mgonjwa, sikuona ndugu wa mama, ilikuwa ni mtihani mzito kumhudumia ukizingatia nilikuwa mtoto wa kiume, lakini sikuwa na jinsi.

Familia yake mama, anao kaka waliokuwa na uelewa kidogo kwani wengine walikuwa na elimu ya form four kwa kipindi hicho mwanzoni mwa miaka ya 2000 it was a big deal, tena walikuwa wanafanya kazi kwenye kampuni yaani kipato chao ilikuwa so haba. Sasa mama aliugua, hakuna mtu alikuja kumjulia hali, hakuna aliyechangia chochote juu ya kumuuguza dada yao.

Kuna siku nikiwa na mgonjwa huko kwa mganga, alizidiwa. Hali ilikuwa mbaya zaidi, mganga akanituma niendeshe baiskeli nimfaate baba nyumbani. Nilitoka saa kumi na moja asubuhi, nyumbani nilifika saa mbili asubuhi ambako nilimkuta mzee wangu nikampa taarifa ya mama kuzidiwa. Baba alishauri tumpitie na mjomba mkubwa, kweli tulienda kwa Anko tukamtaarifu hali ya dadake. Tulipofika kwake tulikuta maandalizi ya harusi mtoto wake alikuwa anatolewa mahari kesho yake. Mjomba alitutaka tutangulie kwa mgonjwa yeye atafuata na pikipiki baadae. Walai mpaka tunafika kwa mgonjwa Anko hakuwa amefika. Kulingana na hali kuzidi kuwa mbaya ya mgonjwa, mganga alishauri tumrudishe nyumbani, kweli tulifanya hivyo.

Mjomba hakuja hata baada ya mgonjwa kurudi nyumbani. Tulisikia tu harusi iliendelea, mama ilimuuma, nilikuwa bado mdogo kuyajua mambo makubwa, lakini iliniuma sana. Mama hakukaa siku nyingi akafariki, ile siku amekufa wajomba walifika, ndio walisimamia shughuli za mazishi, lakini niliwaza, ina maana walijua ni matani haumwi au walisubiri afe ndo waje kuzika?

Pengine niseme tu labda kulingana na jinsi familia yetu ilivyokuwa masikini wakutupwa ndo maana walitutenga. Hata baada ya kifo cha mama yetu tuliwafuata kuomba msaada kwa ajiri ya shule, lakini walizingua na kutoa ahadi feki. Tulisoma kwa kuungaunga, mungu si athumani tumebadilisha muonekano wa familia kwa kuweka mjengo wa maana na mfumo mzima wa maisha kubadilika.

Sasa wamekuwa marafiki wakubwa wa mzee wetu, wameanza kuunganisha familia kwa kuwatuma watoto wao waje wasome kwenye nyumba zetu. Leo watoto wa marehemu Dada yao wamekuwa watamu. Juzi mjomba mdogo aliniomba nimpige kampani ya ada mtoto wake anaenda private kusomea clinical officer.

Kwa niaba ya mama yangu, niliapa nitaishi na kisasi hiki kwani naamini alikufa na kisasi kwa kukosa msaada wa ndugu zake waliokuwa wanajiweza. Potelea pote wacha nilipize kisasi cha mama yangu, kwani walijua tutaendelea kuwa masikini siku zote. Walisahau kuwa siku zinabadilika!!
 
Pole sana kwa yote uliyopitia, kama binadamu ni lazima uwe na maumivu na kumbukumbu ya yale mabaya yote na magumu uliyopitia pasipo msaada na tena ukizingatia kwamba wajomba zako walikua kwenye nafasi nzuri ya kukusaidia lakini hawakujali

Sijaua wewe ni Mkristo, Muislamu au Mpagani lakini naamini hakuna dini inayofundisha kulipiza kisasi, vitabu vyote vya dini na mafundisho ya kiimani yanatutaka tuwe watu wa kusamehe ili na sisi tupate kusamehewa.

Kama Mungu amekubariki na amekuwezesha kuwa na maisha uliyo nayo leo, basi huna budi kuwasamehe binadamu ambao Mungu amewaweka hai mpaka leo hii ili washuhudie mafanikio yako, na kwa kufanya hivyo unazidi kufungulia milango ya mafanikio zaidi

Ninaposema kusamehe simaanishi kwamba umsaidie ada, nanaanisha kwamba uondoe hiyo hasira na maumivu uliyonayo ndani ya moyo wako pasipo kinyongo dhidi ya hao wajimba zako, kama utapendezwa pia unaweza kusaidia ada lakini sio lazima
 
Unaonekana huna roho mbaya kbsaa...yaani kitu kidogo km hiki ndo unamaliza na bando kbsaaaaaaa....
 
Pole sana kwa yote uliyopitia, kama binadamu ni lazima uwe na maumivu na kumbukumbu ya yale mabaya yote na magumu uliyopitia pasipo msaada na tena ukizingatia kwamba wajomba zako walikua kwenye nafasi nzuri ya kukusaidia lakini hawakujali

Sijaua wewe ni Mkristo, Muislamu au Mpagani lakini naamini hakuna dini inayofundisha kulipiza kisasi, vitabu vyote vya dini na mafundisho ya kiimani yanatutaka tuwe watu wa kusamehe ili na sisi tupate kusamehewa.

Kama Mungu amekubariki na amekuwezesha kuwa na maisha uliyo nayo leo, basi huna budi kuwasamehe binadamu ambao Mungu amewaweka hai mpaka leo hii ili washuhudie mafanikio yako, na kwa kufanya hivyo unazidi kufungulia milango ya mafanikio zaidi

Ninaposema kusamehe simaanishi kwamba umsaidie ada, nanaanisha kwamba uondoe hiyo hasira na maumivu uliyonayo ndani ya moyo wako pasipo kinyongo dhidi ya hao wajimba zako, kama utapendezwa pia unaweza kusaidia ada lakini sio lazima
Nashukuru kwa ushauri kuntu mkuu, hii ndo radha ya kushare na wanajf, thanks chief
 
Hizi Hongera za kijinga kijinga ndo zinarudisha maendeleo yetu Nyuma..Alichofanya mleta uzi hata siyo kisasi ni Namna tu ya ku deal na watu wanaotuzunguka hasa ndugu.. sasa wewe unaleta ngonjera zako zisizo na Maana ndo maana asilimia kubwa ya wale ambao hujifanya wasamaria wema Hufa masikini..
 
nikiona visa kama hivi ndo najua kuwa ndugu ni kama marafiki ambao nature imetuforce kuwa nao maishani kwa kuzaliwa tumbo moja ila mbali na hapo, kheri marafiki sometimes

ila jamaa achana na hayo mambo maana unateseka kwa watu ambao pengine hata washasahau. kiukweli hayo maumivu ya vinyongo siyawezi na ni kheri nikae nao mbali tu ili kila mmoja akae na amani yake ila kama umeshadhamiria kufanya kisasi, jua kabisa unaanzisha ugomvi ambao uwe tayari kuupigana na pengine kurithisha kizazi chako maana usidhani upo in control kwa kitu kinachoshusisha reaction za pande mbili.

Hapa namaanisha na ndugu zako wa damu kama wana mawazo kama yako ila kama hawana bhasi unaweza hata kuathiri mahusiano yenu kama mkigawanyika kimsimamo na kimtazamo. Kuwa makini
 
...daaah story yako inataka kufanana na yangu,anko wangu alivyo mnyanyapaa mama yangu kwa kejeli na matusi...kisha kwa maneno yake ya kejeli na matusi aliyokuwa anamwambia mama akawa ananiambia na mimi kwa madai ananipa story ya marehemu...

Mbali na manyanyaso aliyokuwa ananifanyia Mimi na ndugu zangu wengne...aisee nimetokea kumchukia anko na nimeapa lazima nae aonje machungu aliyoptia mama yangu coz kila nkijaribu kusamehe akili inashindwa kabsa kusahau...

Naamini kisasi sio katka dhambi...kama kitampata muhusika tena kisasi kizuri ni kile cha ku double...

Ila mkuu hao watoto wake wachukulie poa hawana hatia ktk kisasi.
 
Back
Top Bottom