Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,231
KILA MTU ANAWEZA, ILA WEWE USIFANYE
Kila mtu anaweza kumshushia mwingine chini, ila ni mashujaa peke yake ambao wanaweza kuwainua wengine.
Kila mtu anaweza kumkatisha tamaa mwingine, kumwambia anachofanya hakitafanikiwa au atashindwa, ni wachache sana wanaoweza kutoa moyo kwa wengine.
Kila mtu anaweza kumsema mwingine vibaya, kumsengenya kwa wengine na
kusambaza maneno ya uzushi.
Ni wachache sana wanaoweza kuwasemea wengine vizuri na kusambaza habari zao nzuri.
Kila mtu anaweza kupata wivu pale mwenzake anapopiga hatua, na kufanikiwa zaidi, anajisikia vibaya na hata kuanza kukaa mbali naye.
Ni wachache wanaoweza kufurahia mafanikio ya wenzao, na kuwaomba ushauri zaidi wanawezaje na wao kufanikiwa.
Kama umegundua kwa makini kile ambacho kinaweza kufanywa na kila mtu huwa hakiwafikishi kwenye mafanikio, kinawafanya waendelee kuwa washindwa.
Lakini kile ambacho kinafanywa na wachache, ndiyo kinachopelekea mafanikio kwao na kwa wengine pia.
Maana unapokazana kumshusha mwingine chini, ni lazima na wewe ukae hapo chini ili kumzuia asipande juu.
Lakini unapomwinua mwingine, ni lazima na wewe upande juu ndio uweze kumwinua zaidi.
Usifanye kile ambacho kila mtu anaweza kufanya, fanya kile ambacho ni bora sana kwao na kwa yule unayekwenda kumfanyia.