Kila mtu anapambana na mtu wake ilimradi kiki na kujipambanua

RickNess

Member
Feb 10, 2019
7
37
Habari watu wa Mungu.
Nimekua nikifuatilia sana siasa za nchi hii,tatizo la wanasiasa wenginwa sasa,hasa vijana,ni kutafuta "nitoke vipi".
Hawana saiasa za masuala,wanafanya siasa za matukio.

Mtakumbuka,ishu ya ufisadi,watu waliamka nayo kwelikweli,sasahivi haipo,hali iliyopo na mwanasiasa kutafuta niseme nini nipate headlines.
Tumeimbiwa nyimbo nyingi,ila ule wa ufisadi ulibamba.

Wakati wa katiba mpya na michakato yake,si busara kuiimba tena leo,paliibuka walioibuka,wengine wakanufaika na mchakato,wengine wakaishia maumivu.
Wakati huo kila mtu aliijua katiba na vipengele vyake.
Walau kidogo wakati huo watu walizungumza masuala.

Hivi karibuni zimeibuka siasa za ku muattack mtu kama mtu,si masuala.
Huku Lisu akipambana na Magufuli ambaye hajawahi kuzungumza chochota mpaka sasa,Lisu haachi kumsakama.."nitoke vipi".
Wakati wa Kikwete,Lisu alifanya kupambana na Kikwete,kidogo mzee alikua anapiga vijembe vya hapa na pale.....ambavyo vilimuongezea Lisu umaarufu.

Zama hizi kidogo Chama na serikali zimejikuta zanawajengea watu umaarufu wa bure.
Mfano ishu ya Mange Kimambi,haikua ya kuipromote kiasi kile,ila serikali na chama wakajikuta wanaucheza wimbo na ngoma za Mange kama Chambua kama karanga wa Saida Karoli.

Zito,naye amepmbana na still anapambana,naye anapambana na mtu,na na serikali kwa mbaali,lakini naye bado ni "nitoke vipi".


Hapa pameibuka mwingine anaitwa Abdul Nondo,naye naona ameamua kufa na Yeriko Nyerere,bado ni"nitoke vipi".
Ukifuatilia yote haya na mengine mangi,utagundua kuwa watu wanataka kujibrand as a person kuliko taasisi walizopo.
Lisu anataka awe juu kuliko Chadema,Nondo anataka awe mwanaharakati kuliko wanaharakati wenyewe.
Nimejaribu kumuangalia Nondo hata kuongea anataka kuongea kama mtu fulani,mdomo utaumwa upande kila baada ya neno,shingo itapindwa kidogo,yote ni "nitoke vipi".

Ushauri wangu kwa sisi vijana,tujikite kwenye hoja,tusidandie mambo ambayo kesho ikipiti inapita nayo.
Tuwe wabunifu,wapo watu wakiongea unatamani aendelee kuongea,mfano Mbowe,sipo upande huo lakini bado ni mtu ninayemkubali akiongea. Rejea speech yake ya mwaka 2011 wakati wa kutaka kuteua mawaziri vivuli wa kambi ya upinzani,niliwaona hata viongozi wa chama changu kuwa nao kidogo hamnazo,hotuba ya Mbowe ilimaliza kila kitu.

Hata leo,ukimsikiliza Mbowe,bado ni materia kwa nchi hii.

Mungu awabariki sana.
 
Back
Top Bottom