Ni wiki moja sasa tangia nipost mada yangu ilikuwa na kichwa kisemacho,Abby nashukuru kwa yote.baada ya dharau nyingi na kejeri nimeamua kuukubali ukweli wa mambo kuwa nilichelewa kujua dhamira yako ya kuniahidi ahadi hewa.wana MMU kumbe yote hayo alikuwa akinitendea alikuwa ana shindwa animwagaje maana sikuwahi kumkosea hata ck moja,hivyo vile vituko vyake vya kutokupokea cm wala kujibu msg ilikuwa ni njia ya kunimwaga na sababu kubwa kumbe kapata mwanamke mwingine.hayo nimejulishwa na kaka yake baada ya mimi kumjulisha kuwa naona nipumnzishe akiri mbona mdogo mwenyewe haelewiki mpaka sasa,ndo akaniambia ana mshangaa sana mdogo wake kwani alimopita kunitambulisha mimi ndo anapita na mwanamke huyo kuwatambulisha na akiulizwa na vp kuhusu mimi anajibu mimi ni bahili.kitu ambacho sina kabisa hiyo tabia.kwakweli viumbe wazito wema wangu wote kasahau ananitafutia tabia ambayo sina,bado nakushuru lakini mema hukumbukwa mabaya hupita.sikujua kumbe ulikuwa na mapenzi ya pesa na si ya dhati.kila la kheli.