Kila la Heri....

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
KWa wagombea wote wa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Urais, kwa wanachama wote wa vyama vinavyogombea uchaguzi mkuu 2010, kwa wapiga kura wote waliojiandikisha na watakuwa vituoni wakipiga kura Jumapili, kwa Wananchi wote wa Tanzania walioko ndani na nje ya nchi. Mchungaji anawatakia KIla la Heri katika uchaguzi huu mkuu.

Jumapili hii tumia haki yako, iheshimu katiba yako, ilinde nchi yako, piga kura kwa kutumia moyo wako na upeo wako na si kwa vitisho au kurubuniwa.

Natanguliza hongera kwa wote watakaochaguliwa, nawapa pole wote watakao shindwa, naomba tuwe na utulivu kama tuna wasiwasi wa dhuluma au hujuma.

KIla la Heri ndugu Mtanzania.
 
Back
Top Bottom