Kila kitu kilichobuniwa kina mbunifu wake

Kila kitu kilichobuniwa kina mbunifu wake

Internal

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Posts
3,579
Reaction score
3,926
Ninaamini kabsa kila tunachokiona leo kimebuniwa.

Ni lengo kwenye shabaha moja kwa moja.

Muundo wa mwili wa binadamu unafanya iwepo haja ya kuwako mbunifu wake.

Wanasayansi wanatuambia kwamba ubongo wetu hukusanya na kukumbuka picha elfu nyingi katika mawazo yetu, huyaunganisha matatizo yetu yote na kuyatatua, hufurahia uzuri, huitambua nafasi ya mtu, na kutaka kukuza yaliobora ndani ya kila mtu.

Chaji za umeme zitokazo katika ubongo huongoza shughuli zote za misuli ya miili yetu.


Compyuta pia zinafanya kazi kwa njia ya mkondo wa umeme.lakini ilichukua akili ya mwanadam katika kutengeneza hio kompyuta na kuiambia lakufanya.

Si ajabu, basi, kwamba mtunzi wa Zaburi alihitimisha kwa kusema kwamba mwili wa mwanadamu unasilimulia habari za muumbaji wake huyo wa ajabu kwa sauti kubwa ilio wazi:
"Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu, wewe wanijua kabsa kabsa" Zaburi 139:14.

Hatuna haja yakwenda mbali ili kuyaona hayo matendo ya ya Mungu.

Umbo la ubongo wetu wenye sehemu nyingi za ajabu na viungo vyetu vingine ni matendo ya Mungu, nayo husonda kidole chake kwa yule mbunifu stadi kabisa.

Hakuna pampu yoyote iliotengenezwa na mwanadamu inayoweza kulinganishwa na moyo wa mwanadamu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom