Kila Jambo na Wakati Wake

Kila Jambo na Wakati Wake

Quartz360

Senior Member
Joined
Mar 27, 2023
Posts
133
Reaction score
318
Haya maisha hayahitaji unyonge hata kidogo. Itafikia hatua utahisi ya kuwa wewe ni fungu la kukosa siku zote.

Kuna watu ambao watawahi kupata pesa, kazi ama mafanikio ya aina yeyote ile, mapema zaidi yako wewe. Pengine inaweza kuwa ni watu wako wa karibu unaofanya nao harakati mjini, lakini unashangaa tu mwamba huyoooo kajipata, wakati wewe hali bado ni mbaya.

Bila kujua ya kuwa kila mtu ana wakati wake, unaweza kupatwa na magonjwa ya akili bure.

Tuendelee kupambana, lakini kamwe tusijilinganishe na watu wengine. Hata kama Leo itakuwa ni ngumu, huenda kesho tukatoboa.
 
Back
Top Bottom