chidy abidal
Member
- Mar 4, 2015
- 6
- 4
*KILA GARI NA PISTONI YAKE*
Anaandika Kibopa[emoji1621]
Siku za hivi karibuni imeibuka mijadala mbalimbali kuhusiana na matukio ya mauaji ya wapenzi ikihusishwa na usaliti wa kimapenzi huku hoja kuu ikiwa ni ‘kusomesha’. Taarifa hizo zikazua taharuki kubwa miongoni mwa wasomesha na wasomeshwaji, Basi kama ilivyo kawaida kikundi kidogo cha wahanga wakubwa wa taharuki hii (wanaume) wakakaa kikao na kutoa maamuzi kuwa ‘hatusomeshi’.
Wakati naendelea kutafakari maazimio ya hiki kikao cha wanaojiita wasomeshaji wale wanaosomeshwa hawakukubali kukaa kinyonge ndipo walipoanza kusambaza picha mbalimbali kwa makusudi kabisa zikiwa zimeacha sehemu nyeti zao wazi huku wakiuliza kwa ghadhabu ‘mtatusomesha au hamtusomeshi?’ nikasikia sauti toka kuzimu ikiniambia ‘hawa ndo wale wanadai haki sawa’ nachoshukuru niliipuuza kwa kuamini hakuna sukari inaweza badili ladha ya maji baharini.
Haya sasa nikarudi kwenye maazimio ya kikao kwamba ‘hatusomeshi’ kisha nikarudisha mawazo yangu miaka mitatu nyuma nikiwa chini ya mti pale Shule ya Kilimo Kilosa kuna Kaka yangu mmoja aliwahi kuniambia hakuna mwanaume fala mbele ya ‘wanaume wenzie’ nauona mpasuko mkubwa sana juu ya hili azimio.
Kwa mbali nauona mstari mwembamba sana kati ya ‘Mapenzi na Biashara’ nikipata mke mwema nitakuja kuwaeleza hili vizuri. Katika hili linaloendelea naona jinsi mapenzi yanavyofifishwa kwa kivuli cha mali. Kumuua mtu aliyekusaliti kisa umegharamia (elimu) ni sawa na Mjerumani aliyewaua mababu zetu walipotoroka utumwani, Hakukua na Mapenzi hapo maana msingi wa mapenzi ni maridhiano (sina Uhakika lakini) na hili pia nikipata mke mwema nitakuja kuwelezea.
Ninaposema kila gari na piston namaanisha kila mmoja amgharamie mpenzi wake kwa kadri ambavyo anaona anaweza, ‘wanawake wote ni sawa lakini hawafanani’. Usiache kumsaidia Mwajuma wa Tandale kwa sababu ya Caren wa Masaki.
Mnaposema wasisomeshwe ni kuzidhulumu nafsi zetu na zao pia, Pistoni ya IST huwezi kuifunga kwenye NOAH, Pistoni ya Range haiwezi ‘kufit’ kwenye HUMMER. Kila mtu ashinde mechi zake.
Kibopa: +255 715 685 395
rajabuathumani123@gmail.com