Kila Binadam amezaliwa na Jinn

Sidhani kama kila mtu anaiamini hiyo quaran kama kitabu kitakatifu...I,e jifunze kutafakari kwa fikra huru mkuu...wengine wanaona hicho kitabu kama cha hadithi tu

Ungetafakari kwa fikra huru ungeweza kufikiri na kupata fikra ni kwa nini Biblia ikabadilishwa na kuandikwa upya ilhali ni maneno ya MUNGU ambayo tayari ilishaandikwa ni kutoka kwa MUNGU iweje tena ibadilishwe kana kwamba ilikosewa kuandikwa. Fikiria tena.

Staki kuzama huko ukiona QUR'AN ni hadithi ni sawa tu ione hivyo lakini haitakaa ije kubadilishwa mpaka kinasmama QIYAMA coz ina walinzi ambao ntawaelezea hapa jukwaani very soon.

Utajua kama ni hadithi au laa.

Ahsanta.
 
Kwa hiyo tufanyeje? Na kama Mungu hakutaka twende kuangamia kwanini amuache hiyo sijui QARINI atuingilie na ashinde nguvu za Mungu?
hapana,hiyo imani labda kwa waislamu tu, mimi siwezi kuwa na ushirika wa aina yoyote na mashetwani

Hapo suala sio muislam au mpagani hili linaongelea binadam, labda kama utakuwa sio binadam lakini kama ni binadam yeyote yule ni lazma awe na huyu kiumbe. Period.
 
Mbona unarusha mawe gizani???...unafikiri nimeelewa chochote???...Ebu watu tutumie lugha zetu tuache kutukuza za watu.

Kwani lugha iliyotumika kwenye mada ni lugha gani, umeielewa ?.
 
Mkuu acha kuitumia Quran kuthibitisha uganga/unachoamini,hakuna kipengele kinachomtaja jini katika hiyo aya.Naamini wewe utakuwa miongoni mwa wanaomshirikisha Mungu kwenye uganga na kuamini majini pengine kuwa na urafiki nao kwa kujifanya mganga na kuagua au kupunga mapepo.Nakerwa na baadhi ya maustadh waganga kutumia kitabu cha Mwenyezi Mungu katika masuala yao ya kishirikina.Kama wewe unamshirisha Mungu basi utakuwa miongoni mwa waliopotea.Kama ni kweli taarifa hizi umezipata wapi au na wewe ni miongoni mwa wale kujenga urafiki na mashetani?
 

Ngoja nikwambie kitu.

Kumuelewesha mtu ambaye hajui na hajijui kama hajui ila akajijua kuwa anajua huwa ni ngumu sana kukuelewa mtu wa aina hii.

Wee tayari unajua kwa hiyo sina sababu ya kukujuza saaaana mjuzi kama wewe, ungetaka kujua ningekujuza mengi tu.

Siku zote ujanja ni kuacha ujanja ndipo unakuwa mjanja coz kuacha ujanja huwezi kuwa mjinga japo wengi hujifanya wajinga kwa kutaka kujua mengi kwa kuuliza japokuwa kuuliza si ujinga.

Pili, nashkuru kwa kauli zako na ALLAH akuzidishie moyo mwema na akuondolee kauli za kishetani autakase ulimi wako In Shaa Allah.

ALLAH ATUEPUSHE SOTE KWA PAMOJA NA MASHEYTWAAN NA SHIRK KWA UJUMLA.

AHSANTE NDG YNG.
 
Mtoa maada naomba uniambia ufafanuzi wa aya 51 ya suwratul Swaaffaaat
Hakika nilikuwa na rafiki (Qaala qaailun minhum in-niy kaanali Qariynun).
Umeitoa katika kitabu gani ambacho kinasema kuhusu qariynun na haya maelezo uliyotuma.

Nimetumia muda wangu zaidi ya masaa 12 kusoma tafsiri ya wanavyuoni mbali mbali kuhusu maelezo yako ya qariynun.
Nimeangalia tafsiri ya wanavyuoni kupitia www.altafsir.com
Ni wanavyuoni wa ulimwenguni waliopasishwa 86 na vitabu vyao, sikuona haya maelezo uliyoyaandika wewe.
Sasa naomba unipatie kitabu gani, mtunzi nani, anaeleZea hizi habari za qariyn ili nipate ufafanuzi zaidi.
Tukimalizana hapo ndio tutakuja kuelezana mengine zaidi,
Kwa wanajf kwanza tusibiri hili jibu
Ahsanteni
 
Hata ukimwambia mtu kuwa wachawi hutumia uume wa watoto wadogo kutengeneza filimbi unadhani ni wote watakuelewa...?

Wenye jicho tofauti kama sisi ndio tunaweza kukaa chini na kutafakari kwa upeo wa hali ya juu na kuweza kuelewa nini kinachoongelewa.
Sawa ila hiyo dhana yako kwamba MTU anazaliwa na jini ni uongo
 
kwa hio mitume wote wa kale kama Ibrahim, musa, solomoni(sulemani), muhamad na yesu nao walizaliwa na majini? maana wao pia walikua wanadamu, sio malaika wale.

au wao hawakuzaliwa nayo kwa sababu walikua chosen ones? acha PUMBALIZATION mzee.
 
kwanza nikupongeze kwa kutia Darasa kwa watu kuwa kumbusha Mambo Kadha wa kadha kuhusu Ibada na uasi Juu ya Mwenyezi Mungu kwa kufanya Mambo Yasiyo Mpa Mungu Utukufu kwa Kufanya Mambo kwa Uongozi wa Shetwani.

Ila nitoe Rai kwa wachangiaji, nikweli Kabisa kila Mtu Ana imani yake na Kitabu cha Imani yake. Kina Mfundisha naye Uamini kile Anachofundishwa kutoka Kitabu Hicho.

Hivyo Basi ni Busara Tukavumiliana Na kuchangia kwa staha bila Kuvunjiana Heshima, kuitolea Lugha ya kuudhi imani ya Mwenzako sio Jambo jema.

Mimi ni Mkristo lakini sifurahii kuona wengine wanatukana Imani za wengine yaani Mkristo kumkashifu Muislam hilo jambo halinibariki kabisa.

Maana hata Mtume Muhamadi alikiri kabisa kwamba Ndugu ya Muislam ni Mkristo.

Hivyo tuheshimiane hata Yesu Alisema Ndugu ya Mtu ni Jirani yake na sio wa Kuzaliwa naye. (Luka 10:25-37) tupendane kama Ndugu.
 

Mpumbavu wewe... Biblia haifundishi mtu akifa roho inaenda mbinguni, Biblia inafananisha kifo na usingizi hivyo wafu wamelala na wanasubiri siku Yesu akirudi ili wafufuliwe na kwenda mbinguni kama walitenda mema.... Na kwa waovu wao watafufuliwa ktk ufufuo wa mara yapili ili waangamizwe kwa moto na huo utakuwa mwisho wa dhambi na wadhambi.
Quran kitabu kilichotungwa na marehemu muhammad na majini ndio kina habari hizi za ushirikina...
 
sawa ustadh nenda madrasa sasa kafundishe.. huku wengine hatuelewagi hayo makitu.

Kasemaje.......?......
Jini labda anae mwenyewe.......
Wengine tuna Roho Watakatifu........na panga za moto......
 
Hapo suala sio muislam au mpagani hili linaongelea binadam, labda kama utakuwa sio binadam lakini kama ni binadam yeyote yule ni lazma awe na huyu kiumbe. Period.
hakuna kitu kama hicho shehe...usiwaaminishe wana wa Mungu HUU ONGO
 
Mara umuite JiNN mara qarin...inaonekana hujaelewa ulichosoma...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…