Kikwete: Waliokihujumu chama Uchaguzi Mkuu 2015 watakiona, majina yao ninayo

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Kikwete: Walioihujumu CCM 2015 kutumbuliwa

Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete amesema mwanachama yeyote aliyekihujumu chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba mwaka jana atatumbuliwa bila aibu huku akisema tayari wana majina ya wasaliti hao.

Chanzo: Mwananchi
 
chanzo: mwananchi

Kikwete: Walioihujumu CCM 2015 kutumbuliwa
===============================

Kwake yeye majina ya wahujumu chama ni hatari zaidi kwa Taifa kuliko majina ya wauza unga ambayo alisema anayo lakini hadi anamaliza muda wake hakuwahi kutaja hata jina moja.

Tumeshuhudia uozo wa kutisha ukifanyika katika awamu yake kiasi cha baadhi yetu kulihurumia Taifa kwa kukosa uongozi kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita,lakini yeye alikuwa 'bize'akishindana na ndege kuruka angani.Yapo wapi majina ya majangili ambayo nayo alisema anayo?Yapo mambo ya msingi ambayo yasiposhughulikiwa yanaweza kulididimiza Taifa,lakini si kuzuia Uhuru wa watu kikatiba kumuunga mkono na kumchagua kiongozi wamtakaye.

Kauli hii inapaswa kukemewa na wapenda demokrasia,kwani inakiuka katiba ya JMT ambayo inatoa fursa kwa mtu kumchagua kiongozi anayemtaka.Taratibu tunaanza kuwabaini wapumbavu halisi,baada ya kituita sisi ni malofa na wapumbavu.
 
Huyu bwana huyu hana zaidi ya majungu tu! Kila akiongea mambo anazungumzia majungu tu mara Jecha, mara wasaliti, yeye kama mlezi wa Chama haoni hata busara ya kuongelea kero za WaTanzania! Yaani sijui kichwa chake kinafanyaje kazi!
 
Back
Top Bottom