Kikwete: Uvumilivu sasa basi...


sera za majimbo ya chadema hiyo ndio inataka kugawanya nchi. nassari anataka kipande chake cha nchi, sugu nae, lema nae yaani hadi balaa
 

Sio jazba mkuu akiwaza 10% aliyokula ya wachina anachanganyikiwa kabisa mbaaba wa watu ,huku wanamtwara wanataka kumvua nguo
 
Anatoa maneno haya kisa ni Gas anataka aipeleke pwani ! Kwa nini hakusema haya Uamsho kule Zanibar walipokuwa wanachoma makanisa na wafuasi wa Shekh Ponde pale Mbagala .!!!?
 
Tatizo ni pale ambapo rasilimali zinapotoweka bila kumfaidisha yeyote..si kule zilikotoka wa taifa kwa ujumla...bali ni watu wachache tena ni walewale kila siku....
 
Katika kipindi cha uongozi wa Jk 90% ya nafasi za watumishi wakuu wa serikali ni Waislamu kwa Tanzania bara,100% Tanzania Zanzibar= Maaskofu.
 
Alipoingia madarakani mwaka 2005 alisema mwenyewe kuwa atamaliza kero zote za Muungano lakini jinsi muda unavyokwenda naona kero za Muungano zinazidi, taifa linazidi kuparaganyika na sasa zimeanza kero za Tanganyika. Mpaka 2015 tutaona kero nyingi sana zikiibuka na yote hayo yanasababishwa na aina ya uongozi uliopo aidha kwa kutojua ama kwa makusudi ili waendelee kujineemesha zaidi.
 
Tatizo ni pale ambapo rasilimali zinapotoweka bila kumfaidisha yeyote..si kule zilikotoka wa taifa kwa ujumla...bali ni watu wachache tena ni walewale kila siku....

... mkuu umenena.., asante kwa mchango wako mzuri.., hasa hilo ndilo tatizo kubwa kwa TZ. "ni walewale... Wana JK na familia yake"
 
Mleta mada umekaririshwa kukosoa,Jk yuko very right, kama ishu ni maendeleo wangezungumzia kupewa mrahaba wa gesi itayovunwa badala ya kulazimisha eti gesi ikichimbwa Mtwara watapata Ajira, kwan pamoja na wingi wa Viwanda vilivypo Dsm unaweza kuthubutu kusema vimewanufaisha wazaramo kiajira? Mnajua kuwa Mama Anna Abdala alipokuwa waziri wa Afya alijitahidi kupeleka NGO nyingi mtwara kuliko sehem nyingine yoyote hapa nchini lakini bado waliopata ajira ni watu wa maeneo mengine wenye sifa za ajira, Nani kakwambia gesi ikichimbwa mtwara Chale za usoni ndo itakuwa Qualification ya Ajira? Madini yanachimbwa shinyanga je kuna kitu cha kujivunia kwa wasukuma?. Kitu cha msingi ni uwepo wa uadilifu wa pesa itokanayo na gesi.
 
Kikwete huwa mara nyingi hajui anachosema. Kama kuna watu wenye hadhi tofauti kisheria kama akina Lowassa, Chenge na Rostam kwanini majimbo yasiwepo yenye turufu na yasiyo na turufu?
 
sera za majimbo ya chadema hiyo ndio inataka kugawanya nchi. nassari anataka kipande chake cha nchi, sugu nae, lema nae yaani hadi balaa

nchi imeshagawanyika mkuu unataka igawanyike mara ngapi ? kati ya walio nacho na wasio nacho ikiongozwa na jk mwenyewe jiulize kwanini ulipokuja mradi wa Bil. Bill Gates wa USA alimpeleka Bagamoyo na siyo Mtwara?? angalia
familia yake ni mabilionea lakini wewe anakupigia gitaa lake utaifa wakati anakula na familia yake. usisikilize maneno yao angalia vitendo vyao kama vinaashiria utaifa please let me know.
 
Hivi kwa nini mnakazana kuona kuwa ili ni suala la vyama vya siasa badala ya suala la kitaifa lisilokuwa na usiasa. Hivi kweli hatuoni huu uwekezaji wa jinsi hii na Menejimenti ya jinsi hii ya raslimali zetu itatupa tabu baadaye.
Hatujajifunza yanayotokea kwingine duniani - mfano wa rahisi ni Nigeria, tumekuwa tunayasikia haya tangu miaka ya 70! Kwa nini tusishauriane na kupata sera nzuri zaidi badala ya hizo command/order nzito?
 
Urais ni suala la kifamilia.
 

jawabu ni moja nalo ni sera mbaya za ccm ambazo zimetufikisha hapa tulipo kwa kuweka maslahi ya wawekezaji mbele kuliko watanzania wenyewe. kabla ya utekelezaji wa jambo lolote andaa kwanza mazingira yatakayowafanya watu wa eneo usika kufaidika na mradi kwa mfano ktk suala la gesi. toka gesi ivumbuliwe songosongo ni miaka 20 sasa kwanini mpaka hivi hatuna chuo cha oil and gas huko kusini ili kuandaa mafundi mchundo wa kuja kufanya kazi kwenye miradi hiyo. Lindi na Mtwara yako masekondari mengi andaa special program ya gas and oil kwy hizo sekondari za kuandaa vijana mazingira mazuri ya kuingia kwenye vyuo hivyo baadaye. unaposikia jk anawaambia watu wa mtwara wajiandae kufaidika na gesi bila kusema how ?? its a joke.
 
onyesha huo uoga na unafiki.
Mbona unaogopa sana suala la mjimbo kwani Tanzania ndo nchi pekee ambayo itakuwa inaendeshwa kimajimbo? kwani hakuna nchi zingine zenye majimbo? wapi ulisikia kuwa Lema anataka Arusha kama nchi? au wapi ulisikia Sugu anataka Mbeya kama nchi na hata kuyo Nassari aliwahi kutamka kuwa ikiwa hawajali watu wa meru basi tujue hatuna raisi na ijitenge hayo aliyazungumza kwa hasira baada ya kuona police ccm wanatumika kuua watu bila hatua kuchukuliwa. halafu hata vifo vingine vilivyo tokea vya utata hakuna ufuatiliaji! sas unaposema Oh sijui wanagawa nchi huo ni uafiki mkubwa
 
Aliyeanza kuigawa Nchi ni JK mwenyewe kwa kuendekeza uswahiba! Sasa hivi kila mtanzania anatamani kuandamana ili kutetea kilicho chake,Si ajabu kuona siku moja watu wa Chunya wakiandamana dhahabu ibaki kwao mpaka pale serikali itakapopeleka maji na barabara

Kwa hiyo JK aache kujiuliza maswali ya ajabu bali ajiulize,why uprising now? Kwa nini isiwe wakati wa Mwinyi au Mkapa? Why now? Majibu ni kwamba watanzania wamejitambua na wanataka haki zao! Ndio maana kuna mabango waliyokuwa waandamanaji yanasomeka Tanzania(Tanganyika) kwanza Mengine baadaye!
Pole sana Rais wangu,hiyo ndio hali halisi,.........!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…