Bahati mbaya sana makusudi rais as a stateman ameamua kusambaza siasa za tumbo. kwa kupotosha madai ya wanamtwara kwa kuamua makusudi kabisa kuchukua maana finyu ya madai ya wanamtwara kwa kusema eti wanataka gesi iwanufaishe wao tu. Kama hajapata nakala ya madai yao, apewe.
ukisema dar kuna viwanda na miundombinu iliyotayari kwa kutumia hiyo gesi, hiyo siyo sababu ya kufanya usafirishe hiyo gesi, kwa sababu hiyo miundombinu inayoongelewa sio kama mlima kilimanjaro, kwamba by nature they are there, ilijengwa, kwa hiyo, as long term plans za nchi, wekeni mitambo mtwara, viwanda vitajengwa. sio lazima vijengwe in two, three, etc years, inaweza ikawa hata baada ya miaka mitano, ishirini, hata dar hivi viwanda tunavyoongelewa havikuja siku moja, vimechukua muda.
All in all, wanasiasa hasa walioko madarakani, wasilete vitisho, bali wajibu hoja. maendeleo yanatakiwa yatoke kila kona ya nchi sio dar tu.