Kikwete: Uvumilivu sasa basi...

Kikwete: Uvumilivu sasa basi...

The Khoisan

Platinum Member
Joined
Jun 5, 2007
Posts
18,229
Reaction score
17,380
SERIKALI imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa mwaka jana.



Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.

Akizungumza na mabalozi kwa nyakati tofauti Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika juzi na alipokuwa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Corner jana, Rais Jakaya Kikwete alisema vurugu zilizotaka kujitokeza mwaka jana zinatosha.

"Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile, inatosha," alisema Rais Kikwete.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kiongozi wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi waJamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Juma Mpango alisema jumuiya ya mabalozi imefurahishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa ikishughulikia vurugu za kidini ambazo zilitaka kujitokeza bila kusababisha madhara kwa wananchi.

"Tumeridhishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa inashughulikia mambo yakevizuri. Tunaomba mwendelee kushughulikia amani ya nchi hii maana ndiyo mhimili wa nchi za Maziwa Makuu," alisema Balozi Mpango.

Kuhusu gesi
Rais Kikwete alizungumzia suala la rasilimali za taifa na kusisitiza kuwa pia hatavumilia kuona wanasiasa wakitumia suala la gesi kujitafutia umaarufu.

Wakati Rais Kikwete akitoa kauli hiyo jana, habari kutoka Mtwara zilidai kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amewekewa magogo barabarani kumzuia asiende kwenye kijiji kinachozalisha gesi hiyo, huku Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo akizomewa.

Hata hivyo, polisi walikiri wananchi kuweka magogo barabarani kwa lengo lakumzuia waziri huyo, lakini ikaeleza kuwa gari lililozuiwa siyo la Simbachawene.

Akizungumza na Balozi Corner, Rais Kikwete alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia suala la rasilimali za taifa, ikiwamo gesi asilia kujitafutia umaarufu wa kisiasa na kuwapotosha wananchi.

"Ni jambo la hatari na lisilo na tija kwa wanasiasa kujaribu kuigawa nchi vipandevipande kwa sababu ya kujitafutia umaarufu kwa kutumia rasilimali zataifa," alisema Rais Kikwete na kuongeza:

"Unawezaje kuwa na nchi moja na taifa moja wakati kila mmoja anadai rasilimali kutoka kwenye eneo moja ibakie na kunufaisha watu wa eneo hilo tu. Huwezi kuwa na nchi moja na yenye umoja wakati kuna nchi ya gesi asilia kule Mtwara, kuna nchi ya kahawa kule Kilimanjaro, kuna nchi ya chai na ndizi kule Bukoba," alisema Rais Kikwete na kuongeza:

"Kwa sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia na kunufaisha watu wa Mtwara tu, basi wenye haki zaidi ya kudai jambo hili siyo watu wa Mtwara, bali ni watu wa Msimbati ambako ndiko ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60 kutoka Mtwara, kilomita 200 kutoka Newala."

Source: Mwananchi
 
Hayo maneno tumeyazoea tokea semina elekezi zilizofanyika Ngurudoto mwaka 2005 sasa naona anayarudia tena mneno hayo baada ya miaka nane huku akiwa amebakiza miwili kabla ya kuwasili The Hague kujibu mashtaka yake

Mkuu The Hague tena.
 
huyo mwenyekiti kashachelewa asubiri miaka yake 2 iishe aende jera.
 
huyo mwenyekiti kashachelewa asubiri miaka yake 2 iishe aende jera.

Ina maana yeye na mtangulizi wake yeye ndio ana makosa? Mbona kasema 2013 ni kumalizia ahadi zake.
 
Na uvumilivu wetu kwa serikali hii isiyojali mnyonge sasa basi. Kubalini matokeo wakati wenu umefika kikomo. Hamuwezi tena kuwalaghai watanzania.
 
this is silly; amejuaje zinatosha? walikuwa na kiwango walichotaka kufikia au kulikuwa na kiasi ambacho kilikuwa kinaweza kuvumilika na sasa kimepitilizwa?

Anavuta shuka wakati kumepambazuka?? May be walikuwa wanatumia vipimo vya DRC, Somalia, Mali .............. a lot yard sticks to use against!!
 
Anatafuta huruma ya mabalozi, wakaadress kwenye nchi zao kuwa vyama vya upinzani vina ukabila na udini, wakati akijua kabisa ni yeye ndio mkabila na mdini
 
Hivi inakuwaje serikali kila siku haielewi madai na matatizo halisi ya wananchi:
ebu ona:

Walimu: Wanadai mshahara laki 3 serikali haina uwezo.
Madaktari: Wanadai mishahara mikubwa
Gas: Wanamtwara wanadai gesi watumie peke yao
Uswisi: Process ya kujua hao watu ni ngumu sana serikali haiwezi
Rada: Hakuna mtanzania aliyehusika
EPA: Waliochukua pesa warudishe
Umaskini: Sijui hata umaskini wa watanzania unasababishwa na nini
Wanafunzi: Mimba vihele hele vyao

Huyu ni daktari and great thinker.
 
Mwaka 2013 umeanza kama mwendelezo wa matukio ya mwaka jana2012 yani kila siku tukio laajabu chakushangaza serikali nikiziwi feki na yuko na mponyaji anaulizwa unataka kusia kiwizi anajibu ndio, kwni husikii anajibu ndio, yaani jk hana washauri bali anashauri tumbo tu, kwn kuhusu gesi jibu liko wazi wamtwara wanadai wapewe nafasi yakujengewa viwanda kuwe na maendeleo, ajira nahuduma za kijamii zitapatikana kupitia wawekezaji hapa jk ni jazba ndio zinamfanya asijue point na hata hiyo jojo the fighter blog walitoa siri kwanini wachina watadumu tz has mtwara.......yani makubalionamyakifamilia na nchi ya china mmh tanzagiza hiii.
 
“Kwa sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia na kunufaisha watu wa Mtwara tu,basi wenye haki zaidi ya kudai jambo hili siyo watu wa Mtwara, bali ni watu waMsimbati ambako ndiko ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60 kutoka Mtwara,kilomita 200 kutoka Newala.”



hv hili ni dai la msingi la wanamtwara kuhusu gasi?
 
Back
Top Bottom