Kikwete: Urais wangu hauna ubia

Kikwete: Urais wangu hauna ubia

Anko Sam

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2010
Posts
3,254
Reaction score
906
Baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 JK alipata kusema "URAIS WANGU HAUNA UBIA", maneno haya yalikuwa ni salamu kwa wanafiki na wapambe wote waliokuwa wanataka kumpangia wa kuwateua kwenye nafasi mbalimbali ama kumpangia atawale vipi nchi. Ndiyo maana wanafiki wa chama chake hawakutaka kabisa kuona mchakato wa katiba mpya unaanzishwa maana utasaidia kuondoa makosa yaliyomo kwenye katiba ya sasa ambayo wanafiki wanafaidika nayo.

JK alilazimika kuwaambia kwa uwazi kabisa "...wanafiki wote wajiandae kisaikolojia..." maana alijuwa Tume ya Jaji Warioba imesheheni maoni ya wanachi ambayo wao wanafiki hawayataki! Baada ya speech ile wanafiki walihararuki na kuanza kujipanga kuhakikisha mchakato wa awamu ya Bunge wanaumiliki wao. Nadhani kwa kutumia mbinu za kinafiki walimshauri JK ateue makada wa CCm kwa kupitia madirisha mbalimbali, mfano; waganga wa jadi, viongozi wa kidini, kundi la wakulima nk!

Hapa JK alizidiwa ujanja na mbinu za wanafiki kwa kudhani mambo yatakwenda sawia kwani hata baada ya UKAWA kususia Bunge, wanafiki walijuwa kwa umasikini wa watanzania, wajumbe waliotoka watarudi kufuata posho na hivyo akidi itatimia na Bunge la Sitta litaendelea kwa kufanya chochote wanachotaka kufanya.

Baada ya UKAWA kukataa kurudi Bungeni, ikaonekana katiba inayotungwa haina "maridhiano ya kitaifa" toka makundi ya kijamii katika Taifa, hapa ndipo JK akili ikamrudia, akagundua hila za wanafiki na akukumbuka maneno yake "URAIS WANGU HAUNA UBIA", juzijuzi kaongeza sentensi zingine "..ntakuwa Rais wa mwisho kutawala Tanzania masikini..." akatupia na nyingine "...Sitaki kuja kusutwa..." nk.

Ameamua liwalo na liwe ndipo kakubali kukaa na 'UKAWA' na kukubaliana na hoja zao. JK kawaacha hoi wanafiki wote wakiongozwa na Bingwa wao Samwel Sitta. JK kwa hila za wanafiki angelipeleka Taifa katika mchafuko ya kisasa ya muda mrefu. Kipindi chako kimekwisha tuachie nchi yetu salama.
 
Hyo Id yako ungebadilisha iwe mnafiki,manake kila baada ya neno moja unatamka unafiki,badilisha fasta
 
Ana paswa kujua kuwa nchi alikabidhiwa yeye na sio ccm wala nani sijui nani?.Kwa hiyo kitakachotokea atasutwa tu,so wafitini wote anatakiwa kuwablock mapema.
 
Kwani alikabidhiww nchi kwa tiketi ya chama gani? Au alikuwa mgombea binafsi?
 
Kikwete kwa kukubali kutumia mabadiliko ya katiba ya zamani ili kufanikisha uchaguzi mwaka kesho amekili kuwa Sitta na unafiki wake hawezi kupata katiba mpya bali ilikuwa uroho wa posho!! Sitta na genge lake watatoswa kiaina pale atakapokataa kuwaongezea muda!!
 
Baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 JK alipata kusema "URAIS WANGU HAUNA UBIA", maneno haya yalikuwa ni salamu kwa wanafiki na wapambe wote waliokuwa wanataka kumpangia wa kuwateua kwenye nafasi mbalimbali ama kumpangia atawale vipi nchi. Ndiyo maana wanafiki wa chama chake hawakutaka kabisa kuona mchakato wa katiba mpya unaanzishwa maana utasaidia kuondoa makosa yaliyomo kwenye katiba ya sasa ambayo wanafiki wanafaidika nayo.

JK alilazimika kuwaambia kwa uwazi kabisa "...wanafiki wote wajiandae kisaikolojia..." maana alijuwa Tume ya Jaji Warioba imesheheni maoni ya wanachi ambayo wao wanafiki hawayataki! Baada ya speech ile wanafiki walihararuki na kuanza kujipanga kuhakikisha mchakato wa awamu ya Bunge wanaumiliki wao. Nadhani kwa kutumia mbinu za kinafiki walimshauri JK ateue makada wa CCm kwa kupitia madirisha mbalimbali, mfano; waganga wa jadi, viongozi wa kidini, kundi la wakulima nk!

Hapa JK alizidiwa ujanja na mbinu za wanafiki kwa kudhani mambo yatakwenda sawia kwani hata baada ya UKAWA kususia Bunge, wanafiki walijuwa kwa umasikini wa watanzania, wajumbe waliotoka watarudi kufuata posho na hivyo akidi itatimia na Bunge la Sitta litaendelea kwa kufanya chochote wanachotaka kufanya.

Baada ya UKAWA kukataa kurudi Bungeni, ikaonekana katiba inayotungwa haina "maridhiano ya kitaifa" toka makundi ya kijamii katika Taifa, hapa ndipo JK akili ikamrudia, akagundua hila za wanafiki na akukumbuka maneno yake "URAIS WANGU HAUNA UBIA", juzijuzi kaongeza sentensi zingine "..ntakuwa Rais wa mwisho kutawala Tanzania masikini..." akatupia na nyingine "...Sitaki kuja kusutwa..." nk.

Ameamua liwalo na liwe ndipo kakubali kukaa na 'UKAWA' na kukubaliana na hoja zao. JK kawaacha hoi wanafiki wote wakiongozwa na Bingwa wao Samwel Sitta. JK kwa hila za wanafiki angelipeleka Taifa katika mchafuko ya kisasa ya muda mrefu. Kipindi chako kimekwisha tuachie nchi yetu salama.

sio 2010 ni baada ya 2005 alikuwa anawapasha waliojifanya wao ndio waamuz wa nn kifanyike badala ya yy
 
Harakati za kutafuta mgombea ndani ya chama,kupitia vikao vya chama bado kundi hili litakuwepo Dodoma.Rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama hawezi kukwepa kwani ni watu alishakuwa nao wakati yeye anawania kuingia madarakani.

Ndani ya vikao imekuwa vigumu kufanya maamuzi kwa sababu ya kuogopa kundi hili ambalo linalomzunguka Rais!!!,na hii imepelekea kusongeza mbele ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama,ikumbukwe miaka ya nyuma mwezi mei,mgombea wa CCM huwa anakuwa tayari keshajulikana.!
 
Back
Top Bottom