Kikwete, urais si umwinyi bali ni kuwajibika kwa wananchi waliokuchagua!

naninibaraka

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
910
668
Heri ya mwaka mpya mh mkuu wa kaya,napenda kukurudisha kwenye kwa kuwa umekuwa ukihama kwenye mstar mpaka wakati mwingine tunajiuliza kama kweli we ndo rais wa nchi hii,acha umwinyi wa kutoa maagizo bila kufuatilia.

Acha uvivu jitume kama rafiki yako Lowassa alivyokuwa anajituma bila kuchoka,watumikie wananchi,rudisha imani kwa watz kwani kwa sasa kura zikipigwa ni wazi unaelewa matokeo yatakuaje,usiwe kiongozi wa kuteua watu kwa kulipa fadhila,ni jambo la ajabu nilipita kwa mmoja wa mawazir wako nikashangaa anacheza karata ofisin,udhaifu huo unaanzia juu,ingekua mfuatiliaji mzur huyu wazir angekuwa busy na kazi..

Nawasilisha
 
Muache jamaa bwana, bado yuko likizo, c unajua alisitisha kwasababu ya matatizo yenu ya dar, funga mwaka kwenye speech akasema 'asiyesikia la mkuu, kuvunjika juu'. Alinimaliza kweli kwa hii statement, yaani watu wamefiwa na ndugu zao na vitu vimepotea, wee unaongelea wahenga.
Huyo ndo bwana mkubwa bana. Truly one of a kind
 
Lowassa alijituma katika kutuibia na kutupora...................akishirikiana na jk swahiba wake kupitia Ridhiwani................wote dugu moja hao............
 
Usiumie kwa vile ni jadi yetu: Tuna kumbukumbukumbu fupi sana na tukishapewa kofia, kanga, pesa, simun pombe na pilau basi tunakuwa hatujui kura zetu zina maana gani tena na hivyo kumchagua mfalme mwinyi wa kututawala badala ya lkumchagua kiongozi wa kutuongoza.
 
hatukumchagua, sisi tunajua na wao wanajua na yeye anajua pia kwamba tuko kwenye utawala wa ki imla, tunatawaliwa kwa nguvu na polisi na kutishiwa na Jeshi. Hatukumchagua yeye anajua hilo na sisi tunajua hilo pia
 
Lazima utakuwa una ajenda yenye manufaa binafsi hasa hapo ulipomfananisha Mndenge na Lowasa. Umenikata stimu
 
Back
Top Bottom