Kikwete, Tunahitaji FBI hapa!

Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,073
341
Albino auawa, wawili wakatwa viungo

albino_mtoto.jpg
Mwigulu Matonange (10) akiwa na baba yake Gimbishi.

KWA UFUPI
Katika matukio hayo, mtoto mwenye umri wa miezi saba alinusurika kuuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia nyumba ya mama yake usiku katika eneo la Lamadi, Wilaya ya Busega, Mwanza siku moja baada ya kupokea ujumbe mfupi wa simu kwamba mtoto wake anawindwa.

Vicky Ntetema
HALI ya wasiwasi imetanda miongoni mwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) nchini, baada ya watu watatu kukatwa viungo na mmoja wao kuuawa mwezi huu.

Katika miaka ya hivi karibuni, jumla ya albino 72 wameuawa, 34 wamenusurika, wengi wao kwa kukatwa viungo au kuumizwa. Makaburi 15 yamefukuliwa na viungo kuchukuliwa na kumekuwa na majaribio manne ya kufukua makaburi.

Katika matukio ya hivi karibuni, walemavu hao wakazi wa Tabora na Sumbawanga wamekatwa mikono ya kushoto. Ukatili huo safari hii umekwenda kinyume na ilivyokuwa mwaka 2010-2011 wakati mikono ya kuume ndiyo iliyokuwa inakisiwa.
Aliyeuawa ni
Lugolola Bunzari (7) na waliojeruhiwa ni Mwigulu Matonange (10) na Maria Chambanenge (39).

Marehemu Lugolola
Kijiji cha Kanoge kina umbali wa takriban kilomita 75 kutoka Tabora Mjini, barabara iendayo Ulyankulu kwenye machimbo ya dhahabu.
Imenichukua saa mbili na nusu kufika huko. Saa moja na nusu kati ya hizo, nilizitumia katika safari ya kilomita 15 tu kutoka Kanoge makao makuu ya kijiji hadi Kitongoji cha Kinondoni alikouawa mtoto Lugolola.

Nyumbani kwa Bunzari niliwakuta ndugu na jamaa kutoka vijiji vya jirani vya Wilaya hiyo ya Kaliua, Tabora. Bibi mzaa baba wa Lugolola, Gama Zengabuyanda (60), ndiyo kwanza alikuwa amerejea kutoka Hospitali ya Mkoa ya Kitete alikokuwa akitibiwa baada ya kushambuliwa na majambazi alipotaka kumwokoa mjukuu wake.

Huku akilia kwa huzuni, Zengabuyanda alinisimulia jinsi mjukuu wake na baba yake mzazi, Zengabuyanda Meli (95) walivyouawa kikatili.

Katika muda wa kati ya saa 10 na 11 alfajiri ya kuamkia Februari Mosi mwaka huu, Lugolola aliuawa kikatili baada ya kukatwa mkono kwa panga, kukwanguliwa nywele, kujeruhiwa mkono wa kulia na sikioni na kuondolewa ngozi kwenye sehemu ya paji la uso.

Katika mashambulizi hayo, babu yake Meli pia aliuawa alipojaribu kumwokoa mjukuu wake. Vilevile baba yake mzazi, Bunzari Shinga alijeruhiwa wakati alipojaribu kumlinda mwanaye.
Nilimkuta mama mzazi wa Lugolola aitwaye Kulwa akisaidiana na ndugu zake kumenya maharage mabichi waliyoyatoa shambani mwao muda mfupi tu uliopita.

Yeye ni mke mkubwa wa Bunzari Shinga (35). Walibahatika kupata watoto sita, wawili kati yao ni albino. Lugolola na marehemu mdogo wake aitwaye Maganga aliyefariki kwa malaria mwaka 2011.

Usiku wa mashambulizi hayo, Kulwa anasema alikuwa amelala na watoto wake wadogo wa kike (mmoja, Shija mkubwa) na Lugolola kwenye nyumba yake inayotazamana na ile ya mke mwenzake Pili, umbali wa takriban mita 20. Bunzari alikuwa amelala kwa mke huyo mdogo na binti yao mwenye umri wa mwaka mmoja hivi.

Mzee Meli alikuwa amelala na watoto wa kiume upande wa kulia wa nyumba ya Kulwa.
"Aliamshwa usingizini na kelele za watoto waliokuwa wakilalamika kwamba wanapigwa na fimbo. Alipotaka kwenda chumbani kwa watoto alishambuliwa kwa mapanga kichwani, usoni, mgongoni, mikononi na miguuni," Gama anaelezea huku akilia

Kutoka Gazeti la Mwananchi 27.02.13

Kweli hali inatisha! Serikali imeshindwa kumaliza ugaidi huu sasa ni lazima waombe FBI waje kufanya upelelezi! au huu sio ugaidi?
 
Nchi imekosa ulinzi. Nakumbuka enzi za mwalimu Watanzania walikuwa salama zaidi

FBI wenyewe wanashindwa kumaliza mauaji marekani .
Chicago ndo makao makuu ya mauaji duniani.
 
Wanaofanya hivyo ni watu wanajulikana, Serikali ikitangaza dau kubwa la kukamatwa hawa watu watakamatwa.
 
Kweli Wa TZ tumefika hapo! hatumtaji mhalifu mpaka tuhongwe! huo ni ufisadi na ukijumlisha na ugaidi huo jibu unalo wewe!
Kama Rais Kikwete ameweza kuleta FBI toka USA kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri sidhani kama atashindwa kuwaleta huku bara ili kunusuru roho za albino waliobakia ama kama haiwezekani nawashauri Albino wote wajisalimishe na kuomba hifadhi ktk ofisi za wakuu wa wilaya, mikoa na ikibidi ktk ofisi za Umoja wa Mataifa ili kunusuru maisha yao! na ni jukumu letu wa TZ kuwasaidia Albino ili wasalimike!

Wa TZ ni lazima tubadilike na tusingojee Serikali kumaliza tatizo hili naona kama Serikali imeshindwa kulinda roho za Wananchi wenzetu sasa naomba tuwasaidie wenzetu au sivyo wataisha!
 
Yawezekana watu walioko serikalini wanahusika ndo maana wako kimya? Ama wahusika wanalindwa? sina hakika....lkn umetoa angalizo zuri la kufanyia kazi sio kuishia JF tu...anza wewe, familia yako, waambie majirani zako....tuko wengi, tutafika!
 
Wanaopatikana na hatia wanyongwe!

Mkuu, kuna sheria ya ugaidi iliyopitishwa na Bunge mwaka 2003 na kama ikitumika inaweza kupunguza kasi ya mauaji ya Albino! lakini kwanza ni lazima Serikali itangaze kuwa kuuwa au kumkata viungo Albino ni Ugaidi!
Sheria nyingine ni ile ya kumnyonga muuaji! ila sikubaliani na wewe kumnyonga kila mhalifu hata kama amenyofoa mkono mmoja! hiyo sio haki! anaeuwa na yeye auwawe!
 
Muuaji auliwe,anaemkata mkono nae akatwe,anaekata mguu nae akatwe.Waganga (wachawi,washirikina,wapiga ramli)wote wakamatwe na ipigwe marufuku kwa yeyote mwengine na tuishi kwa kumtegemea mungu muumba.Maana huu ni upumbavu na uonevu mkubwa wanaopata hawa watu.Hao waganga ama ndio wachawi tuwaite siku hizi wanajipatia ajira zisizo halali kwa kuwasaidia watu kinyume na sheria.Utamkuta mpaka jambazi linakwenda kwa mchawi amsaidie kazi yake ya ujambazi iende vizuri.Ndio maana Taifa halifanikiwi kutokana na njia za shot cut kuwa ndio tegemezi.:A S 39:
 
Rais piga marufuku uganga wa RAMULI

We unaweza kupiga marufuku hewa ya oxygen isipatikane humu duniani? likitokea hilo na wewe si utakuwa mmojawapo wa waathirika? kwahiyo kufuta uganga wa Ramli prezdaa hawezi coz na yeye anategemea mumo humo
 
Tumefika mahali pabaya sana, hizi Imani ya kwamba ili ufanikiwe haraka ni lazima upate Viungo vya Binadamu mwenzako ni mbaya sana. Dawa ya kufanikiwa ni kufanya kazi kwa bidii, ku save kidogo unachopata, kuweka akiba na mambo mengine muhimu.

Nchi imekosa ulinzi. Nakumbuka enzi za mwalimu Watanzania walikuwa salama zaidi
 
Damu inayomwajika juu ya ardhi ya Tanzania juu ya mauwaji haya itatucost sisi wenyewe kama taifa. Kilichopo tutubu ili tupate kupona. Kwani damu hii inalia mbele ya uso wa Mungu kama tunakumbuka vizuri kisa cha kaini na Habeli kwenye bibilia. (Mwanzo 4: 8-15)
8. Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]. Walipokuwa uwandani, Kaini akamshambulia Abeli ndugu yake akamwua.
9. Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
10. Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
11. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;

Nawashauri Albino wote TZ wajisalimishe ktk Ofisi za wakuu wa Wilaya, mikoa na ofisi za Umoja wa Mataifa ili kunusuru maisha yao!
 
Back
Top Bottom