kwa ufupi ni kwamba Rais hana uwezo wa kuwafukuza mafisadi.Angekuwa na huo uwezo angeshawafukuza. Yaani Kikwete anafanya kazi kwa ushikaji na watendaji wake,hadi watu wapige kelele ndio anashtuka?Utendaji gani huo? Kinachonishangaza ni taarifa ya Ikulu kwamba Kikwete asihusihwe na Richmond.Tusipomuhusisha Kikwete,tumuhusishe nani? Hata kama Kamati ya Bunge haikumuhusishaa,bado anapaswa kuwajibika kuwachukulia hatua wahusika. Hata baada ya Bunge kuchunguza na kubaini ukweli,bado Kikwete akawa mzito kuwachukulia hatua watuhumiwa. Baada ya mawaziri wake kujiuzulu,Rais alionekana kusikitishwa na hatua hiyo.yaani badala ya kusikitishwa na ufisadi uliotokea kwenye mkataba huo,Rais alikuwa anasikitishwa na mawaziri wake kujiuzulu.,isitoshe, Rais ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri,tamko lolote la serikali linatolewa na Waziri,lazima liwe limeidhinishwa ma Mwenyekiti wa Baraza hilo au tuseme limepata baraka za Rais.Kwa hiyo tamko la kuwasamehe Hosea na Mwanyika lilitolewa na Waziri Ngeleja lilipata baraka za Rais Kikwete..mi naona tusubiri Novemba tuangalia maamuzi ya RAIS..wizi mtupu...