Kikwete Sio Mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Sio Mungu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Majasho, Aug 5, 2009.

 1. M

  Majasho JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nawaomba watanzania wenzangu tuondokane na dhana kwamba rais ni kama Mungu kwa hiyo hasogelewi wala haguswi kwa maana ya kukemewa. Woga huu ndiyo uliotufikisha hapa tulipo na mambo kuharibika huku tukiona na kujua ni nani anaharibu lakini tunakaa kimya eti kwa sababu tunamuogopa mjomba,huo si uzalendo. Kwa walio madarakani kama mtamuonea haya Rais Kikwete kama mnavyomuonea haya Rais Mstaafu Mkapa,eti kwa sababu mtapoteza mkate wenu wa kila siku,basi hamuitakii mema Tanzania na ubinafsi utawahukumu. Na kwa mpendwa Rais,lionee huruma taifa lako hakika linaweza kuangamia likiwa mikononi mwako kama utakwenda na mwendo huu wa sasa. Wanaokupigia makofi,wanakupongeza sasa utambue kuwa wengi wao wanakupaka mafuta kwa mgongo wa chupa huku wakijua fika kuwa mambo hayaendi sawa. Usimuonee haya mtu yeyote, chonde chonde nchi inakwenda pabaya. Mafisadi wanakudai nini kiasi cha kuwaogopa hivi!!
   
 2. m

  maembe Member

  #2
  Aug 5, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi alivyosema watanzania tuache kununua magari ya kifahari tununue matrekta cjajua anaanisha nini!!
  kwani yeye na serikali ndio wanunua ji wakubwa wa magari ya kifahri ya pesa nyingi na wanayatumia kwa muda mfupi utaona yamebadilishawa kwa nini serikali isinunue matrekta kwanza !
  ili sisi tukiona mfano ndio tuanze kufata nyayo au sisi ndio wakupanda matrekta wao ni kununua mashangingi ?? cjamfaham mweshimiwa namaanisha nini bado
   
 3. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Nafikiri viongozi waandamizi ndio wanamuona kama Mungu. Kila swali linalohitaji jibu, either mpaka Rais atoe uamuzi au Rais ndio alitoa uamuzi. Sasa unajiuliza, "Rais alikuteua kushika wadhifa wa wizara, mkoa, wilaya, au idara ufanye kazi gani?"

  Kwa nini alionee huruma? Ni wajibu wake na aliapishwa kutumia katiba ya nchi kuwa atalitumikia Taifa na kulilinda kwa kufuata hiyo katiba. Hili suala la kulionea taifa au viongozi huruma ndio lililotufikisha hapa. Sidhani katika katiba ya nchi kuna kifungu kinachosema kuwa Rais anaweza kuonea watu, idara, rasilimali au nchi nyingine huruma. Ninachujua mimi, ni wafungwa peke yao ndio wanaonewa huruma tena baada ya kusota mvua kadhaa, na evaluation yao baada ya hizo mvua.

  Kwa hiyo hao mafisadi kwanza lazima wafikishwe mahakamani, wale mvua na baadae ndio tufikirie kama wanahitaji kuonewa huruma.

  Nchi haiwezi kuendeshwa na "Mama Huruma"
   
 4. O

  OLIVO G. M Member

  #4
  Aug 5, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu ndugu kasema kweli Rais Siyo Mungu
  Lakini inabidi awe na uchungu na watanzania. Jaribu kuona sasa watanzania wanaotumia Reli wanavopata shida. Rais kama mwenye Nchi angeweza kuamua wahindi hawa waendeleze Reli zote ama sivyo tuna rasilimali watu Kibao Tanzania waendeshe.
  Je, Na hawa mafisadi aliowateua yeye mwenyewe, ameshindwa kuwawajibisha hadi watu wake wanaanza kumtetea kinamna ile! Kimsingi anahitajika kuwaonea huruma watanzania.
  Kwanza, watanzania wenye Uwezo wa Kuongoza Takukuru ni wengi Hivyo Hosea amwondoe huyo siyo Mungu.
  Pili, wote waliotuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo awaondoe au awabadilishie kazi na wengine wenye nia hiyo hawatafanya hivyo.
  mikataba kama ya TRL aamue yeye ndo mwenye nchi, hawa wahindi wanatuhuma ya kuwatesa watanzania kwa usafiri hivyo wafukuzwe na kushtakiwa.
  Tatu, Afanye ufuatiliaji kama alivyofanya mara tu baada ya kuchaguliwa. Ilipendeza na watu tulifurahi.
   
 5. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,372
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wacha niendelee kufanya observation kabla ya kutoa maoni yangu
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni Chaguo la Mungu ndivyo makasisi walivyomnadi labda tuwaulize hapa kama wapo watuelezee namna walivyoshushiwa maelekezo na roho mtakatifu au ni mawazo yao binafsi.
   
 7. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2009
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kama wananchi walimchangua raisi ni budi raisi wahatumikie, na sio wanamnchi wamtumikie na kumwogopa. Tanzania tunasema kunademocracy lakini ni reality hamna. Ni tabia yetu watanzania kuwaogopa wenye hela na maulaka ya nchi! sijui kwanini? we cant stand by our values and dignities
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  Si mlisha ambiwa kwamba Mungu si Athumani!!! Sasa haya ya Kikwete siyo Mungu yanatoka wapi? Nafikiri hayo ni mawazo binafsi. Watanzania wengi tunajua kuwa JK siyo Mungu. Yeye mwenyewe anawaogopa mafisadi. Sasa yeye na mafisadi nani zaidi?????
   
 9. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2009
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa ndio hapo swali linakuja kwanini anaogopa mafisadi? wakati wnanchi ndio tulimpa kura zetu!
   
 10. M

  Majasho JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kwa ufupi ni kwamba Rais hana uwezo wa kuwafukuza mafisadi.Angekuwa na huo uwezo angeshawafukuza. Yaani Kikwete anafanya kazi kwa ushikaji na watendaji wake,hadi watu wapige kelele ndio anashtuka?Utendaji gani huo? Kinachonishangaza ni taarifa ya Ikulu kwamba Kikwete asihusihwe na Richmond.Tusipomuhusisha Kikwete,tumuhusishe nani? Hata kama Kamati ya Bunge haikumuhusishaa,bado anapaswa kuwajibika kuwachukulia hatua wahusika. Hata baada ya Bunge kuchunguza na kubaini ukweli,bado Kikwete akawa mzito kuwachukulia hatua watuhumiwa. Baada ya mawaziri wake kujiuzulu,Rais alionekana kusikitishwa na hatua hiyo.yaani badala ya kusikitishwa na ufisadi uliotokea kwenye mkataba huo,Rais alikuwa anasikitishwa na mawaziri wake kujiuzulu.,isitoshe, Rais ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri,tamko lolote la serikali linatolewa na Waziri,lazima liwe limeidhinishwa ma Mwenyekiti wa Baraza hilo au tuseme limepata baraka za Rais.Kwa hiyo tamko la kuwasamehe Hosea na Mwanyika lilitolewa na Waziri Ngeleja lilipata baraka za Rais Kikwete..mi naona tusubiri Novemba tuangalia maamuzi ya RAIS..wizi mtupu...
   
Loading...