Kikwete - Polisi acheni kuua na kutesa raia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete - Polisi acheni kuua na kutesa raia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Mar 8, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete akiwasili Chuo cha Polisi mjini Moshimkoani Kilimanjaro jana
  kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi cha Polisi.


  Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete, amelitaka Jeshi la Polisi kukomesha vitendo vya mauaji, unyanyasaji dhidi ya raia na ukiukaji maadili miongoni mwa askari kwani vitendo hivyo vinalipaka matope jeshi hilo. Kadhalika amelitaka kuwaelimisha askari wake na kuingiza kwenye mitaala ya vyuo vya polisi nchini somo la haki za binadamu, kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa raia ya kuuawa na kufanyiwa vitendo vya kikatili wakiwa mikononi mwa polisi.

  Rais Kikwete alitoa rai hiyo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa maboresho wa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Chuo cha Polisi Moshi (CCP). Alisema malalamiko ya raia juu ya vitendo vya kuuawa, kunyanyaswa, kubambikiwa kesi matumizi ya nguvu kubwa, kusababisha raia kujeruhiwa na kupoteza maisha pamoja na kuteshwa wakiwa chini ya mikono ya Polisi si vya kupuuzwa hata kidogo, hivyo Jeshi hilo linapaswa kujitizama kwa jicho pevu.
  Alisema taarifa mbalimbali za Tume za Haki za Binadamu za ndani na nje zimekuwa zikiyaeleza hayo kuwa yanafanyika, hivyo ni vyema wakatumia mkutano huo kujadili kwa kina na kutoka na mazimio ya kukabiliana na hali hiyo, ili wananchi waendelee kuwa na imani na Jeshi hilo.

  “Ipo haja ya kuwaelimisha askari kutumia elimu na akili zaidi kuliko nguvu kubwa, maneno yanayosemwa na raia si ya kupuuzwa yatageuka kuwa kero na kuwafanya mshindwe kufanya kazi zenu vizuri, kuweni na utaratibu mzuri wa kupokea kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi,” alisema na kuongeza: “Msiwapuuze, mkiwa karibu nao na kutunza siri watawapa taarifa nyingi na kuwa na imani nanyi, vinginevyo italeta matatizo sana, hawapati ushirikiano hadi wananitumia ujumbe mfupi wa simu nami namtumia IGP.”

  Aliongeza kuwa Jeshi hilo linapaswa kujisafisha dhidi ya malalamiko ya rushwa, kwani utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utawala Bora umeonyesha kuwa linaongoza kwa maofisa na askari kuomba rushwa na kwamba taarifa hizo zisipuuzwe bali zifanyiwe kazi, ili kuwaondoa wale wote wanaosababisha Jeshi hilo kuanza kupoteza imani kwa raia. “Tumieni njia zenu kuwatambua wale ambao wanapokea rushwa, wawajibishwe kwa mujibu wa sheria zilizounda Jeshi la Polisi, kwani wanakwenda kinyume cha maadili na ndio wanaosaidiana na wahalifu na hivyo kulichafua Jeshi hilo na kulikwamisha katika utekelezaji wa majukumu yake,” alisema.

  Aidha, Rais alilitaka Jeshi hilo kuweka utaratibu wa kuwafuatilia kwa karibu askari wake kama wanaishi kwa nidhamu inayotakiwa, kwani wapo ambao ni walevi kupindukia na utovu wa nidhamu mwingine, kiasi cha raia kuona kila anayevaa vazi la Polisi amechafuka kwa rushwa, utovu wa maadili na mambo mengine machafu. “Kuweni na utaratibu endelevu wa ndani kuwafuatilia askari wenu wakati wote, kuwatazama kabla ya kuwaingiza kazini, inapotokea askari anaonekana kuwa na mienendo yenye kutia aibu aitwe na kuonywa na akiendelea hatua ya kufukuzwa mara moja ifuate,” alisema na kuongeza: “Unakuta askari anakaa baa hadi usiku wa manane akiambiwa atoke ifungwe anajitapa yeye ni ofisa wa polisi hawezi kukamatwa, hili ni tatizo anachafua sifa nzuri mliyonayo, mfukuzeni.” Alisema nidhamu ni sifa ya msingi kwa askari, hivyo kwa wale ambao wameshindwa kufuata maadili ya kazi yao waondolewe mara moja, kwani haina maana polisi kuwa na mavazi mazuri, lakini tabia yake ni yenye kulichafua jeshi hilo.

  MADEREVA WAKAIDI WAFUTIWE LESENI
  Kuhusu kukithiri kwa ajali za barabarani, alilitaka Jeshi hilo kuwafutia leseni madereva wasiotaka kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani, kwani ajali kwa sasa ni tishio kiasi cha kukaribia kuwa janga la taifa. “Ajali zimezidi zinaweza kuzuilika zisifikie kuwa janga la Taifa, fanyeni kila njia kupunguza, zamani chanzo kilitajwa ni ubovu wa barabara sasa barabara zetu ni nzuri na ajali ndio zinaongezeka, madereva wanalalamikia matuta, hatutayaondoa hadi hapo madereva watakapotaka kufuata sheria na kuendesha magari kwa nidhamu,” alisisistiza.

  UHALIFU UDHIBITIWE
  Kikwete alilitaka Jeshi hilo kuongeza mikakati na mbinu za kukabiliana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na kutumia rasilimali zilizopo katika kutoa elimu kwa askari wao juu ya mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu kama wa fedha chafu na ugaidi.
  Alisema matukio makubwa ya jinai yamepungua kutoka 94,390 mwaka 2010 hadi 76,052 mwaka 2011, na kwamba bado idadi hiyo ni kubwa na serikali itaendelea kuwasaidia kupata vifaa vya kisasa, magari na zana zote muhimu, ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika mafunzo ambayo ndio msingi wa weledi wao. “Dunia ya sasa imebadilika na Tanzania imebadilika pia, mbinu za uhalifu zimebadilika, Polisi wanahitaji mafunzo yatakayoendana na dunia ya utandawazi, ambako kuna uhalifu unaofanywa kupitia mitandao na simu za kiganjani,” alisema Kikwete. Alisema serikali inaendelea na mpango wa kuboresha makazi ya askari na kwamba kwa sasa ipo kwenye majadiliano na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili wapunguze riba ya mkopo ili waweze kukopa zaidi ya Sh. bilioni 100, ikiwa ni pamoja na kujadiliana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Magereza kupunguza gharama za ujenzi.

  KAULI YA WAZIRI NAHODHA
  Awali, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Naodha, alisema mkutano huo una lengo la kujadili, kutathmini mafanikio na changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, ambao unategemea weledi, umahiri, utii kwa maafisa wa jeshi hilo.
  Alisema nguvu ya Jeshi la Polisi inategemea umahiri wa kazi na si wingi wa fedha wala nyezo na kwamba lina uwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu hayo.

  IGP: TUMEANZA KUJISAFISHA
  Wakati Rais anaendelea na hotuba yake, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, alisema tayari hatua zinachukuliwa kwa askari ambao wanakwenda kinyume cha maadili ya kazi zao kwa kuwaondoa kazini baada ya kukutwa na makosa.
  Mwema alisema mkutano huo utajadili wapi walipofanya vizuri na walipokosea kwa ajili ya kurekebisha kwa kupata mrejesho kutoka kwenye vituo, wilaya na mikoa ili kuboresha na kuidhinisha mikakati ya utekelezaji.
   
 2. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duh! Sasa serikali si ndio inayoagiza polisi kuua na kubambikia raia kesi? Rejea matukio ya arusha, mbeya, songea, kibaha mjini, tanga, pemba na kwengineko! Rejea malalamiko ya Mzee mengi kwa jeshi la polisi, Dr mwakymb, ishu ya Manumba!
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama kawaida yake anajitakasa aonekane yuko safi, na kwa mtindo huu wa kutoonekana wazi anawavisha lawama aliowapa majukumu.
   
 4. N

  Njele JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hili Kikwete amenena
   
 5. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,173
  Likes Received: 1,175
  Trophy Points: 280
  Simwamini kabisa mtu huyo" mimi niliye mgonjwa mtarajiwa naunga mkono mgomo halali wa ma dr"
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yametokea mauaji huko Songea wakati yuko UK, wazungu hawana aibu kwa vyo vyote walimwuliza kulikoni, alivyoumbuka ameamua kujioshwa kwa kutamka hadharani ingawa si ya kutoka moyoni, Kwani kama yangekuwa ya moyoni kwa nini alinyamazia siku zote hizi hata aibu ya polisi kutelekeza maiti barabarani?
   
 7. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Huko Policy Academy nasikia kuna kozi maalumu wa KUOMBA OMBA maana vijana wetu wakitoka huko wanakuwa mahodari. Nasikia ndio course wanayoipenda na kufaulu kuliko zote!
   
 8. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kagasheki nakumbuka alikana bungeni juu ya uwepo vitendo kama hivyo ktk jeshi la polisi,haya sasa boss wake kamuumbua!
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  aaaaaarrrgh ndo maana siingiagi jukwaa hili..........

  yaani badala ya kutake action anatoa rai?


   
Loading...