kikwete ongea na watendaji sio wazee!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kikwete ongea na watendaji sio wazee!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chizi1, Mar 10, 2012.

 1. chizi1

  chizi1 Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio sikatai ilikua tangu enzi za mwalimu, alikua akiongea na 'wazee wa dar es salaam' na kwa jambo lolote kubwana tz, lilikuwa linapitia kwa hawa wazee. Na imekua mfano kwa viongozi waliofuata mpaka sasa. Lakini mda sasa umebadilika, enzi za mwalimu, wazee hao ndo walikua wakisambaza news nchi nzima, wazee hao ndo walikua wakituhabarisha vigengeni na mitaani,wazee hao ndo walikua na influence kubwa kwasababu walikua wanaheshimika sana. Na nakubaliana na hayo mia mia kwa kina nyerere hadi mkapa kutumia huo mfano.

  Lakini ndugu zangu, wakati umebadilika, hawa wazee hawana mvuto wala hawasikilizwi nchini hapa, hawawezi kumchallenge rais wala kupinga akisemacho.dunia imebadilika technology iko mikononi kwenu, enzi za mwalimu ilikua kwa kutumia wazee ndo habari zinafika nchini nziman, sasa ivi tv,radio,magazeti, internet na simu zinasaidia sana kusambaza kote. Ni mara kumi angeita waandishi woote nchini wa habari.
  Kama kweli rais anajambo kubwa na la muhimu sana kutwambia ni bora angeita vikundi vinavyoheshimika nchini, angeita marais wa vyuo vikuu hapa nchini,angeita viongozi wa vyama hapa nchini, angeita wakuu wa mikoa, angeita mabalozi wa nchi,wakurugenzi mbali mbali kwenye sekta ya kilimo, afya e.t.c.hapo angeweza kuaddress na muonekano ukaheshimika zaidi ya kuwaita hawa wazee ambao siku izi hawana ajira, hawana influence na kujichekesha mbele yao. Kama jambo anataka liwe concrete na litendeke nchi nzima, angetumia vigezo ivyo na ikiwezekana atoe nafasi za kuuliza maswali machache. Ingelete changamoto zaidi na tungemuheshimu zaidi.
   
Loading...