Kikwete ndie aliyembeba Lowassa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ndie aliyembeba Lowassa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Apr 26, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145

  Kikwete ndie aliyemmbeba Lowasa na hivyo hivyo, ndivyo hatakavyo mdondosha.

  Japo jamaa yake huyo anakusudia adondoke nae,na kwa kuwa yupo aliyemjenga mwenzie, huyo aliyemjenga mwenzie ndie atakae mmbomoa mwingine kwa kuwa anajua wapi alisimamisha nguzo zake za kumjenga.

  Na tayari tukianzia miaka mitatu iliyopita,mwenye uwezo wa kumparua mwenzie alishaanza kufanya.Na kwa kuwa cheko lake uwaponza wengi wakiona ni mzaa kumbe....................Ukizingatia alishasema jamani msinione nacheka.


  Uwa sipati picha kuwa kuna watu wanaamini Rais Kikwete alibebwa na L, wakati ukweli ilimgharimu Kikwete kiasi kuwa, kumbe angelisikiliza ushauri siku hizo kuwa mdau jamaa aliyepembeni yako hafai usisafiri nae haya yote ****** huyu wa watu yasingemfika.Mwaka 1995 wakati anagombea mimi nilikua Shule ya Sekondali nilikua nampenda sana kama kiongozi ukichanganya na umri kuwa ni mtu aliyekuwa amechanganyikana na usasa [kukubalika na kizazi kipya].

  Baadae hata 2005 bado nilimuona katika picha ileile ya 1995,lakini magazeti yanavyompamba kuwa yeye na L anaonekana kama yeye amefaidika zaidi kuwa madarakani kwa kubebwa na L, kumbe sivyo.Aliyefaidika na mwenzie ni L,kwa kujua huyu jamaa ni LULU kwenye jamii [Kwa waliopitia College Politics wanajua hili],nikiongozana nae upepo wa Bata utanidondokea.

  Kikwete ni karasmatiki [Charasmatic] na anapendwa na kwa hilo uwezi kumnyanganya daima, ataharibu kwa jamii, lakini bado kuna watu wataendelea kumpenda,mfano wa watu wa karismatiki ni kama Augustine Lyatonga Mrema,Barack Obama. Obama alipewa tuzo ya mshindi wa nobel akastuka kipi kikubwa kafanya kustahiki tuzo hiyo kubwa duniani. Kumbe kazi kubwa aliyofanya ni kuifanya dunia kuwa moja wakati wote wa uchaguzi wa Rais Marekani,hata waarabu waliokuwa wameanza kuzidisha uadui dhidi ya Taifa la Marekani wote walibadilika na kuanza kushabikia ujilio wake wa kuwa Rais wa Marekani.

  Kwa watu wenye falsafa kubwa dunia kitendo cha Barack Obama kuiweka dunia pamoja kwa sababu ya karismatiki yake wanapata maudhui [Concept] nini cha kufanya kuiendesha dunia chini ya mhimili mmoja.Hivyo watu aina ya Kikwete wajanja wakijua kuwa huyu ni UA linalonukia watakaa karibu ili wanukie nalo.

  Ndio maana watu wengi walipiga kelele ya kuwa Serikali yake imejaza marafiki zake,yeye kama binadamu nae alilewa na genge la watu waliomzunguka akifikiria wote ni wasafiri wa meli moja. [Kumbe kwenye msafara wa mamba kenge nao wapo] amekuja kustuka amechelewa, ingawa is not too late.

  Anamilki kila chochote cha kuweza kuludisha karistimatiki yake kuludi kazini, lilipo kuludisha matumaini ya watanzania kwa vitendo halisia na mstakabali mzima wa kauli mbiu yake ya maisha bora.

  Kosa lake angesikiliza mapema ushauri wa ndugu zake wakongwe kuwa huyu mdau wako yuko kimaslahi zaidi, nafikiria angekuwa na yeye nyuma ya Mwalimu kuwa baada ya utawala wake anaacha legacy.Matokeo yake hata yule ambae yeye ilimgharimu kumtetea kwa msimamo wake wa kungangania kuongozana nae katika kuwaongoza watanzania leo hii anaonekana ni mchapakazi halisi zaidi ya yeye.Kwa kuwa tu ni aina ya watu wenyekufanya vitu kupita magazeti [Publicity].

  Kama rafiki yake si kuwa hakutoa michango yake kumsupport [friend in need is a friend in .....], and thats what friends are.....Lakini yeye Jakaya Kikwete kama muhusika mkuu ilimpasa kuwapima wale wote waliomzunguka kuwa je wanastahiki kuingia nae nyumba takatifu pamoja na ushauri wote aliopewa.

  Tena ilikuwa kosa kubwa sana kumtumia yeye kama kiongozi wa kampeni [hivi jamani kinana alikua wapi?],manake haya matumizi ya pesa yanayowaumiza kichwa [EPA] na hakika TUHUMA hizi kama kampeni zingekuwa chini ya Kinana yasingetendeka haya. I appriciate that old man is smart on that side of the campaign. He has that talent and skills to draft the so called political campaign.

  Kulikua hakuna sababu ya matumizi ya makubwa ya pesa ya EPA., kwa mteule aliyekuwa ameshakubalika ndio maana walio wengi wanaona ni wizi na si pesa kwa ajiri ya uchaguzi.

  Hawa wakina RACHEL pamoja na kigogo wao ambae, kwa umri wakina RACHEL yeye ni mkongwe na bingwa wa sarakasi za kizamani.Manake kama tuhuma zinaenda kwa kina BEN,RACHEL wakati yeye ndie aliyetakiwa kuwa Kiongozi wa kuwaongoza wadogo aliokabidhiwa na Mwalimu kama kaka,matokeo yake yeye ndie Mwalimu wa kukubali na kusimamia,mikakati mibovu na hatari ya wafanyabishara kuchukua pesa za EPA.Yakiwazidi wazee wakati Watanzania wanapongangania kujua EPA ni nini jamani semeni ili mue huru, kwanini mkose usingizi kwa gharama za wengine.
   
Loading...