Kikwete na UKAWA wakubaliana

Kikwete na UKAWA wakubaliana

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
Ukawa-Ikulu.jpg

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TDC) alipokutana nao jana Ikulu ndogo mjini Dodoma. Picha na Ikulu

NA WAANDISHI WETU DAR, DODOMA
HATIMAYE mvutano kati ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Serikali umefikia kikomo baada ya pande mbili hizo kukubaliana na Rais Jakaya Kikwete kuboresha Katiba ya mwaka 1977 na kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani.

Hatima hiyo ilifikiwa jana kwenye kikao kilichofanyika kati ya Rais Kikwete na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kinachoundwa na vyama vyenye wabunge ambavyo ni CCM, Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF, TLP, UDP na UPDP inayowakilisha vyama visivyo wa wabunge, kilichofanyika Ikulu ndogo mjini Dodoma.

Mkutano wa awali wa viongozi hao ulifanyika Agosti 31, mwaka huu, katika Ikulu ya Kilimani, mjini Dodoma ambapo walipeana majukumu ya kufanya ili kuangalia namna bora ya kufikia mwafaka.

Katika mkutano wa jana, chanzo cha habari kutoka ndani ya mkutano huo kilieleza kuwa viongozi hao walikubaliana kuwa kutokana na mazingira ya sasa, ni vigumu kupata Katiba mpya ambayo itatumika mwakani.

Kutokana na hali hiyo, viongozi hao walikubaliana kuwa ni vyema vyama hivyo vikakaa na kuangalia mambo muhimu ya kuwekwa kwenye Katiba ya sasa.

"Vyama vinatakiwa vikae na kuangalia ni nini cha kuchukuliwa na kuwekwa kwenye Katiba hii ya sasa, baada ya kumaliza Uchaguzi Mkuu ndiyo sasa turudi kwenye mchakato wa kuandika Katiba mpya," alisema.

Alisema kuwa baada ya vyama hivyo kukaa na kukubaliana kitu cha kuweka kwenye Katiba inayotumika sasa, watayapeleka mapendekezo hayo serikalini kisha muswada wa marekebisho ya Katiba utapelekwa bungeni.

Kwenye suala la kuahirishwa kwa Bunge, chanzo kingine kilisema kuwa halikuzungumziwa, lakini busara inatarajiwa kutumika zaidi.

Mwenyekiti TCD
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo, alisema kuwa wamekubaliana kindugu.

Waandishi wa habari walipotaka afafanue kauli yake na kama kukubaliana huko kunamaanisha kusitisha Bunge ama Ukawa kurudi bungeni, Cheyo alisema: "Mimi naongea kama mwenyekiti wa vyama vyote, tumekubaliana kindugu, mazungumzo yalienda vizuri na kesho nitatoa taarifa kamili."

Mwanasheria Mkuu
Agosti 16, mwaka huu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, alizungumzia ugumu wa rais kuvunja Bunge la Katiba na kusema Katiba mpya ikishindwa kupatikana, iliyopo sasa itafanyiwa marekebisho.

Jaji Werema alikuwa akizungumzia hatima ya upatikanaji wa Katiba mpya na mwenendo wa vikao vya kamati za Bunge Maalumu vinavyoendelea sasa Dodoma, ambavyo vimesusiwa na wajumbe wanaounda Ukawa.

Alisema tathmini iliyofanyika ya mwenendo wa vikao hivyo, imeonyesha kuwa theluthi mbili inayohitajika ili kupitisha vifungu vinavyojadiliwa inapatikana, isipokuwa wasiwasi umebaki kwenye kupitisha vifungu hivyo wakati wa vikao vya pamoja vya wabunge wote.

Jaji Werema alisema kwa kutambua hilo, iwapo akidi ya theluthi mbili ya wajumbe haitapatikana wakati wa kupitisha Katiba iliyopendekezwa, baadhi ya vifungu vitakavyopitishwa vitachukuliwa na kupelekwa kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kuingizwa kwenye Katiba ya sasa ya mwaka 1977.

"Kwa sasa akidi kwenye kamati inatosha, tukifikia Bunge kuja na Katiba inayopendekezwa na kama hakuna theluthi mbili, tutarudi kwenye Bunge la kawaida (Bunge la Jamhuri ya Muungano) na kukubaliana, yaliyokuwa hayana ubishi tutayaweka na kuyatumia kwenye Katiba ya sasa, likiwamo suala la mgombea binafsi," alisema Jaji Werema.

CHANZO: Mtanzania
 
Watu wameziba masikio, wanafatuna posho ya mlala hoi, nadhani hata hizi ajali ni mwenyezi Mungu anatutumia ujumbe kuwa kama nchi tuko kwenye kipindi cha makosa makubwa, tumrejee Mungu na kutenda haki.....lakini hatuoni wala kusikia.

Mungu ibariki Tanzania
 
Kabisa sr. Hivi hatujiulizi hiki kipigo ni cha nini kwenye hizi ajali?
 
hapa hakuna hata jambo la kufurahisha, hivi hao wanasiasa wote wa CCM na Upinzani hawakujua kuwa muda wa kuanda katiba hautoshi? imekuwaje leo baada ya kutumia mabilio ya walala hoi wanakuja mbele yetu na kusema muda hautoshi kuandaa katiba mpya?

wanasiasa wanatupeleka pabaya, sitaki kuamini kama hawakuujua muda hauutoshi, wanatupeleka pabaya hawa watu na sisi tumebaki kuwachekea either kwa kujua ama kutojua, nina baki na maswali mengi kichwani bila jibu.

kwa mtazamo wangu naona wanainchi TUMESHIDWA VIBAYA, na wanasiasa WAMESINDA. poleni sana wakulima serikali haina hela ya kununua mazao yenu hela imeishia bunge hewa la katiba.
 
Bandu bandu kweli una waza kwa kutumia makalio badala uwaze na kuumia jinsi kodi yako inavoliwa na wajinga wachache wanaojiona wana akili kuliko wengine wewe unachekelea, acha ushoga kama ccm mabasha zako toka humu ndani humu tunataka watu wenye akili na wenye uchungu na hii nchi kama nyerere na ukawa
 
hapa hakuna hata jambo la kufurahisha, hivi hao wanasiasa wote wa CCM na Upinzani hawakujua kuwa muda wa kuanda katiba hautoshi? imekuwaje leo baada ya kutumia mabilio ya walala hoi wanakuja mbele yetu na kusema muda hautoshi kuandaa katiba mpya?

wanasiasa wanatupeleka pabaya, sitaki kuamini kama hawakuujua muda hauutoshi, wanatupeleka pabaya hawa watu na sisi tumebaki kuwachekea either kwa kujua ama kutojua, nina baki na maswali mengi kichwani bila jibu.

kwa mtazamo wangu naona wanainchi TUMESHIDWA VIBAYA, na wanasiasa WAMESINDA. poleni sana wakulima serikali haina hela ya kununua mazao yenu hela imeishia bunge hewa la katiba.

Mkuu CDS mda ulikuwa wa kutosha wa kuandika katiba,,lakini hao wanasiasa walipoteza mda mwingi sana mwanzoni mwa kikao wakijadiliana jinsi ya kupiga kura…yaani kura ya wazi au ….
 
Nape nauye naomba uje jukwaani na utufafanulie juu ya uamuzi huu. Ni wewe ndiye uliyesema hata Bila UKAWA KATIBA ITAPATIKANA NA AKIDI INATOSHA na wala hata hawawasumbui.
Inakuwaje tena mchakato mzima unaonekana hauna maana?
 
Hadi hapo ndo unaweza kuwa mwisho wa ukawa kwani huo mjadala wa katiba utakuwa umefungwa rasmi. Ni wakati wa kila chama kuvaa koti lake la siku zote tuone kama kuna walichovuna kupitia umoja wao wa kinafiki walokua wameunganisha.

Mpaka hapo mshindi CCM. Agenda za serikali 3 na serikali ya mkataba yenye kiti chake UN ndo imetoka hiyo labda msubiri awamu ya 5.
 
Watu wameziba masikio, wanafatuna posho ya mlala hoi, nadhani hata hizi ajali ni mwenyezi Mungu anatutumia ujumbe kuwa kama nchi tuko kwenye kipindi cha makosa makubwa, tumrejee Mungu na kutenda haki.....lakini hatuoni wala kusikia.

Mungu ibariki Tanzania
Dah,kwa hiyo makosa ya bungeni ndio maskini wanateketezwa huku kwenye ajali mkuu???
 
Ukawa hii ya bunge liendelee kujadili hadi October na kusita mpaka uchaguzi mimi sijaipenda kwanini lisisite sasaivi? kinachojadiliwa kule bungeni baadae ccm hawatataka kurudi nyuma ndio shida. bora mngeacha hayo mazungumzo tukaisubiri tu hii katiba yao kwenye kura ya maoni kuliko mlivyokubaliana.
 
Kikwete anachekewa mno kufanya maamuzi..ila washauri wenyewe ni kina wasira na lukuvi..!! Haishangazi
 
Hadi hapo ndo unaweza kuwa mwisho wa ukawa kwani huo mjadala wa katiba utakuwa umefungwa rasmi. Ni wakati wa kila chama kuvaa koti lake la siku zote tuone kama kuna walichovuna kupitia umoja wao wa kinafiki walokua wameunganisha.

Mpaka hapo mshindi CCM. Agenda za serikali 3 na serikali ya mkataba yenye kiti chake UN ndo imetoka hiyo labda msubiri awamu ya 5.

Njia nyeupe Zanzibar kudai kura ya maoni ya Uhuru.
 
Baada ya uchanguzi mchakato wa katiba utaendelea pale ulipoishia, ukiwa na baadhi ya sura mpya kabisa na akidi itatosha kila upande wa muungano, kwa ongezeko/ pungufu ya idadi ya wajumbe kwa pande zote mbili UKAWA au Tanzania kwanza vitaonekana dhahiri, ni kazi ya pande mbili kuchachalika kuongeza idadi ya wabunge
Ukawa hii ya bunge liendelee kujadili hadi October na kusita mpaka uchaguzi mimi sijaipenda kwanini lisisite sasaivi? kinachojadiliwa kule bungeni baadae ccm hawatataka kurudi nyuma ndio shida. bora mngeacha hayo mazungumzo tukaisubiri tu hii katiba yao kwenye kura ya maoni kuliko mlivyokubaliana.
 
Mauzauza ndo ninayoyaona hapa!shame on you all!1
 
Baada ya uchanguzi mchakato wa katiba utaendelea pale ulipoishia, ukiwa na baadhi ya sura mpya kabisa na akidi itatosha kila upande wa muungano, kwa ongezeko/ pungufu ya idadi ya wajumbe kwa pande zote mbili UKAWA au Tanzania kwanza vitaonekana dhahiri, ni kazi ya pande mbili kuchachalika kuongeza idadi ya wabunge

tafran tu sifaham mambo haya
 
hapa hakuna hata jambo la kufurahisha, hivi hao wanasiasa wote wa CCM na Upinzani hawakujua kuwa muda wa kuanda katiba hautoshi? imekuwaje leo baada ya kutumia mabilio ya walala hoi wanakuja mbele yetu na kusema muda hautoshi kuandaa katiba mpya?

wanasiasa wanatupeleka pabaya, sitaki kuamini kama hawakuujua muda hauutoshi, wanatupeleka pabaya hawa watu na sisi tumebaki kuwachekea either kwa kujua ama kutojua, nina baki na maswali mengi kichwani bila jibu.

kwa mtazamo wangu naona wanainchi TUMESHIDWA VIBAYA, na wanasiasa WAMESINDA. poleni sana wakulima serikali haina hela ya kununua mazao yenu hela imeishia bunge hewa la katiba.

Kwa fikra zako ulifikiri katiba mpya hii ingetumika kwenye uchaguzi wa mwakani?
 
Back
Top Bottom