Kikwete na Davos, Kagame na LA Times!


Kaka~Issue hapa ni kwamba pamoja na Rwanda kupokea misaadi kwa kiwango kinachozidi inayopokea Tz, kuna gap kubwa kwenye matumizi ya misaada kwao na matumizi ya misaada hiyo kwa Tz. Rwanda wametumia na wanaendelea kutumia misaada hiyo kuboresha kilimo cha kahawa, wakati huku Tz asilimia kubwa ya misaada inatumika kwenye shughuli za kiutawala, na kuwekeza zaidi kwenye mizingi ya chama tawala kuwekeza matumizi makubwa fedha za misaada kuhakikisha kwamba wanaendelea kubakia madarakani. Hilo ni wasi kila Mwuungwana hapa Tz anajua hilo. P. Kagame alijua kwa nini Rwanda ilikuwa masikini na akachukua hatua kulikabili tatizo. Lakini kwa upande wa Tz sio rais wala waziri wake mkuu anayejua kwa nini Tz ni masikini. Na mara nyingi wamekuwa wanakiri pasipo aibu tena kwa confidence kubwa tu. Tz kuna raslimali za asili ukilinganisha na nchi yeyote hapa East Afrika lakini tatizo ni viongozi hawa wasio wazalendo ndiyo wanao ifisidi hadi tumefikia hali tuliyonayo sasa. Ili tuweze kujinasibu walau tuamue kwa nia moja kuiondoa huu mfumo wa uongozi uliofikia uko wa kufikiri na tuupachike mfumo wenye mawazo mapya. Eidha kwa kupitia sanduku la kura au nguvu ya umma kama ilivyo na inavyotokea sasa kule mashari ya kati.
 

Kwanza nikupongeze kwa uandishi wako uliotukuka. Ama kweli ni faraja kusoma posting iliyowekwa na mwandishi wa habari aliyesomea. Ni tofauti kubwa sana na hizi tunazoandika sisi ma laymen😉

Nilitaka tu nikazie ubaya wa huu usombaji wa maliasili unaofanywa na waChina. Ni usombaji mbaya kuliko huu unaofanywa na makampuni ya magharibi kama Barrick na Anglo. Hawa waChina wako tayari kuilipa serikali kodi kubwa zaidi na kutoa misaada nikubwa zaidi na watu wasioelewa wanaishia kuchekelea.

Tunaoelewa tunajua kuwa mradi wa kiChina una linkages ndogo sana na uchumi wa taifa lenyeji. Wachina watakuja na wafanyakazi wao, mitambo yao, na hata hawatapangisha nyumba za wenyeji. Angalia walivyojenga Sam Nujoma Road, na Wanja la Taifa. Ni full waChina. Afadhali hata hawa mabepari wa magharibi wanatoa ajira za maana na kutumia vitu vyetu - hivyo kuacha pesa nchini.
 
Hakuna humiliation kubwa kwa watu wa Taifa hili kama hili jambo la watu kujazana kwenye ndege kila siku wanaenda ulaya na marekani kuomba misaada. Tumeletewa mpaka misaada ya vyandarua hapa na kujisifu eti ni moja ya matunda ya ziara zetu nyingi nje.
Zamani tulikuwa na siasa ya ujamaa na kujitegemea...why did we abandon both? Sasa hivi tunafuata siasa gani? Kuombaomba? Tunaopenda kubisha tuendelee na ubishani. Rwanda haina dhahabu, gas wala resources nyingine nyingi tulizonazo hapa. Ila wana leadership ya kuaminika. Sisi uongozi kwetu ni kuuza sura maana tunafanya biashara na biashara ni matangazo. Mhhh!
 
MM I am with you. Though people dont like to dwell with the truth. In order to explain the truth, you need to show some proof to those with puny minds. No wonder TZ, a rich and diverse independent country, still has to depend on aid and grants. No one cares. As long as they have ham burgers in the stalls. Not withstanding the bigger picture.

50 years after independence. With rich gold fields mined. Coffee, tea exported. Basically a Tanzanian lives bellow the poverty line. No wonder no European or American country is willing to help TZ. There is no accountability. People simply dont care. But it is this ambivalence which has landed this nation where we are now. A nation of beggars.

Even GOD will not help us if we dont help ourselves. Buckle up my fellow TANZANIAN. Pressure the govt. to change its stance. Let there be arrests of all those who have ripped this country. UNITED WE WOULD STAND BUT SEPARATE WE WILL FALL
 
Hilo nalikubali.
Lakini hypocrisy inaonekana wazi. Hawajaonyesha kama hawategemei misaada.
Mkisema misaada ni mitego, basi msisahau kuwa AFRICOM ni moja ya malipo na bado wamekatazwa kuuza Coltan za Kabila. Lakini in public, wanaponda wenzao wanaotegemea misaada.
Whats the difference?
 

Kaka~Unajua mara nyingi watu hawaachi kuyasema yale wanayoyasikia na kuyaona. Chukulia mfano rais Kagame tokea akiawa kamanda mkuu lile jeshi lilokuwa likiitwa Enderehamwa. Ambalo ndilo jeshi pekee lililofanikiwa kuzima yale mauwaji ya kimbari ya Rwanda, Kagame hakuwahi kutoa kauli ya kuonyesha proudness wala pompasity yeyote. Na hata baada ya kushika hatamu na kuwa rais kamili wa Rwanda bado ameendelea kuwa mnyenyekevu kwa raia wake huku akiwa very principled and sober katika nyanja zote za uongozi wake. Ndiyo maana watu wengi ambamo mmoja wao ni mleta thread (Johnson Mbwambo) huwa wanamtumia kama exampler wa some sort of elevated leadership. Kagame huwa busy na mambo ya inch yake wala hana muda wa kukaa kudiscuss issues za inch jirani kama vile akina Mwai Kibaki na Raila Odinga wanavyomsunda vidole JK wetu kwa uongozi wake dhaifu kama wengi wanavyouita hapa Tz.
 
Kuna mtu alianzisha thread jana kuhusu rwanda kwamba hamna kilichofanyika, hali ni mbaya etc etc, sijui aliuliza watu wizara ya elimu hawajui etc etc. Naomba aje asome hapa. Kagame ni mfano, tena wa kuigwa haraka.
 
Kuna mtu alianzisha thread jana kuhusu rwanda kwamba hamna kilichofanyika, hali ni mbaya etc etc, sijui aliuliza watu wizara ya elimu hawajui etc etc. Naomba aje asome hapa. Kagame ni mfano, tena wa kuigwa haraka.


Siku zote ombaomba huwa hajui kujitegemea, hata umpe duka leo pale kariakoo ataenda barabarani tu. Kifupi wabongo sisi i wavivu. Hata dhana ya uongozi hatujui. Naomba mtu mmoja mmoja aanze kujitegemea kwa rasilimali alizonazo si kwa rushwa au ubadhirifu.
 
Kwani hamjui wanatuletea kile walichochukua kwa percent ndogo sana? Kama 97% ya mapato ya dhahabu na almasi ni mali ya muwekezaji toka nje unategemea nini?Anachofanya JK ni kuomba zaidi kutoka kwa aliyemuuzia madini (dhahabu na almasi).Anachotakiwa kufanya nikurekebisha mrahaba ili ulisaidie taifa lake sasa kama wanauchumi na washauri wake hawatumii taaluma zao tuwaulize kwa nini walisoma uchumi?
 
Yaani niache kujipodoa nikae chini kusoma insha. Babu usituchoshe eeh. Kama vipi jaribu kuifupisha hiyo habari yako vinginevyo hupati mchango wangu ng'oooo......
hujaombwa kuchangia! Mbn hamko serious! Pumba Pumba ndo mnazowaza, vinyeo wengn!!!!!
 
JK heri angempa Lipumba homework ya kumuandalia cha kuongea maana tunapata shida ughaibuni uku maana wote wanajua nasi uwezo wetu ni kama JK.
[TABLE="align: left"]
[TR="class: afr_light"]
[TD="width: 390"] GDP (purchasing power parity):
[/TD]
[TD="align: right"]

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"] $13.46 billion (2011 est.)
country comparison to the world: 140 $12.55 billion (2010 est.)
$11.73 billion (2009 est.)
note: data are in 2011 US dollars
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 

In absolute numbers TZ inategemea bakuli zaidi ya Rwanda by far. 17.9 % ya GDP ya Rwanda (5.63 billion US$) ni ndogo sana ukulinganisha na 13.7 ya GDP ya TZ (23.6 billion US$),
 
Yaani niache kujipodoa nikae chini kusoma insha. Babu usituchoshe eeh. Kama vipi jaribu kuifupisha hiyo habari yako vinginevyo hupati mchango wangu ng'oooo......

mawazo yako kama ya madam spika...haki sawa italimaliza taifa hili..
 

Haya yanayosemwa kuhusu Rwanda ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika huenda ni kweli tupu. Rafiki yangu mmoja mwezi uliyopita alifanya 'African overland adventure', akasafiri kwa 'public transport, bus, train, boat, etc.' kutoka Cairo hadi Cape Town. Anadai Rwanda ni nchi iliyoendelea kuliko nchi zote alizopita ukiangalia makazi ya watu, mabarabara, mipangilio, etc. There is evidence on ground to this assessment .....
 
Kwanza kabisa (nataka twende poin by point) si kweli kuwa Tanzania inapokea misaada mingi zaidi ya Rwanda.

Uje na ushahidi kamili kuthibitisha kauli yako
 
Kuna mtu alianzisha thread jana kuhusu rwanda kwamba hamna kilichofanyika, hali ni mbaya etc etc, sijui aliuliza watu wizara ya elimu hawajui etc etc. Naomba aje asome hapa. Kagame ni mfano, tena wa kuigwa haraka.

Ule uzi ulikua umejaa propaganda za kitoto mno,yaani ni uzi ambao mtu alitoka kwy kijiwe cha wapiga debe akapata mawazo huko akaja kuupost!uzi haukwenda shule kabisa!tatiza kuna baadh ya watanzania uwa hatupendi ku appreciate na kujifunza toka kwa wengine!ila huu uzi wa sasa nimeusoma mpaka nasisimka,umetoa mwanga wa kutosha!najipanga nirudi kutoa mchango wangu
 

Well said mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…