Kikwete na CCM wanaua muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete na CCM wanaua muungano

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Laiser, Apr 16, 2012.

 1. L

  Laiser Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muasisi wa Ukomunisti Karl Marx akinukuu maneno ya Mwanafalsafa wa Kijerumani Hegel, alisema, Na Naomba kunukuu. "Kila mfumo una mbegu ndani yake za kujiharibu, au kujimaliza wenyewe" Nasema hivi kwa sababu kwamba ukiangalia wajumbe wa Katiba waliotangazwa na Rais na kwa maana hiyo CCM, wanaashiria hatari kwa Muungano.

  Serikali imetoa msimamo kila mara kuwa muungano upo hapa kudumu, na wala hautafutwa. Sasa kitendo cha kuchagua wajumbe sawa kutoka mikoa mitano ya Zanzibar dhidi ya wajumbe kutoka mikoa zaidi ya ishirini ya bara, kunaashiria kuanguka kwa muungano. Nasema hivi nikiwa na sababu.

  1. Kwanza ikumbukwe kwamba ndugu zetu wanzanzibar wamekuwa wakisukuma kila mara kuvunjika kwa muungano, Jambo ambalo serikali imekataa. Sasa kuwapa wingi wa idadi katika hii tume ni kugongea msumari wa mwisho

  2. Kitendo cha kugawa wajumbe hawa wa Zanzibar na hawa wa bara, kinaashiria kuwa hizi ni nchi mbili tufoauti zinazojaribu kujenga katiba mseto.

  3. Ninachojua mi kuwa Tz ni nchi moja chini ya muungano, na watu wote wana haki sawa mbele ya maswala ya
  muungano. Sula la katiba ni la muungano. Sasa kwa nini kundi la watu wachache toka sehemu ya muungano wapewe uwakilishi mkubwa kuliko wengine walio wengi? Haiwezekani kwa mantiki yoyote tano kulinganishwa na 21. Lengo la Kikwete na CCM ni nini?

  Kama Hypothesis yangu itakuwa ni sahihi, basi nadiriki kusema Kikwete, CCM na mfumo wake mzima wa utawala una makusudi mazima ya kuua muungano. Kulinganao na wingi wao, azma yao itatimia. Suala la Referendum halitasaidia hapa, kwani tunajua kuwa watanzania wengi wanasukumwa na siasa na udini kufanya maamuzi muhimu yanayogusa mustakabali wa Taifa letu.

  Naomba kuwakilisha kuwa, chembe za kuua muungano zimo ndani ya mfumo wenyewe (Serikali) inayopaswa kuulinda.
   
 2. m

  mtalii1 Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii kama ulikua hujui ss waznz tunajua kabla ya hili swala la katiba, na kwa kuthibitisha kikwete aliwaunganisha aman na seif sharif ili kupata nguvu ya kuuvunja muungano,
   
 3. Lastname

  Lastname JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 925
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wewe muungano wa nini ukiulizwa leo hii???
   
Loading...