Kikwete mpumzishe IGP Mwema

Kikwete mpumzishe IGP Mwema

Mzizi mkavu hii thread ilishaletwa hapa na picha ya huyo Meja Jenerali Kale Kayihura, tukaijadili na nimekubaliana na wewe kuwa umei-copy na kuipaste ila kwa kifupi sijaliona kosa la jeshi letu la POLISI
  • Kwani kuna lile suala la Usalama shirikishi ambapo tunashirikiana nao kama ndugu tofauti na huko Uganda
  • Sheria nyingi za kikandamizi zimeondolewa kulinganisha na mwaka 1979 baada ya (Vita vya kagera ulikuwa hujazaliwa) ilikuwa kila POLISI ni mwanajeshi yaani usiku hakuna kutembea bila kitambulisho
  • Kesi zote hata za madai POLISI walikuwa wakiziamua wao wenyewe wakati siku hizi hawaruhusiwi ila Mahakama tu
  • usiku mwisho kutembea ni saa moja kwa kuendesha Baiskeli kama haina taa leo ni mpaka asubuhi
sijui manataka POLISI ya aina gani
 
Last edited by a moderator:
Mimi nilikuwa polisi niliingia nikiwa na degree nikamaliza mafunzo pale Moshi CPP baadae niakaacha baada ya miaka kadhaa.Naweza kujaza pages kuelezea profile ya jeshi la polisi, kwa ujumla kama ni mtu wa maadili na mcha mungu polisi ni taasisi ya ovyo kabisa kwa Tanzania ,bora uwe mkulima na mfugaji wa njiwa kuliko kuendelea na kazi ya polisi.Polisi wanaongana wao kwa wao yaani we acha tu.

Nyie ndo mnaliharibu jeshi. Afadhali uliondoka. Uliingia na degree halafu ukaifanyia ama uliikalia tu. Baba yangu kila siku ananiambiaga nyie mlioingia na madegree yenu (na wengi wenu ni wa kufoji) ndo mnaliua jeshi kwamaana wanawategemea muwatetee ila ndo mpo tu na nyie kimaslahi.
Jeshi la wananchi si tulikua nao sawa ilikuaje wao wameweza kujitetea wameongezewa maslahi??!

Now my point is....toa solution hatutaki uongeze tena malalamiko.
 
Kweli umenena mkuu. Pale CCP wanachofundishwa ndicho hicho wanachotenda kwani pamoja na mambo mengine wanafundishwa kuiba na kuomba rushwa na ma instructor wasiokuwa waadilifu.
Pia mfumo wenyewe ni mbovu ni kwani hata wenyewe kwa wenyewe hawasemi ukweli hata sikiu moja yaani kwao ukweli ni dhambi kubw. Je tutegemee nini?
Sio hao polisi hata hata hao wanaojiita Jeshi la Uhamiaji nalo ni la ovyo kwenye mfumo wao afadhali na hoa polisi wana unafuu pamoja na uozo wao.
 
binafsi, naona tatizo, linapotokea tunashindwa wapi? tupeleke, shutuma zetu, na ndo maana, mengi ya malalamiko yetu, yanakwenda na maji, kiasi cha kutuacha tume duwaaaa, hatujui cha kufanya. Polisi inashutumiwa , imeorodheshwa orodha ya matukio, ambayo mtoa uzi, anaamini yanatosha kabisa rais, kufanya mabadiliko, ndani ya jeshi lake. lkn mimi naona kabla ya kumtaka rais afanye ,mabadiliko hayo, hebu kwanza ,tumtake IGP mwenyewe, awajibike kufanya mabadiliko, kwa wasaidizi wake, kulingana na uhitaji wa matatizo yaliyojitokeza ktk eneo husika.
 
Jeshi la polisi tz ni uozo mtupu, halina weledi wala uzalendo, ni genge la wahuni na wahalifu linalolindwa na sheria za ovyo, operation na mafunzo yake ni ya kijima yamepitwa na wakati na mkuu wake paul chagonja ni mtu wa ovyo aliyefura kwa kitambi cha rushwa! IGP Mwema alianza vizuri na alibuni mikakati na mipango ya kisasa ila kwa sasa amezidiwa kazi imemshinda hawezi kurekebisha nidhamu za askari wake jambo ambalo ni muhimu sana katika jeshi! jeshi hili lifumuliwe na liundwe upya kwa kuweka watu wazalendo, utii, kujali haki za binadamu, wakakamavu, hodari n.k na si polisi tulio nao sasa ambao ni waoga sana na mbinu wanayojua ni kufyatua risasi na mabomu bila kujali uzito wa hali halisi, ndivyo askari waoga walivyo, hawa polisi wetu hawawezi physical combat na akiwa hana silaha hata mtoto mdogo anaweza kumchakaza! polisi wa tz bila silaha ni sawa na kuku aliyenyonyolewa manyoya! ona jwtz inapotokea wakatembeza kichapo kwa raia(japo huwa si halali) huwezi kusikia wametumia silaha, ni ngwala, mangumi n.k na watashughulikia mtaa mzima!

Naamini IGP angekuwa anaitwa George Lucas usingesema hayo uliosema!

hakuna kitu kibaya kama kugubikwa na udini........
 
binafsi, naona tatizo, linapotokea tunashindwa wapi? tupeleke, shutuma zetu, na ndo maana, mengi ya malalamiko yetu, yanakwenda na maji, kiasi cha kutuacha tume duwaaaa, hatujui cha kufanya. Polisi inashutumiwa , imeorodheshwa orodha ya matukio, ambayo mtoa uzi, anaamini yanatosha kabisa rais, kufanya mabadiliko, ndani ya jeshi lake. lkn mimi naona kabla ya kumtaka rais afanye ,mabadiliko hayo, hebu kwanza ,tumtake IGP mwenyewe, awajibike kufanya mabadiliko, kwa wasaidizi wake, kulingana na uhitaji wa matatizo yaliyojitokeza ktk eneo husika.
 
MOJA ya sifa kuu za jeshi lolote lile duniani ni nidhamu, bila nidhamu ya kweli miongoni mwa askari na maofisa, basi jeshi husika hugeuka na kuwa ‘genge la wahuni’. Kwa wale wenye kumbukumbu nzuri miaka kadhaa iliyopita katika nchi jirani ya Uganda, Rais Yoweri Museveni, alimteua Meja Jenerali Kale Kayihura, kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchi hiyo.[/COLOR]

Hatua hiyo ilitokana na jeshi hilo kupoteza hadhi na heshima mbele ya umma baada ya kukithiri kwa vitendo vya uonevu dhidi ya raia, rushwa, ukiukwaji wa maadili ya kazi ya polisi na dhambi nyingine nyingi.

Wakati Meja Jenerali huyo anateuliwa, hakuwa askari polisi, bali alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Jeshi la Wananchi la Uganda (UPDF), na hadi sasa bado anaendelea na wadhifa huo nyeti.

Kusema kweli bila kung’ata maneno, Jeshi la Polisi Tanzania limepoteza hadhi na heshima mbele ya jamii yetu kwa kiasi kikubwa sana, na hakuna hatua zozote zile zenye dhamira ya kweli zinazoonekana kuchukuliwa kurekebisha hali hiyo.

Kama isingekuwa kazi iliyotukuka inayofanywa na vyombo vya habari nchini, bila shaka hali ingekuwa mbaya zaidi, lakini vyombo vya habari vimesaidia kuweka hadharani dhambi za polisi, hata pale polisi wanapoamua kusema uongo, mathalan katika tukio la kupigwa risasi mwanahabari Shaaban Matutu, Desemba 4, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Ukiukwaji wa haki za binadamu unaoambatana na mauaji yanayofahamika na yasiyofahamika ya raia wasio na hatia na hata wenye hatia kwa pamoja, vimelifanya Jeshi la Polisi kuwa chombo kisichoaminika tena mbele ya Watanzania, hasa wale masikini ambao ndio wengi.

Kuthibitisha hili, hebu Serikali iandae utaratibu wa kura za maoni miongoni mwa Watanzania ili kubaini imani ya wananchi na jeshi hilo, bila shaka zaidi ya asilimia 90 watasema hawana imani na polisi.

Katika kuthibitisha hilo ndani ya muda usiozidi wiki mbili, viongozi wawili wanaoheshimika kabisa katika jamii ya Watanzania wametamka bayana kuwa jeshi hilo linakiuka misingi ya haki za binadamu.

Si lengo kurudia kile walichokisema viongozi hao, lakini hapa nawazungumzia Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza Mzalendo, Jaji Mark Bomani, ambao wote walizungumzia ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na polisi.

Ukiacha viongozi hao wawili, hata Mkuu wa nchi, Rais Jakaya Kikwete, wakati akihutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wiki kadhaa zilizopita mjini Dodoma, alionyesha kutofurahishwa na vitendo vya polisi.

Ila kwa sababu hakuwa anazungumza na polisi, bali wanachama wa CCM, aliwaambia waache kuwatumia polisi katika kukabiliana na hoja za wapinzani, badala yake wapambane na wapinzani kwa hoja si kwa kutumia polisi.

Kwa lugha rahisi, Rais Kikwete aliliambia Jeshi la Polisi kuwa wakati umefika sasa liache kutumiwa na makada na viongozi wa CCM kunyanyasa wananchi kwa sababu ya tofauti za kiitikadi.

Kauli hiyo ya Mwenyekiti wa CCM Taifa ilikuja baada ya vilio vilivyodumu kwa miaka mingi kutoka kwa wananchi wakilaumu jeshi hilo kuwa linatumiwa na chama tawala kuvikandamiza vyama vya upinzani, jambo ambalo viongozi wa Jeshi la Polisi wamekuwa wakilipinga bila soni, ilhali hata mtoto mdogo anaweza kuthibitisha hilo.

Tabia hiyo ya polisi kutumiwa na wanasiasa wa chama tawala sio tu imekuwa ikizuia ukuaji wa demokrasia nchini kama chachu ya maendeleo, lakini imesababisha wananchi kupoteza maisha mara kadha wa kadha bila hatua zozote kuchukuliwa, zaidi ya kuambiwa mauaji yanachunguzwa.

Polisi wetu wanaua raia, kwa mfano, kwa mujibu wa vyombo vya habari, kauli iliyotolewa na wauguzi wa Hospitali ya Mwananyamala baada ya kumpokea mwanahabari Matutu, kwa kweli ilikuwa ya kutisha na kuhuzunisha.

Nanukuu moja ya magazeti ya kila siku yaliyomnukuu mwandishi Matutu; “Tukiwa pale huku maaskari wakiwazuia baadhi ya wafanyakazi waliofika kuniona wasipige picha, askari walijaribu kila mbinu kunishawishi nisifungue malalamiko dhidi yao na ndipo manesi waliokuwa eneo hilo waliniambia nina bahati kwa vile nimeletwa nikiwa hai.

pumba nyingi umeongea ni TANZANIA POLICE FORCE na wala sio jesh la mkonge...acha kuingza chokochoko kwa jesh
 
Ndo shida ya kuwapa mashemeji cheo.Polisi imepoteza mvuto kabisa maana hawana tofauti na majangiri.
 
Ni kweli kabisa I wish tungejilinda wenyewe baada yakunikwaza jana.Nilikuwa sijalipia stika ya bima wakanikamata.Nimeenda kulipa naambiwa najifanya bishoo wakati mi najua naichangia serikali baada ya kuihijumu.Mapokezi yote imekuwa vita kisa siwapi rushwa.Na nimeepa bora hizi hela zangu ziendelee kuliwa na Chama kuliko hawa mabaradhuli hapa mjini.
 
Back
Top Bottom