Kikwete kuteua Tume ya Katiba kabla ya Krismasi au Mwaka mpya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kuteua Tume ya Katiba kabla ya Krismasi au Mwaka mpya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 30, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuteua Tume ya kusimamia mchakato wa Katiba (Tume ya Katiba) ambayo itakusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba na hatimaye kuandika rasimu ya Katiba Mpya kabla rasimu hiyo haijapigiwa kura ya maoni na Watanzania wote. Rais Kikwete anatarajiwa kufanya hivyo baada ya kutia sahihi mswada wa Mapitio ya Katiba wa 2011 siku ya Jumanne kufuatia juhudi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo kushindwa kumshawishi asifanye hivyo ili kutoa muda wa kubadilisha mswada huo. Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu – ambayo haikuambatanishwa na picha ya kusainiwa huko – Rais Kikwete amefanya hivyo ili kuweza kuanzisha mchakato wa kupata Katiba Mpya ya Tanzania. “Kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010” imesema taarifa hiyo ya Ikulu iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu.
  Katika kuonesha kuwa Ikulu imezingatia mazungumzo ya Rais Kikwete na chama kikuu cha upinzani CDM Ikulu imesema kuwa “Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo”. Vile vile taarifa hiyo imetoa wito kwa Watanzania wenye maoni mbalimbali juu ya sheria hiyo kuendelea kutoa maoni hayo na kuwa “serikali itasikiliza na kuchukua hatua zipasazo”.
  Maoni ya baadhi ya wachunguzi wa mambo ya kisiasa nchini na Watanzania wengine sheria hiyo iliyopitishwa na Rais haina msingi wa Kikatiba kwani inapingana kabisa na Ibara ya 98 ya Katiba ya sasa ambayo hairuhusu mchakato wa kuandika Katiba Mpya isipokuwa mchakato wa Kibunge wa kufanyia marekebisho Katiba ya sasa”. Kutokana na hilo baadhi ya watu wanaamini kuwa kuna uwezekano wa mabadiliko makubwa ya sheria hiyo kwenye kikao kijacho cha Bunge kwani ili mchakato wa Katiba Mpya uweze kuwa halali kunahitajika mabadiliko katika Katiba ya sasa kwanza.
  “Katiba ya sasa imepuuzwa; hakuna mtu yeyote Tanzania mwenye madaraka ya kuamua kuandika Katiba Mpya wakati katiba ipo na ina mchakato wa kufanyiwa marekebisho mbalimbali chini ya Ibara ya 98” amesema mmoja wa wachambuzi hao – aliyekataa kutajwa jina lake- ambaye ni miongoni mwa wanaharakati wenye kupinga mchakato wa sheria ambao umependekezwa.
  Hata hivyo vyanzo mbalimbali vilivyo karibu na Ikulu vimedokeza kuwa kwa vile Sheria imeshapitishwa na ni halali hakuna kinachomzuia Rais Kikwete kuanza kuunda tume ya Katiba kabla ya mkutano ujao wa Bunge. “Ukweli ni kuwa sheria ipo sasa hivi na Rais amepewa madaraka ya kuunda tume na tunatarajia kuwa yumkini kabla ya Krismasi au mara tu kabla ya mwaka mpya, kutangaza tume ya Katiba Mpya kama zawadi ya kufungia mwaka” amesema afisa mmoja wa Ikulu aliyezungumza na FikraPevu na mwenye ujuzi wa jambo hilo.
  Alipoulizwa kwanini Rais asisubiri kuunda tume hadi Bunge likutane na kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na CDM kwenye mkutano wao na Rais afisa huyo ambaye si msemaji wa Ikulu alisema kwamba “mchakato wa Katiba mpya ndio umeanza na kupitishwa Sheria ni jambo la kwanza; jambo linalofuatia ni kuunda tume na kuipatia hadidu rejea na kuanza mchakato rasmi kwa mujibu wa sheria hiyo na hivyo hakuna sababu nyingine ya kuchelewa” na kuongezea kuwa “kama taarifa ya Ikulu ilivyosemwa sheria inaweza kufanyiwa mabadiliko mbalimbali kama sheria nyingine zinazofanyiwa bila kuathiri sana kazi za Tume”.
  Hata hivyo alipohojiwa kuwa itakuwaje kama mapendekezo ya sheria yatakayotolewa yanahitaji mabadiliko makubwa katika muundo wa tume na hata madaraka yake kuhojiwa afisa huyo alisema kwa kicheko kidogo “hakuna mabadiliko makubwa ya sheria yatakayofanyika, CCM ndio chenye serikali na CDM au chama kingine kitaweza kuleta maoni yao lakini mwisho wa siku CCM ndio itaamua ni maoni gani yanastahili kuingizwa kwenye sheria; Serikali haitakuwa tayari kuona mabadiliko makubwa yanafanyika na hivyo kupoteza maana ya tume yenyewe” alisema afisa huyo leo jioni.
  Hata hivyo, kama kidokezo cha pembeni afisa huyo alisema kuwa endapo Rais Kikwete hatotangaza tume siyo kwa sababu hajui wajumbe wake bali atajaribu kuwapa CDM taswira ya kusikilizwa na hivyo anaweza kusubiri hadi kikao kijacho ambapo CDM wataweza kutoa mapendekezo yao lakini yatazimwa kwa kutumia taratibu za Bunge. “Ujue wakirudi Bungeni watapewa nafasi ya kuwashawishi wabunge wa CCM walioukubali ule mswada; sasa wakishindwa na kura ikiitishwa watakuwa wameshindwa kihalali na hawawezi kulalamika na hawawezi kukimbia tena Bungeni” alisema.


  Na. M. M. Mwanakijiji (FikraPevu.com)
   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Of course
   
 3. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,424
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Rip demokrasia tanzania
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  MZEE MWANAKIJIJI ukumbuke kuwa huu ni mchezo haujanza leo. Kuwakaribisha Chadema Ikulu ni kuwazuga watu tu na kujustify yale wanayotaka. Katba imezungumzwa toka zamani sana. Mh SUmaye alizungumzia Whitepaper ambayo ilipitishwa sehemu mbalimbali kuhusu kitu hicho, lakini maoni yale yalipelekwa wapi? Tume ya vyama vingi iliyoundwa na Mzee mwinyi ilifanya kazi ya kuonesha vipendgele vingi ambavyo vinatakiwa kubadilishwa, what happened?


  Mabadiliko ya kweli ya katiba, hasa yenye maslahi ya Tanzania, hayakubaliki kwa CCMm unategemea nini? ni kuwazuga tu watu. Kama weli wewe ni mtanzania nakushauri usitegemee kitu na process hii. Wastage of time and money.

  Hii topic JK ameidaka ili kudivert attention, unajua kabisa kwa sasa issue muhimu ni magamba na kuyavua. sio katiba.
   
 5. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Hapo ndipo walitakiwa kujua kuwa mchezo aliocheza JK ni dirty politic. Kweli kazi ipo. Yangu masikio na macho. Hakuna kiongozi makini nchi za kiafrika. hakuna haki ilipatikana ikulu. Afrika haki hunyakuliwa haiombwi.
   
 6. babad

  babad Member

  #6
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM waache unafiki kwani hakukuwa na haja ya kujikosha eti waonane kumbe anajua alichopanga,kweli tusipopambana na serikali yetu wenyewe hakuna katiba ya wananchi
   
 7. l

  limited JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  tangu mwanzo serikali ya ccm haina mpango wa katiba mpya hiki ni kiini macho kingine na kutaka kuendesha nchi kwa udikteta fulani ivi na hii ni common in a lot of african coutries bado sana demokrasia ya kweli watu hwataka kumini kwamba wengine wanaweza kuongoza
   
 8. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lets get cool for a moment. Our freedom is at the door. Mind you nothing is so important than the one last minute. It will determine who loos and who win.
   
Loading...