watanzania wamekuwa wakichaguliwa kiongozi kila wakati. Ndo maana CCM wanasema hata jiwe litashinda, kikubwa tu liwekwe na CCM. Wanapojitokeza kupiga kura majina yao hawayakuti, wale wenye ufahamu mdogo kwa ajili ya njaa wamejikuta shahada zao zikinunuliwa. Na wale waliojitokeza kupiga kura, wakachagua rais wao wanaemtaka, hawakuheshimiwa kwani Tume ya Uchaguzi tayari ilikuwa na mshindi wake ambaye kwa vyovyote vile lazima wamtangaze mshindi. Mtu mmoja alisema ili mbunge chama pinzani ashinde inabidi amzidi wa CCM zaidi ya kura 7,000 sababu mbunge wa CCM akisimama tu tayari ana kura kama 4,500 hivi kutoka tume ya uchaguzi.
Kama kweli tunataka mabadiliko katika nchi hii NI LAZIMA TUWE KATIBA MPYA. Hili nafahamu si geni hapa JF na Tanzania kwa ujumla. Lakini hofu yangu ni kwamba katiba mpya itapigwa danadana mpaka 2015, na hapo maana yake ni MIAKA MINGINE 5 YA MATESO NA MASUMBUKO KWA WATANZANIA.
Labda hili la kumtoa JK litawachanganya tume na usalama wa Taifa kiasi kwamba watatenda haki. Mie sijui.
My take is kumtoa JK ndani ya CCM kwa katiba ya CCM haiwezekani sababu yeye ndiye mwenye Chama na kumtoa JK urais kwa katiba ya TZ haiwezekani sababu yeye ndiye mwenye NCHI. Na sidhani kama hali imefikia hapo, ukizingatia so far JK amewalinda sana "wafadhili" wake.
Watu wasipoteze muda wao!