Kikwete: Hakuna kura kwa mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Hakuna kura kwa mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 6, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Awashangaa wanaorubuniwa kwa vipapatio vya kuku
  [​IMG] Ni katika uchaguzi mkuu wa CCM mwaka huu  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete ,akihutubia wafuasi wa chama hicho Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana ikiwa ni maadhimisho ya miaka 35 ya chama hicho.(PICHA: IKULU)


  Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amewataka wanachama wake kutowachagua viongozi wenye tuhuma mbalimbali katika uchaguzi wa ndani ya Chama utakaofanyika baadaye mwaka huu.

  Rais Kikwete amesema makada wenye tabia za uchochezi, wala rushwa, wenye fitina na sera za kibaguzi wasichaguliwe na badala yake wachague viongozi wazalendo wenye kukijenga chama chao.

  Kadhalika, amewataka wanachama wa CCM kuwaumbua viongozi ambao si waadilifu watakaotaka nafasi mbalimbali kwa kutumia fedha kwa kutokuwapa nafasi yoyote ya uongozi.

  Aliyasema hayo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya kutimiza miaka 35 ya CCM tangu kuzaliwa kwake yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  “Viongozi wasiokuwa na sifa mnawajua; viongozi wachochezi, wala rushwa, wenye fitina, sera za kibaguzi wote hao mnawajua. Hawatakiwi kwenye chama bali tunataka viongozi wazalendo hivyo ni jukumu lenu kutekeleza sera za uongozi wa chama chetu ili kidumu katika amani iliyopo,” alisema Rais Kikwete.

  Alisema kauli mbiu ya Chama katika maadhimisho ya mwaka huu inasema ‘CCM imara inaanza na mimi, ninaimarisha chama changu kwa kuchagua viongozi waadilifu’ ni wazi kila mtu anaelewa maana ya kauli mbiu hiyo na wajibu wake.

  “Kwa nini mtu upoteze utu wako kwa kupokea Sh. 1,000 na kipapatio cha kuku? Wakati wa uchaguzi msikubali kudanganyika na viongozi wasiokuwa waaminifu hawatakuwa waadilifu kwenye chama…jukumu la viongozi wa chama ni kutekeleza matakwa ya raia na matatizo yanayowakabili pamoja na kuchukua hatua za kutatua changamoto za wananchi ili waendelee kuwa na mapenzi na CCM,” alisema.

  Aidha, alisema chama chake kina sifa ya kutekeleza sera zake na matatizo ya wananchi na kwamba ukweli huo upo nchi nzima ikiwemo kufanya tathmini ya shughuli zake katika kuhakikisha inatekeleza Ilani yake ya Uchaguzi wa mwaka 2010.

  Hata hivyo, aliwataka wanachama kubadilisha chama hicho kutokana na wakati kwa kuwa makini zaidi, kwenda na wakati, kujenga tabia ya kupambana na propaganda chafu zinazoashiria kukibomoa.

  “Tujenge uwezo wetu wa kujisemea na kufafanua yanayokuwa ya uongo dhidi yetu, likitushinda hili shughuli ya chama itatushinda; idara ya propaganda ni muhimu sana, ikitushinda hiyo tutapoteza mengi kwani CCM ni mlinzi wa taifa hili bila CCM imara nchi yetu itayumba,” alisema Rais Kikwete.

  Rais Kikwete alifafanua kuwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu uliopita, walikubaliana mambo makuu 23 ambayo wamekubaliana kuyafanya ikiwemo kuunda upya uongozi wa nchi pamoja na kutazama upya maamuzi yao.

  Alisema miongoni mwa mambo waliyokubaliana ni pamoja wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wachaguliwe kutoka wilayani kule waliko wanachama ili wajue wajibu wa kutembelea wanachama katika matawi badala ya ilivyokuwa awali wajumbe kuchaguliwa kutoka mkoani na ngazi ya taifa.

  “Tuchague viongozi wabunifu watakaokuwa na uwezo wa kukijenga chama na sio kukibomoa chama, wenye upeo mfupi wasio na uwezo wa kukitetea chama wasipewe bali wazalendo wa dhati na wenye mapenzi mema kwa chama,” alisema.

  Aliwataka wanachama wa CCM hasa vijana kujitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali kwenye chama chao wakati wa uchaguzi utakaofanyika mwaka huu na ikiwa hujuma zitajitokeza kwa wagombea wakati wa uchukuaji fomu za kugombea watoe taarifa mapema ili wahusika wachukuliwe hatua.

  “Wanawake wajitokeze kwenye nafasi mbalimbali pamoja na kuwepo nafasi maalum lakini wajitokeze kwa wingi katika nafasi mbalimbali za kugombea na wapewe kipaumbele kwani wanaweza,” alisema Rais Kikwete.

  Akizungumzia Katiba mpya, Rais aliwataka viongozi wa CCM kufanya mikutano ya kutoa elimu kwa wanachama ili wachangie maoni yao kwenye mchakato huo.

  “Tujipange vizuri katika mchakato wa kupata Katiba mpya kwa kuwa CCM ni jukumu letu kuchangia kwa asilimia kubwa; viongozi wote wajipange kutoa elimu ya kutosha kuwahamasisha wanachama kutoa maoni yao kuhusu mabadiliko ya Katiba mpya,” alisema Rais Kikwete.

  Naye Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Wilson Mukama, alisema chama hicho hakina msongo wa mawazo na kwamba kipo imara tofauti na watu wanavyokijadili.  Sherehe hizo zilihudhuriwa na maelfu ya wanachama wa CCM pamoja na viongozi kadhaa akiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Pius Msekwa, Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

  Hellen Mwango, Dar na Juma Ng’oko  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Adoe

  Adoe JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye red, mmmh!!!!
   
 3. Adoe

  Adoe JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye red, mmmh!!!!
   
 4. k

  kwini Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Penye red ni burudani ya kutisha! Kulia kugumu,kucheka haifai!
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  maji taka kwa lowassa=maji taka kwake,el knows to read between the lines,mafumbo yako ya pwani kayastukia atakujibu
   
 6. k

  kwini Member

  #6
  Feb 6, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Acha ajibu timsikie kwa kweli!yan ni vigumu sana kuelewa ukijaribu kulinganisha maneno na hali halic
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  good show Jk mwendo mdundo hakuna kumwangalia fisadi usoni
   
 8. King2

  King2 JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Fisadi Kikwete mbona yeye aliiba kura.. Awaachie mafisadi wenzake nao wapate shavu.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hadi kufikia 2015 mafisadi watakuwa wamejipima na kukimbia nchi
   
 10. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Serikalini vipi, wanatakiwa????????????
   
Loading...