kingadvisor
Senior Member
- Dec 21, 2011
- 109
- 30
Raisi Kikwete amekuwa akisumbuliwa sana siku za karibuni na watu kumtaka aachie ngazi hilo haliwezekani na haliruhusiwi sababu
1.Yeye kachaguliwa na watanzania wote si chama fulani tu.Hivyo chama fulani kikitaka aondoke ni sababu isiyo na maana wao ni minority na si majority
2.Kuna wabunge kwa hasira zao za kukosa vyeo na kukosa posho walizokuwa wakilipwa mara mbili mbili na kukosa nyongeza za posho wanamtolea macho wakiota atoke kwa hasira za ulafi wao hiyo si sababu ya maana ya kumfanya aachie ngazi
3.Kuna kundi la viongozi wa awamu zilizopita ambao walidhania uongozi ni hati miliki unayotakiwa ukiwa nayo uendelee kushika madaraka sehemu nono kila awamu inayoingia hadi ufe au ustaafu.Kikwete kabidili hali hiyo kawatupa nje waliozoea kudhani madaraka ni hati miliki kuanzia majeshini,serikalini na kwenye mashirika kaweka sura mpya na za vijana waliokuwa wako kwenye makabati ya kusahauliwa hilo linawauma hao waliozoea kuona uongozi kama hati miliki hivyo kujiona wamesahaulika na kutangaza vita za kutaka aaachie ngazi.Hahitaji kuachiia ngazi uongozi si hati miliki Kuwa kama ulikuwa kiongozi awamu fulani uendelee inayofuata.Kikwete kaweka rekodi ya kukomesha mtindo wa watu kuona kuwa uongozi ni hati miliki.Hana sababu ya kupata presha sababu ya kundi hilo
4.Kundi la wafanyabiashara wahuni na wapambe wao wanasiiasa wahuni na viongozi waandamizi wahuni wa serikalini na vyombo vyake waliozoea kujitoea mihela serikalini na mashirika yake kwa michoro ya aina mbalimbali kuanzia EPA,RICHMOND,n.k ambao kawapiga chini wao na michoro yao hao nao wanapiga yowe hawa nao wameshupalia aachie ngazi kwa kupitia wapambe waliozagaa ndani ya CCM,na ndani ya vyama vya upinzani.Wanamtaka aachie ngazi ili waibe sana si kuwa wanaitakia nchi mema hakuna kitu uongo mtupu.Hata kama Kikwete ni Mwizi ni heri kuliko l likiingia hili kundi nchi itabaki nyeupe haina kitu.
5.Kuna wale walioahidiwa vyeo fulani wakati wakati wa chaguzi zilizopita ambao baada ya Kikwete Kushika madaraka hakuwapa hao nao imekuwa nongwa wanataka aachie ngazi hawa wanafanya hivyo kwa maslahi binafsi si ya Taifa.Hana sababu ya kuachia ngazi kwa ajili ya hao.
6.Kuna wale ambao wanadhani kashindwa kazi na wanamshupalia ajiuzulu.Wanasahau kuwa uraisi ni taasisi.Akishindwa katibu mkuu si raisi kashindwa.Akishindwa Waziri si Raisi Kashindwa.Kundi hilo linataka kila kitu abebe Raisi sukari ikikosekana Raisi ajiuzulu,Dawa zikikosekana Raisi ajiuzulu.Kundi hili nalo ni kundi la waota ndoto ambao kila kitu huota Raisi tu.Halijui nani anahusika na kipi kwao kila kinachoshindikana au kuharibika Rais anahusika iwe ni mahakamani,bungeni ,na serikalini.Kundi hili linajua Raisi tu si mtu mwingine.
7.Kuna makundi ya kidini ambayo yalikuwa yakipata ruzuku au kupata misamaha ya kodi ambayo walikuwa wakiitumia vibaya kujineemesha KIBINAFSI kwa mgongo wa dini.Baada ya misamaha hiyo na ruzuku hizo kupungua au kuziondoa au kuziba mianya waliyokuwa wakitumia baadhi ya viongozi wa dini waliokuwa wamezoea michoro wamekuwa maadui wakubwa wa Raisi Kikwete wakizurura huko na huko kwenye dini zao na mikusanyiko ya dini zao kumtangaza kuwa hafai aachie ngazi sidhani kama hii ni sababu tosha.
Kwangu sioni sababu ya Raisi kuachia ngazi sijaona hoja nzito.Naomba aachwe amalize salama muda uliobakia wa uongozi wake kwa amani na utulivu.