Bukyanagandi,
Ninaomba utupe takwimu unazozijua wewe kuwa ni sahihi tofauti na alizoziandika mtoa mada ambaye ametoa takwimu na yuko precise. Tunahitaji ujustify utetezi wako kwa takwimu za kueleweka na si kubahaatisha kwa Mfano:-
Kikwete hajasafiri mara mia tatu na zaidi ila amesafiri mara kadhaa.
Siyo Raisi anayeshikilia nafasi za juu za maraisi watalii duniani ila anashika nafasi fulani akitanguliwa na maraisi fulani fulani na fulani.
Msafara wa Uingereza haukuwa na watu 40, ila alikuwa na watu kadhaa. AMA, Hao watu 40 aliokwenda nao uingereza ni watu fulani na walikuwa na umuhimu fulani katika hiyo safari. (Siyo kusema pengine...yawezekana.... labda....).
Unatakiwa kutetea kwamba matembezi ya kikwete hayana madhara katika mgawanyo na matumizi ya raslimali kwa sababu......
Pengine utusaidie kutupa mwanga kwa nini anakwenda yeye na hiyo misafara wakati nchi nyingi tunabalozi zetu kule au kwa nini asitume uwakilishi ambao unaweza ukafanya hizo shughuli kwa gharama nafuu kuliko anazotumia yeye na wapambe.
Lakini pia utuambie, maslahi gani ambayo nchi imenufaika na safari za kikwete, ambayo yanazizidi nchi maskini zinazohitaji misaada kama sis ambazo maraisi wake hawavinjari kama huyu wa kwetu.
Ni vizuri pia ukatuambia mafanikio yaliyotokana na utalii huo ambayo yamekuwa yaki pekee na ya juu zaidi kuliko yale yalyopatikana katika awamu ililyopita ama zilizopita ambazo hazikuwa na maraisi wa aina hii ya sasa.
Naomba usiwe imotional. Jaribu kuwa reasonable, analytical, fair but sincere. Lakini pia naomba ufahamu kwamba, kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje kwa miaka kumi ama kuwa raisi, hakubadilishi tabia ya asili ya mtu. Atabaki kuwa ni yule yule na tabia zake kama ni kujirusha na mademu, kutalii, kustarehe, kujionyesha na mbwembwe, ubinafisi, visasi, uchapa kazi, hila za kichini chini, udanganyifu, uadilifu, unafiki, ufisadi, n.k hata umpe cheo gani. Sana sana ataonyesha hadharani yale yanoyokubalika ili apigiwe makofi na yale yasiyokubalika atayatafutia mikakati ya kuyatekeleza kwa usiri lakini hatayaacha!.
Katika masuala haya naomba tufahamu kwamba yapo yenye yanayokidhi haja za taifa, na pia yapo yenye maslahi na yanakidhi haja za mtu binafsi.
NDIYO MAANA MIMI NASEMA, NI VIZURI KUWA NA MTU SAHIHI KWA KAZI FULANI, NA SI MTU YEYOTE HATA KAMA HANA SIFA SAHIHI SAHIHI UKITEGEMEA KWAMBA OFISI UTAKAYOMPA ITAMBADILISHA NA KUMFANYA AWE SAHIHI.
Hi Tabby,
Kabla sijakujibu nataka tuelewana kwanza katika mambo yafuatayo:
1. Mazungumzo yetu yawe
confined kwenye safari za
Mh. J.M.Kikwete kama zinaleta faida kwa Taifa au zinatutia hasara, that should be our main theme. Tusichanganye mambo.
2. Tusizungumzie mambo ya maisha yake Binafsi kwa kuwa hayatuhusu, na Wazungu wana msemo usemao kwamba
kama huna mambo mazuri ya kumsema/kumzungumza binadamu mwenzako ni vizuri kukaa kimya au umshauri kwa upendo.
3. Mimi sitazungumzia mambo ya
leadership quality zake au jinsi anavyo wateuwa viongozi wenzake wakumsaidia, yeye ndiye mwenye mahamuzi ya mwisho katika hilo na sisi tulimpa ridhaa ya
KUTUONGOZA-
dont you forget. Kama kuna kitu cha kujadili katika hilo basi kiletwe kwenye thread nyingine tusichanganye
MAMBO.
Nataka nikumbushie kwamba kila raia ana uhuru wa kutoa maoni katika fani ambayo ana ujuzi nayo, mimi humu nimezungumzia fani ninayo ielewa vuziri siyo mambo ya siasa au sijuhi itikadi. Baada ya kutafakali kwa muda mrefu niliamua kufanya tathimini ya thamani ya misaada ya kisayanzi na tekinolojia ambayo imeletwa nchini kufuatia effort za JK mweyewe, nazo ni kama zifuatavyo:
- Ujenzi na ukarabati wa Mahospitali ya kisasa including vifaa/mashine za dunia ya kwanza.
- Vyuo Vikuu(sayansi na technolojia na vifaa vya kufundishia vyote).
- Barabara (especially flyover na RT ambazo ziko mbioni kujengwa).
- Reli (anazo taka kuzifufua namely TAZARA na reli ya kati-Reli ya kati anataka kutandaza reli na mataruma mapya na kuiweka kwenye standard gauge, mtu uwezi kubeza Mega Project za magnitude kama hizo, ni gharama kubwa - najuwa hapa watu watasema hizo ni ahadi tu hakuna litakalo fanyika - you are DEAD WRONG, mbona Tazara watahanza hivi karibuni).
- Alizungumza na kupata misaada kutoka kwa kina Bill Gates wa kampuni ya Microsoft kwa ajili ya vyuo vikuu, vile vile na IBM.
- Aliwahi kutembelea mpaka Silicon Valley na kufanya mazungumzo na makampuni yaje kuwekeza Tanzania-nilimsikiliza vizuri alicho zungumza huko, yuko commited kweli kweli kuendeleza Taifa letu katika fani ya sayansi na technolojia na yuko well informed katika nyanja hizi na anajua manufaa ya sayansi na tekinolojia nchini.
Natoa ufafanuzi katika hili kwa kuwa nami ni mwana sayansi kwa hiyo siwezi kubeza effort zake kweye fani
ninayo ielewa vizuri in terms of gharama za ku-establish vitu kama hivyo nchini ni gharama KUBWA, ndiyo maana mimi siko
overly concern na safari zake kama zina manufaa kwa
TAIFA naona ni
HERI tu, watu wengine wanaweza kuwa na maoni tofauti.
Juzi juzi hapa nilimuona anazungumza na mwakilishi wa kampuni ya DELL, mwaka jana mama Clinton alipo tembelea Tanzanai nilimsikiliza alicho kuwa anazungumza kumuhusu Kikwete na kwa nini Kampuni ya Symbion imeamua kuja kuwekeza nchini na kutoa mafunzo kwa vijana kule Kidatu, vile vile nafikili Kikwete alikuwa Raisi wa kwanza au wa pili kutoka Africa kukaribishwa White House baada ya kuapishwa Raisi Obama-the question is, why pick JK - one may ask? hawa watu awafanyi mambo ya kubahatisha-kuna kitu watakuwa wamemtathimi ambacho wengi wetu hatukioni. (Please no name calling tuwe wastaraabu kidogo).
Kuna mwana JF aliuliza hivi
"kuna haja gani ya JK kwenda nje wakati kuna Mabarozi ambao wanaweza kumuwakilisha", mimi mambo ya protocols siyaelewi vizuri, lakini kwa akili za kawaida
Raisi wa nchi akienda physically kuomba misaada iwe kutoka kwa Raisi mwenzake au makampuni, ombi lake litachukuliwa seriously kuliko la
BAROZI.
Mwisho labda niseme kwamba
JK ni binadamu kama wewe na mimi siyo malaika, anaweza kuwa na mapungufu yake kama tulivyo sisi sote-tumpogeze pale inapobidi na tumshauri pale inapobidi aipendezi kumbeza beza bila ya kutoa ushauri wowote. Nazungumza ninayo practice mimi-kwa mfano nimetoa maoni/ushauri wangu wa kina kuhusu
TAZARA nini cha kufanyika kuiboresha-siyo lazima wachukue maoni yangu lakini I have played my part, nataka niwahakikishieni kwamba tukiwa na moyo wa kusaudia/kutoa maoni pale inapobidi mbona
TAIFA letu litapiga hatua kubwa ya kwenda
MBELE.