PreGE2025 Kikwete: Demokrasia ni zaidi ya Uchaguzi, Uwazi wa kuandikisha Wapiga Kura, Kupanga Vituo na Kuhesabu kura huleta Amani!

PreGE2025 Kikwete: Demokrasia ni zaidi ya Uchaguzi, Uwazi wa kuandikisha Wapiga Kura, Kupanga Vituo na Kuhesabu kura huleta Amani!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,521
Rais wa awamu ya 4 mzee Kikwete amesema Watu Wengi hufikiri Demokrasia ni Uchaguzi kumbe siyo bali Demokrasia ni zaidi ya Uchaguzi kwani ina mambo mengine mengi

Mzee Kikwete amesema kukiwa na uwazi Kwenye Uandikishaji Wapiga Kura, kupanga Vituo vya kupigia kura na uwazi Kwenye kuhesabu kura basi amani inakuwepo

Kwa ujumla michakato ya Uchaguzi inapokuwa wazi na Watu hawajazuiwa kutumia haki yao ya Kidemokrasia ya kuchagua na Kuchaguliwa na Uchaguzi wao ukaheshimiwa hapo ndipo amani inakuwepo, amesisitiza mh Kikwete

Mzee Kikwete ametoa nasaha hizi Kwenye Chuo Kikuu Cha Ulinzi na Usalama Nchini Nigeria

Source Mwananchi

My take; Uchaguzi wa Chadema Kanda ya Nyasa haukuwa Wazi na amani imetoweka hadi Leo 😀
 
Back
Top Bottom