Kikwete azidi kupata sifa kimataifa, aalikwa New York

Kikwete azidi kupata sifa kimataifa, aalikwa New York

Obugwa Izoba

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2013
Posts
10,482
Reaction score
11,690
Akihudhuria kongamano kuhusu afya
ya wakina mama na watoto, Toronto,
nchini Canada, Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa amekutana na Rais Jakaya
Kikwete wa Tanzania. Ban amempongeza Kikwete kwa
mwongozo wake katika maswala ya
maendeleo endelevu, akiwa
Mwenyekiti wa Kamisheni kuhusu
Elimu na Uwajibikaji kwa Afya ya Watoto na Wakina Mama, na pia katika Kamati ya Viongozi wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi.

Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo
kumwalikwa Rais Kikwete kuhudhuria
kongamano la tabia Nchi
litakalofanyika Septemba, tarehe 23, mjini New York.

Wawili hao pia wamekubaliana kuhusu
umuhimu wa kufikia maelewano ya
kudumu kuhusu mabadiliko ya tabia
nchi. Katibu Mkuu amesisitiza pia umuhimu
wa kuchukua hatua ili kutimiza
malengo ya maendeleo ya milenia na
kushughulikia ajenda ya maendeleo
endelevu baada ya mwaka 2015.


Wamezungumzia hali ya usalama ya
Ukanda wa Maziwa Makuu. Katibu Mkuu
ameishukuru Tanzania kwa mchango
wake katika Ujumbe wa Umoja wa
Mataifa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, DRC, MONUSCO, ikiwemo katika kikosi maalum cha kujibu
mashambulizi. Wamekubali kwamba ni
lazima kuondoa vikundi vya waasi
vinavyotishia DRC, hasa FDLR.
Halikadhalika, walijadili kuhusu
Burundi.
 
Mpenda safari Kikwete fursa hiyo hatoipisha ikapita hivi hivi. 🌴
 
Tunajivunia kuwa na rais kama kikwete kwenye taifa hili amefanya mambo makubwa sana lazima apongezwe kwa kazi kubwa anazofanya.
 
Tunajivunia kuwa na rais kama kikwete kwenye taifa hili amefanya mambo makubwa sana lazima apongezwe kwa kazi kubwa anazofanya.
Ah sana,Kikwete akiondoka tutampata wapi rais mwingine atakayezifuja kodi zetu kwa safari za kujivinjari?Sisi ndiyo ndiyo Wadanganyika bana wengine ni photocopy tu,Eti eeh!!!!?
 
Akili zako zinatosha kwenye kisoda tu jk kafanya vitu ambavyo hakuna rais aliyefanya waliomtangulia.

ni kweli kabisa, nyerere hakuwa rais wa kwenda ulaya kuhudhuria mabonanza. safari nyingine ni aibu kwa rais, membe ana kazi gani?
 
mzururaji haogopi ndege kupotea kama ile ya malaysia!!..mwaxhie membe safari zingine,unatutia aibu kila siku nguo zjmo kwenye begi...dah
 
Rais Kikwete mtu wa maana sana. Watanzania tuna haki ya kujivunia Rais wetu.
 
Ukiona wamagharibi wanakusifia ujue wewe ni rahisi na sio raisi tena
 
Rais omba omba naenda kuomba hd ushogo ni rais huyo, mm naona ka hana akili wazir wa mambo nje anakaz gan? Kikwete anasafiri mpaka nchi nyingine anadharaulila anapokewa na Meya wa jiji
 
Alihudhuria msiba wa msaani Recho na mwanae? Au anaboresha afya ya mama na mtoto kwa maneno na safari tu?
 
Ni ujinga kudhani Marekani wanampenda JK au wanamhusudu la.Wamarekani wanaihusudi rasrimali zisizo na mwangalizi za Tanganyika. Ndio maana kila mmarekani anashinda Tz mathalan,Clinton,Bush na familia zao.

Kauli mbiu ya kudumu ya marekani juu ya uhusiano wa kimataifa ni, "HATUNA RAFIKI WA KUDUMU NA WALA HATUNA ADUI WA KUDUMU."
Saadam Hussein rais wa zamani wa Iraq na mwasisi wa kundi la Al-Qaida Osama bin Laden walipata kuwa marafiki wakubwa wa marekani lakini wakaja kuwa adui wa kubwa wa marekani.
 
hivi kwa nini CCM mnamlisha maneno Ban,mnajidhalilisha
Hakuna aliyemlisha maneno Ban hapa. Ni wewe ndiye uliyemlisha maneno Lissu kwenye ule uzi wako kuhusiana na msiba wa mama Zitto. Amini usiamini, kubali usikubali, JK ni Rais mwenye upeo wa juu sana katika ukanda huu wa Maziwa makuu na Afrika kiujumla na ndiyo maana jitihada zake zinatambulika hata katika anga za kimataifa.
 
Kweli safari moja huanzisha nyignine,dah jamaa anatisha kwa safari.cjui anataka aweke record ambayo haitavunja miaka hamsini au mia moja ijao?nafikiri hili ndio ameliona litamfanya awe na record ya kukumbukwa kwa muda mrefu zaidi dunian baada ya urais wake.
 
Back
Top Bottom