Kikwete awapa Mafisadi Ahueni?

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Nikisoma hii habari kutoka Gazeti la Rai, najiuliza, hivi kweli Tanzania tuna nia ya kupambana na Uhujumu uchumi na kupiga vita Rushwa na Takrima?

Iweje sheria hii ifanyiwe mabadiliko ya haraka haraka na kwa usiri wakati nchi imefuniwa na wingu zito la rushwa?

Kwa nini Mwanasheria Mkuu alipeleka Bungeni muswaada huu wa kubadili sheria? Ni nani aliyeko Serikalini ambaye aliridhia kuwa jambo hili ni lazima lifanyiwe mabadiliko ili kutoa mianya ya kuruhusu wahujumu na hasa viongozi wanaotuhumiwa kuhujumu wapate njia ya mkato ya kujivua makosa na adhabu kali za Uhujumu na Rushwa?

Je lilipofika Bungeni, Spika na Wabunge wake kwa nini walilikubali na kulipigia kura? Ni kina nani walipiga kura ya ndio na ni Wabunge wangapi walipiga kura ya hapana? Kama Bunge linalojidai kujitutumua sasa hivi eti linapigana na Ufisadi, lilifumba macho na kupiga kura, ni vipi leo ling'ang'anie kudai kuwa Bunge ni mhimili wa tatu wa Serikali na kazi yake ni kuidhibiti Serikali ilhali inaelekea lilirubuniwa na kupewa Takrima na kupitisa muswaada huu wa kubadilisha Sheria hii kali ya Uhujumu uchumi?

Muswaada ulipopitishwa na Bunge na kufika Ikulu, kwa nini Rais Kikwete aliuhalalisha kwa kuweka Sahihi na kuufanya ni sheria mpya kufuta sheria ya awali? Je Rais Kikwete alisoma na kuelewa alicholetewa akibariki na kukigeuza kiwe sheria mpya? Je alihusika kutoka mwanzo kupitia Mwanasheria Mkuu kutunga marekebish ya Sheria hii ? Maana kama sikosei, marekebish ya Sheria mara nyingi hupata baraka ya Baraza la Mawaziri kwanza kabla ya kwenda Bungeni.

Kwa Rais Kikwete kukubali kuanza kwa Sheria hii mpya iliyorekebisha Sheria kali ya walai dhidi ya Uhujumu na Rushwa, atatuambia nini Watanzania leo hii Serikali yake inapodai imewafungulia kesi kina Yona, Mramba, Mgonja, Lukaza, Jeetu Patel na hat haya madai ya kumfungulia kesi Chenge?

Je kulikuwa na maana gani kuunda kamati ya Mwanyika, kamati ya Richmond, kamati ya Bomani ambazo lengo kuu ilikuwa ni kuchunguza tuhum za hujuma ikiwa amepitisha na kuhalalisha marekebisho haya ya Sheria ambayo yanafanya vita dhidi ya Hujuma, Rushwa, Takrima na Ufisadi sasa kuwa Butu?

Je Mheshimiwa Rais ni kweli ana nia ya kupiga vita Rushwa na Hujuma kama alivyotamka kwenye ufunguzi wa Makao Makuu mapya ya Takukuru?

Yetu macho!

http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1660


 
Acha wafanye haya madubwasha yote kwa mbwembwe wapendazo. Yanabakia kwenye hard-copy milele. Ipo siku yatarekebishwa moja baada ya jingine na vitukuu vyao kubebeshwa laana za mababu zao. This war ain't over, cheche za fikra ndo kwanza tu zimepekechwa, iwe miaka 10, 20, 50, 100...kuanzia sasa, these murky affairs of theirs are now documented and will be filtered out!!
 

Sasa ndio unachimba biti au?
 
mwisho wa mwisho wao waja,wache wafanye watakavyo kwa raha zao.2010 sio mbali tutazirudisha sheria kali zitafune matumbom yao.Tumechoka na ubabaishaji wa jk.
Bado hajatuambia fedha walizorudi za epa ziko wapi?
 
... Sheria hii mpya iliyorekebisha Sheria kali ya walai dhidi ya Uhujumu na Rushwa,

.. ili kutoa mianya ya kuruhusu wahujumu na hasa viongozi wanaotuhumiwa kuhujumu wapate njia ya mkato ya kujivua makosa na adhabu kali za Uhujumu na Rushwa?

Adhabu kali za rushwa pia zimeondolewa? Wapi wamesema hivyo?

Mkuu Kishoka,

Naomba tusaidiane kufanya kauchambuzi kadogo ambako naamini gazeti ilibidi lifanye, lakini media yetu ni maiti, ((ndio maana hata unaona wamegundua leo kitu kimetoka Bungeni January (as if ndani ya Bunge hakuna waandishi ), na kabla ya bunge muswada uliwekwa kwenye G'vmnt Gazette (angalia nchi nyingine wanavyotafakari miswada way before kwenda bungeni); kutoka Dodoma muswada ukaenda Ikulu way back in March ( Ikulu kuna kitengo cha waandishi, ambapo wana habari wanatakiwa wamuulize Rweyemamu nini kinaendelea ndani, Rais anafanya nini, every damn day! Marais wengine wakisaini kitu watu kibao wanamzunguka, dunia nzima inajua), muswada ulipotoka Ikulu ukarudi tena kwenye G'vmt Gazette kuutangaza kuwa sheria. Wao wamegundua leo! Sasa hapo kuna siri au ni kazi za uhoro tu wa waandishi wetu?))

Tuache hayo, sikutaka kwenda sana huko, samahani.

Nilichoanza kwa kusema naomba tusaidiane kukifanya ni hiki: tuonyeshane ni kwa vipi hili badiliko linamrahisishia maisha mra rushwa! Kilichobadilishwa, kwa mujibu wa RAIA MWEMA: zamani sheria ilisema aliyekula rushwa atakuwa mhujumu uchumi. Sasa hivi sio lazima.

Nambie, sheria mpya inasema aliyekula rushwa sasa atakuwa malaika huru wa bwana? Kama bado ataadhibiwa, tutafute, nambie, adhabu ya uhujumu uchumi ni nini, na adhabu ya rushwa ni nini.

Hapo ndo tutajua kweli "adhabu kali zimeondolewa," au tunaongea ongea tu bila kudadavua kwa undani.
 
Rev.Kishoka,

..kila kitu kilifanyika kwa uwazi kabisa. nashangaa hao raiamwema wanadai sheria imebadilishwa "kimya kimya."

..sijui kama wabunge wetu wana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi. inawezekana wanalegeza sheria ili na wao wakipata nafasi waweze "kutafuna" bila uwoga.
 
mwisho wa mwisho wao waja,wache wafanye watakavyo kwa raha zao.2010 sio mbali tutazirudisha sheria kali zitafune matumbom yao.Tumechoka na ubabaishaji wa jk.
Bado hajatuambia fedha walizorudi za epa ziko wapi?

Hiyo nyeusi teh teh teh teh mkuu umesema karibu mno. Kwa sheria zitakazowekwa na chadema ama!!
 
Woga wa Wa Tanzania katika kuchukua hatua stahili kwenye mambo ya Msingi ni tatizo kuliko matatizo yanayoikabili nchi kwa sasa...
 
Dilunga,
Mkuu wangu Mla Rushwa ni Mhujumu Uchumi kama mnavyoona kwamba hakuna tofauti kati ya Corruption kubwa na ndogo... crime ni ile ile tu isipokuwa wanachozidiana ni utaalam na utekelezaji wa hujuma yenyewe.
Mla Rushwa yeyote ni mtu anayedai malipo zaidi ya thamani ya huduma au mali..Yaani wale wanaohalalisha cha juu kuwa ni sheria, kibiashara hii pia ni Hujuma ya uchumi.

Mkuu ni lazima nyie viongozi muelewe kwanza source ya Mla rushwa na kwa nini anafanya hivyo. Mla Rushwa yeyote hudai fedha ya Ziada, kukiuka Policies ambazo ndizo nguzo ya Uchumi wa shirika au nchi.. Ni mtu ambaye anaweza kupunguza makusanyo ya pato au kodi. Mla Rushwa ni Mhujumu uchumi sawa na kiongozi anayeweka mikataba inayotuweka utumwani miaka yoite na kibaya zaidi basi hao viongozi wa juu kina Mkapa ndio husamehewa zaidi kwa sababu sheria za kumtuhumu mhujumu uchumi zitakuwa tofauti ili kuwaepusha viongozi wa juu na wale samaki wadogo wote wataangukia ktk sheria ndogo za Rushwa.

Na wananchi wakilalamika tutaambiwa huyu sii Mhujumu uchumi ila nmi mla Rushwa.. Mkuu wangu hakuna tofauti ya mwizi iwe mchomoa mifukoni au mbinjukaji wote ni wezi. Mlichofanya nyie ni kutofautisha aina ya wizi na thamani yake bila kujali kwamba madhara yake ni kitendo cha kukiuka taratibu za uzalishaji na kutoa huduma.
Nyie sii wanasheria ila ni wabunge viongozi ambao mnashindwa kuelewa kwamba mnapotenganisha vitu namna hii ndio kwanza mnawapa loopholes mawakili kuweza kuzishinda sheria zetu ktk vita hii ya Ufisadi.

Aidha mnafanya makusudi kuwakinga baadhi ya watu au ni makosa yaliyofanyika... still Public tulitakiwa kuyajua haya kama siku mlottangaza sheria ya Uhujumu Uchumi.. haikwenda ktk gazzeti la serikali pekee na viongozi wetu walihutubia ktk mikutano mabadiliko hayo wakizoa sifa na makofi ya wananchi kwa kufikia hatua hiyo. Leo mnafanya mabadiliko mkitumia gazeti la serikali kama njia ya kuwataarifu wananchi?.. come on now acheni uzembe!
 
Hakuna kiongozi aliye katika mamlaka ya kuhakikisha good governance ambaye yuko serious wewe. Kila kitu ni bora liende. Itaaachaje kuwapa mafisadi ahueni wakati wanatumia mafisadi hao hao kuingia madarakani???
 

Dilunga,

Labda nianze kwa kukuuliza kwa nini Sheria iliyokuwepo tangu mwaka 1984 ilifutwa? Je Serikali, Bunge na Rais walitueleza ni kwa nini wamefanya marekebisho hayo?

Nilichosema kuwa Sheria imeletwa ili kulegeza adhabu ni maoni yangu, sikuyasema kama hili ndio agizo kuu. Ni maoni yangu kutokana na kuona kwangu vita hii dhidi ya Uhujumu na Rushwa inavyoendeshwa.

Nitatafuta adhabu za Sheria ya Zamani na ama kutafuta adhabu kupitia sheria mpya ili tuweze kusonga mbele.
 
Dilunga,
Mkuu wangu Mla Rushwa ni Mhujumu Uchumi kama mnavyoona kwamba hakuna tofauti kati ya Corruption kubwa na ndogo... crime ni ile ile tu
Okay, Mkandara,

Basi kama kula rushwa ni exactly the same as kuhujumu uchumi, na kila aliyekula rushwa amehujumu uchumi, basi huhitaji sheria mbili mbili vitabuni. Wazungu wanasemaje, a dog is a dog by any other name, sio? Kwa hiyo whatever you call that law, it bans the same thing! Ha haha haa

...Nilichosema kuwa Sheria imeletwa ili kulegeza adhabu ni maoni yangu, sikuyasema kama hili ndio agizo kuu.

No, no, don't bail out! Don't give me that "ni maoni yangu" thing!

Umeshutumu serikali ya Kikwete kwa kuwapa ahueni wahujumu uchumi!

Kivipi? Umejuaje? Kwa nini? What do you mean "ni maoni yangu", umepewa maono kwenye njozi? Leo utatutajia hukumu ya uhujumu ni nini, na hukumu ya rushwa ni nini! Haha ahaaaaaaa...

Labda nianze kwa kukuuliza kwa nini Sheria iliyokuwepo tangu mwaka 1984 ilifutwa? Je Serikali, Bunge na Rais walitueleza ni kwa nini wamefanya marekebisho hayo?
Haikufutwa, ipo!

Kishoka, please soma hii link hapa, super important. Wamesemaje? Iliyofutwa Kishoka, ni ile ya 1983, ambayo ililalamikiwa sana na jamii, ilikuwa haina due process protections, watu wanakuwa rounded up bila taratibu za evidence, mahakama zenyewe zilikuwa maalum kama tribunals za kijeshi, tena hakuna rufaa, na huruhusiwi dhamana, and above all, huruhusiwi kuleta mwanasheria wa utetezi! I am not making this up Kishoka, unakuja peke yako mahakamani! Soma hapa.






 
Kwa ufupi tu jamaa hawezi kupambana na ufuisadi. Hivi mnajua kuwa vita ya ufisadi ni vita dhidi ya Chama Tawala cha CCM. kwani ufisadi ukiisha nchi hii ujue CCM haipo tena co tu madarakani bali hata kuwepo kwake kutakuwa ni ndoto. Hat siku moja ucitegemee C.C.M watondoa ufisadi. Labda wale wazee wakikaa kule DODOMA litupwe bomu wafe wote. waanze upya
 

Wewe hata kusema na waandishi hufai, inabidi uende kupeleka moto bungeni.
 
Tusikate tamaa, hawa akina JK hawana miaka 20 watakufa na hao akina chenge et al. Cheche za fikra zinendelea kuimarika miongoni mwa jamii na baadaye tutawafunga hata hao wajukuu zao. Kubadiri sheria ni kitu cha siku chache sana, sana sana tukiwa hurumia wajukuu zao tuta taifisha mali ya serikali iliyokombwa na babu zao (mkapa, chenge, dr. rashid, lowasa,) rostam yeye atakimbilia iran, n.k.
 
Dilunga,
"In the past three years covering 2006/8, some 8,725 cases were filed of which 3,239 were concluded. Some 4,486 cases which remained were at different stages of determination," the deputy minister noted.
Nipo nawe ukurasa mmoja bro!.
Haya hizi case 3239 ni zipi hizo au wale walioachiwa na kupewa msamaha na kadhalika ndio wanaifanya idadi hiyo maanake sikumbuki kabisa hata kesi 10 tu za wahujumu Uchumi toka mwaka 2006 wamehukumiwa Kifungo..
Mwenzangu, by any chance unayo list ya wahujumu wanaozungumzwa hapo juu?.
 
Dilunga,

I am not bailing out. My opinions are based on what I read on Raia Mwema and I have not seen any of parliamentary procceding in regards to the whole issue.

In addition, the actions of PCCB, AG and Central Government, signifies that the law has been reversed to delibarately create a pass to some fo the big shots who were involved in sabotage and corruption as a way to save the face of poor judgment or incompetence from Serikali Kuu (ndio kisa cha kusema maoni yangu).

For example, the allegations that Chenge has been involved in a dubious deal to purchase the Radar. Todate, not a single government entity has come out and give us a clarification on what URT is doing on its part to handle the officials who were involved with the whole saga.

What the URT has stated in recent days is its desire to get Vithlani back in Dar to face corruption (sabotage) charges, but no charges have been filed against Chenge and URT has declared that the corruption charges are UK government problem through SFO and all we want is our compensation from BEA!

I may not be a scholar of Judicial system or laws of Tanzania like you Mr. Dilunga, but I am guided by simple common sense just like ho Mkandara presented to you in response to your questions.

If URT had true intentions to fight Ufisadi, Hujuma and Rushwa, the laws that were created in 1983 which are considered harsh, would not have appear to be dilluted especially at time like these where majority of culprits are Government officials and all the conspiracy behind the rulling party involvement with embezzelment of our national treasury!
 
Katika habari yote nimevutiwa na sheria ya Uchawi hivi kuna mtu anaijua hii sheria ya uchawi ikoje au ni kitu gani ,labda wengine tutazidi kuelimika .Please kwa anaelifahamu hii atuwekee tuone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…