Kikwete awang'ong'a watanzania

Kikwete awang'ong'a watanzania

somijo

Senior Member
Joined
Apr 14, 2012
Posts
110
Reaction score
47
Wana JF

Leo mkulu amezindua hati ya ahadi ya madili kwenye sekta ya uma na sekta binafsi eti kwa lengo la kupunguza rushwa.
Kusema ukweli huku ni kuwakebehi na kuwang'ong'a watanzani. Yeye ndo amekuwa wa kwanza kutokuwa mwadilifu. EL kamnanga kimtindo kwenye sakata la Richard wa Mondi. Halafu ameishi nje ya nchi Kwa zaidi ya mwaka mmoja. Serikali yake imeongoza kwa kuwa na maadili mabovu. Rushwa sasa ivi imekuwa ni haki ya mtumishi na hajawahi kuonyesha kwa mfano kuwa rushwa inamkera zaidi ya kulalamikia. Mimi nategemea kiongozi awe kioo cha jamii Kwa yale anayoyafanya na kuafiki. Akitaka wananchi wawe waadiliifu basi yeye awe mwadilifu number 1. Sasa maswali ni je

Mkulu kuzindua hiyo hati anamaanisha nini??

Kwa nini anazindua sasa ivi wakati kabakiza miezi miwili tuu??

Akijachunguzwa hapo baadaye na kuonekana anaguswa na ubadhilifu atakuwa tayari kupokea adahabu yake??

Inaudhi sana!!!

Chanzo cahenel 10 habari.
 
Sijui kama akili yako inaakili wewe.
 
Ni kawaida yake mbona? Kama alishawaita waalimu waliompigia kura kuwa ni Mbayuwayu ndio ushangae kung'ong'a?
 
Hayo ndiyo makosa tuliyoyafanya watanzania mwaka2005 na ambayo hatutakiwi kuwapa kura wasanii, huyu ni msanii tena sana
 
Anapunguzaje rushwa wakati bembea lake analo tumia kubembea(CCM)rushwa ni patashika nguo kuchanika.
 
Back
Top Bottom