Kikwete atoa msimamo kuhusu Zimbabwe

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
1,862
Wadau,
Katika kuendeleza mashirikiano mema baina ya tanganyika na nchi nyingine, rais wetu sikivu Dr. J.M.K ametamka haya.


Rais Jakaya Kikwete, amesema Tanzania itaendelea kuunga mkono kwa dhati jitihada za Zimbabwe katika kutafuta mwafaka wa kudumu wa kisiasa na daima itaendelea kushikamana na wananchi wa Zimbabwe katika jitihada hizo.

Rais Kikwete aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipompokea na kuzungumza na Mjumbe Maalum wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kwenye Ikulu Ndogo mjini Dodoma alikokuwa akishiriki semina elekezi kwa wakuu wa mikoa, maafisa tawala wa mikoa na wakuu wapya wa wilaya.

Mjumbe huyo maalum, Sydney Sekeremayi, ambaye ni Waziri wa Nchi katika Serikali ya Rais Mugabe, yuko kwenye ziara ya kanda ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc), kuwaelezea wakuu wa nchi hizo maendeleo ya kisiasa nchini Zimbawe na utekelezaji wa Makubaliano ya Kisiasa (GPA) nchini humo.

Sekeremayi alimweleza Rais Kikwete kuhusu maendeleo ya utungaji Katiba mpya nchini humo ambayo rasimu yake ya kwanza tayari imetangazwa na sasa inajadiliwa na wadau wakuu wanaounda GPA kabla ya kuwasilishwa kwenye Bunge la nchi hiyo.

Waziri huyo amemwelezea Rais Kikwete kuhusu baadhi ya maeneo makuu katika Katiba hiyo ikiwa ni pamoja na mfumo wa serikali, usambazaji madaraka kwa wananchi, suala la uraia wa zaidi ya nchi moja na uhuru wa kijinsia.

Rais Kikwete aliipongeza Zimbabwe kwa kuendelea kutekeleza makubaliano ya GPA bila kuyumba pamoja na changamoto zote zinazokabili utekelezaji huo na kusema kuwa Tanzania itaendelea kuunga mkono kwa dhati jitihada za wananchi wa Zimbabwe kuleta mwafaka wa kisiasa nchini humo.

Aidha, Rais Kikwete alimweleza Sekeremayi kuhusu maendeleo ya mchakato wa utunzi mpya wa Katiba nchini Tanzania.


sosi: :: IPPMEDIA
 
Zenji kunawaka moto, JK kapiga kimya. anatoa misimamo kuhusu Zim! JK bana, ni zaidi ya tumjuavyo
 
Ni jambo zuri kwa JK kuunga mkono jitihada za ZIMBABWE kupata mwafaka wa kitaifa; ila mkuu wetu akumbuke kuwa hapa nyumbani ZANZIBAR kunawaka moto;wabara wakifukuzwa huko!!! Hata maandiko matakatifu yanatuhimiza kujali wa nyumbani mwetu;hivyo badala ya kung'ang'ana na nchi zingine JK aweke msisitizo kuokoa kabanda chake ambacho kinaungua!!!!
 
Zenji kunawaka moto, JK kapiga kimya. anatoa misimamo kuhusu Zim! JK bana, ni zaidi ya tumjuavyo

Aongee nini, mwenzako anafikiria kwa nini hayakutokea haya akiwa safarini?? Utaambiwa yuko busy na wageni wa Iran......... Kenya alikimbilia kwenda kutatua mgogoro, Comoro akapeleka mpaka jeshi, Zenji hata tu kuzungumzia ni shida!!!! Siasa za CCM sasa zinaanza ku-back fire!!
 
Back
Top Bottom