The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,950
- 12,550
Ni baada ya dc Makonda kushindwa kujibu swali aliloulizwa na Rais kwamba ni hatua gani amechukua kushughulikia tatizo la mafuriko pale basihaya Tegeta. DC alisema wanapanga mipango ya muda mrefu ndipo Rais kwa hasira akamwambia yeye anataka utafutwe ufumbuzi wa haraka kwani waathirika wanateseka sana.
Chanzo: chanel ten Habari
Mmh.. ningekuwa kuwa mimi ndege anayenong'ona ningemnong'oneza Makonda amuulize "Kwani wewe umefanya nini?"
Huko kwenye part alienda kama mgeni rasmi?Kwani DC Makonda alikwenda Disco na White Party.....sio vizuri ndugu zangu kumpaka matope Mh.Makonda.
Du heading imetisha kuliko uhalisia
hebu kaangalie tena hiyo taarifa ya habari,
Mkuu akisisitiza majukumu ndio KUFOKA?
Kwani Makonda ndio kaleta mafuriko?
chuki utazijua tu
Du heading imetisha kuliko uhalisia
hebu kaangalie tena hiyo taarifa ya habari,
Mkuu akisisitiza majukumu ndio KUFOKA?
Kwani Makonda ndio kaleta mafuriko?
chuki utazijua tu
Mipango ya muda mrefu kwani mafuriko hayo yameanza leo??
Kikwete anajua serikali yake dhaifu,zile siku 14 alizotoa stendi ya ubungo ihamishwe mbona mpaka leo hakuna kitu???
Yule hakukemea chochote. We utakemeaje wakati huo huo una cheka cheka. Body language na alichokuwa anatamka haviendani kabisa. Alikuwa anaongea nao kama washkaji vile. Sasa unakemea halafu wakati huo huo unacheka?hivikukemea ndio iko hivyo hahahaha
Mkuu DC amekemewa ili 'pepo' wa mipango ya muda mrefu amtoke na badala yake achukue hatua za HARAKA kuwanusuru waathirika wale wa mafuriko. Kuna tofauti KUBWA kati ya 'kukemea' na 'kukaripia', teh teh! mjulishe na Simiyu yetu.Mkuu hapo amemkemea wapi?
Anashindwa kutoa maagizo yanayotekelezeka anambana DC mbumbu kwenye uhandisi wa miundo mbinu, yeye mwenyewe kama rais hana jibu sembuse DC...poor me.