Kwa sasa mama, HAWAPO. Hapo awali/zamani kidogo walikuwepo Wawili MURTAZA LAKHA na ISSA SHIVJI Watanzania wenye asili ya Kiasia. Waliobaki Chai rangi mkate mkavu!!!
Temea mate chini! Mambo ya msituni yasikie hivi hivi tu na usiyaombe. Tuache mdhaha tuzidi kupigania kwa maneno makali na maandishi amani tuliyorithishwa na wahenga waliokuwa wakijali maisha na maslahi ya Taifa kwa ujumla.
Maneno yanaweza sana kuzaa matunda iwapo tutapata wanaojua/wenye vipaji vya kuhamasisha wananchi. Humu JF kuna watu wanaoandika vizuri mno na kama wanayoandika wanaweza kuyahamishia majukwaani, 'nyoka anaweza kutoka pangoni'. Mzee Mwanakijiji, Rev. Kishoka, FMEs, Mkandara, Mikael, Jasusi, Joka Kuu, Omarilyas, to name a few. Natamani hawa na wakereketwa wengine wote tunaolitakia taifa letu mema tungeunda kundi la uhamasishaji na utoaji wa elimu kwa raia mijini na vijijini ili wananchi waweze kutambua hali halisi na jinsi kundi la wachache wenye ubinafsi wanavyotupeleka kusikostahili.