Kikwete aikosesha CCM jeuri ya mwaka 1995 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete aikosesha CCM jeuri ya mwaka 1995

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Aug 21, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kikwete aikosesha CCM jeuri ya mwaka 1995


  MWAKA 1995 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa na jeuri. Baada ya mkutano mkuu kumteua Benjamin Mkapa kuwa mgombea urais wake, na Mwalimu Julius Nyerere akapita kumnadi, hofu ya kushindwa ilifutika.

  Ndiyo maana lilipotolewa pendekezo la kuandaliwa kwa mdahalo kwa wagombea urais, hawakuwa na wasiwasi.

  “Mgombea wetu, yuko tayari iwe sasa, kesho, usiku au mchana,” alisema kwa jeuri kabisa, katibu wa uenezi Kingunge Ngombale-Mwiru nilipomuuliza mwanasiasa huyo mkongwe. Wakati ule nilikuwa gazeti la Uhuru.

  Aliongeza, “Tena mgombea wetu yuko tayari kwa lugha yoyote; Kiswahili, Kiingereza au Kifaransa. Sasa nenda kawaulize, na wao wamejiandaa kwa Kiingereza na Kifaransa?”

  Kingunge alikuwa anatambia uwezo wa Mkapa ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Hakujulikana sana kwa wananchi, lakini pia hakuwa na doa la kisiasa.

  Swali la Kingunge “kawaulize na wao wamejiandaa kwa Kiingereza” lilimlenga aliyekuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi, Augustine Lyatonga Mrema, ambaye alivuma sana. Hakuwa na elimu ya Chuo Kikuu na kwa hiyo lugha hiyo ya Malikia Elizabeth inadaiwa haikuwa inapanda.

  Siku ya mdahalo ikafika. Katika mdahalo ule uliofanyika Hoteli ya Kilimanjaro (Leo Kilimanjaro Kempiski), Mkapa alionyesha uelewa mkubwa na alishawishi watu kwamba anaweza kuaminiwa Ikulu.

  Mwelekeo wa nani atakuwa rais ulionekana pale na kura za Mrema aliyekuwa anapewa nafasi kubwa kushinda zilipungua. Mrema aliwaangusha wafuasi wake.
  Kwa nini? Takriban mwezi mzima wasomi wa NCCR -Mageuzi Mabere Marando, Dk. Masumbuko Lamwai, Prince Bagenda nk walikuwa wakimfundisha mambo muhimu ya kuzungumza katika mdahalo, lakini ilipofika siku yenyewe akawa hajahitimu.

  Mrema aliishia kueleza historia yake; alivyokamata almasi uwanja wa ndege, alivyosuluhisha ndoa za watu nk lakini hakuwa na ubavu wa kuelezea masuala ya kiuchumi na maendeleo ya wananchi.

  Mgombea kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Lipumba alijieleza vizuri ila aliathiriwa na hila za CCM waliokichafua chama hicho kwamba kimejaa Chuki, Udini, Fitina. John Momose Cheyo wa United Democratic Party (UDP) alifurukuta bila malengo.

  Baadaye Cheyo, akiwa amezama katika lindi la mawazo wakati wa chakula alizinduka na kusema; “After all, I am a business man” (isitoshe mimi ni mfanyabiashara).

  Na wakati wa uchaguzi alipokosa kura hata kwenye kijiji chake, mwelekeo wa siasa wa Cheo ulibadilika akaanza kuamini kwamba haiwezekani kuishinda CCM. Kwisha!

  Mwaka jana Rais Jakaya Kikwete alipofanya ziara katika mkoa wa Shinyanga, Cheyo alimumwagia sifa kiongozi huyo wa kitaifa akisema hakuna wa kushindana naye. Msimamo huo anao hadi leo.

  Wenye fikra kama hizo ni pamoja na Mrema ambaye sasa anapita kila mahali kumpigia debe JK ilhali chama chake cha TLP kimemteua na kumpitisha Mutamwega Mugayuwa. Mrema yuko TLP kimwili, kifikra yuko CCM kama Cheyo.

  Mwaka 2005, TPP Maendeleo ilifanya kichekesho kama hicho. Kilimteua mgombea kiti cha urais mwanamke, Anna Senkoro lakini mwenyekiti wake, Peter Kuga Mziray alikuwa shabiki mkubwa wa Kikwete. Kwa hasira ya kutoswa Senkoro amerudi CCM.

  Mwaka 1994 Mchungaji Christopher Mtikila wa DP alialikwa pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aeleze sera zake. Alipotaka kujieleza kwa Kiswahili fasaha ili wanafunzi wamwelewe vizuri, wakamwambia “English please”.

  Aah! Mtikila alimwaga ung’enge na baada ya mkutano ule wanafunzi walimbeba juujuu hadi kwenye gari lake. Mtikila wa wakati ule alikuwa anahutubia na unapata msisimko. Alipohutubia umati wa watu Jangwani, akiita Wahindi ma*********, watu waliondoka na kwenda kuvunja magari ya Wahindi Kariakoo.

  Leo vipi? Mtikila wa leo amebadilika amekuwa ‘friendly fire’ yaani risasi inayofyatuka na kuua ndugu zake wa upinzani. Mtikila ni adui wa kambi ya upinzani kuliko hata CCM.

  Sababu ni moja tu, analipa fadhila za kibopa mmoja wa CCM aliyechangia kanisa lake na inadaiwa amesaidiwa kulipa deni asifungwe. Sasa anaachia friendly fire.

  Aliwahi kugombea kiti cha ubunge kupitia CUF katika uchaguzi mdogo wa Ludewa, aliposhindwa alidai CUF wana mapepo.

  Katika uchaguzi mdogo Jimbo la Tarime kujaza nafasi ya Chacha Wangwe, Mtikila alikuwa ‘beneti’ na Yussuf Makamba kuinanga CHADEMA. Kwa hiyo, haishangazi kusikia ameapa kummaliza Dk. Willibrod Slaa.

  Huo ndio mwelekeo wa upinzani, kila ukipiga hatua fulani ya mafanikio unakumbwa na friendly fires chini ya usimamizi wa CCM.

  Nimeeleza haya ili vijana wajue kwamba baadhi ya viongozi wetu kama Mtikila, Mrema, Mziray, Cheyo ni friendly fires kwa upinzani. Kwa lugha nyepesi hawa ni wapinzani wanaohujumu upinzani.

  Kwa hiyo, ukiwepo mdahalo leo kama walivyoomba CUF, wajue watakabiliwa na changamoto nzito kutoka friendly fires na siyo CCM ambayo imesema haitaki.

  Rais Kikwete alimjibu Prof. Lipumba mjini Dodoma: “Tutakutana jukwaani”. Makamba alipigilia msumari hivi karibuni akisema Rais hatafutwi kwa mdahalo.
  Siri nyuma ya majibu hayo ni kwamba CCM hawana ujasiri waliokuwa nao CCM mwaka 1995.

  Sababu za kuukataa zipo. Mwaka 1995 Mkapa hakuwa na doa lolote kisiasa wala kiutendaji ndiyo maana CCM haikuwa na shaka. Isitoshe Mkapa alikuwa mteule wa Baba wa Taifa.

  Lakini miaka mitano ya utawala wa Rais Kikwete (2005-2010) imemwacha majeruhi wa ahadi zake. Aliomba apelekewe orodha ya mafisadi, wala rushwa, wauza unga na wahalifu wengine, lakini majina yamebaki kwenye mashubaka ya ikulu.

  Ameshindwa kuwasaidia wapambanaji wa ufisadi na amewakumbatia mafisadi; wmeshindwa kuwachukulia hatua vigogo wenye kashfa mbalimbali; ufisadi katika ununuzi wa ndege ya rais, uidhinishaji kampuni tata ya Richmond kwa ajili ya kufua umeme wa dharura, ujenzi duni wa shule za sekondari za kata, safari zisizo na tija, kukataa kuwapa nyongeza wafanyakazi, kubagua watu wa kuwashtaki kati ya waliokwapua pesa za EPA nk.

  CCM wanapotazama yote hayo katika kipindi hiki ambacho kila kona ya nchi inalalamikia uongozi na utawala wa CCM—japo wamejipanga kusaidiwa na friendly fires—wanaona kasoro ni nyingi, hivyo suluhu pekee ni kukwepa mdahalo Kikwete asiumbuliwe.


  Chanzo: Mwanahalisi - toleo na. 202
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Mbona wadau nyie huwa hambandiki makala kama hizi moja kwa moja humu jukwaani mnasubiri kuhamishia humu? Kwani makala kama hii source yake haiwezi kuwa jf? Back to topic; kiukweli ni makala yenye viwango, data, vyanzo na kueleweka. Tatizo la ccm hapa kama wasemavyo wengi imekosa dira na mwelekeo. Kauli hizi zilimgharimu Horace maisha yake lakini leo kauli hizi zipo sana kwenye vinywa vya wana ccm wenyewe tena kumhadhara. Hawa wapinzani uchwara huwa hawakosekani wandugu. Laiti kama watanzani wangekuwa na uwezo wa kuwapuuza tungekuwa mbali. Asili ya kumpuuza mtu ni kumjua na kumsoma kwa kitambo fulani. Mrema, mtikila, cheyo, n.k. tunawafahamu tangu 1995. Kwa nini leo watuumize kichwa? Kina makamba pia ni watu wa kupuuza tu. Enzi za kina Mangula upuuzi huu wa kuropoka haukuwepo kwa kasi hii. Kwa mambo yanavyoenda kienyeji hata uchaguzi inawezekana kwenda kienyeji. Mdahalo ni chujio bora sana na wa kuamua kuwepo au kusiwepo mdahalo ni chombo huru kilichopewa mamlaka kitaifa na wananchi na si utashi wa watawala kusema leo tunaweza kumpeleka mgombea wetu kwenye mdahalo na kesho hatuwezi kwa vile tuna mapungufu mengi. Haya mambo yatawezekana pakiwepo na mabadiliko makubwa na pengine yasiyotarajiwa ila yenye amani ndani yake. Kipindi hiki ndio wakati pekee cha kufanya yote mazuri yatokee, pamoja na chombo huru na halali na cha kitaifa chenye uwezo wa kumwita mgombea yoyote kwenye mdahalo na asikaidi. Akikaidi ndio anguko lake
   
 3. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mtikila ameshaanza mbinu za kummaliza Dr Slaa. Kajifanya kutokutimiza masharti ya tume ya Uchaguzi kw amakusudi ili anyimwe kugombea uraisi. Hii si mara ya kwanza mtikila kugombea uraisi, so hizo fomu anazijua vizuri, iweje leo ashindwe kuzijaza na kutimiza masharti Akishakuwa huru kutokuwa mgombea, atakuwa na nafasi ya kumshambulia Dr Slaa. Chadema adui yenu no 1 sio ccm, ni watu kama Mtikila, Mrema, Lipumba , Mbatia etc. Hawa wasageni sageni mapema kwenye mikutano ya awali ya kampeni zenu, ili watanzania wajue kuwa mnawajua, na mnazitambua mbinu zao chafu na watawadharau pale watakapofungua midomo yao iliyosheheneshwa na fedha za kifisadi

  Mmalizeni mbali "kituko Mrema" kwa kuwa sasa ametia aibu, nadhani kuna ukichaa kwenye akili yake kwa kuwa hata kama ni ccm basi afanye kwa kutumia akili. Nakubaliana na spika Sitta kuwa kweli kafulia na sasa natafuta fadhila ili apate kitoweo.

  Halafu huyu Lipumba nadhani amepoteza dira, haya mambo ya umoja wa kitaifa ameyatoa wapi. Demokrasia haiivi kwa kuunganisha vyama,sasa nani ataukosoa huo umoja wa kitaifa. I doubt kama Prof anajua maana yake nini. Kwamba CUF wakishinda, atawaalika CCM kuunda serekali, and so what? Mimi nawafagilia sana Chadema, kwa kuwa wamemleta mtu tofauti na si Mbowe ambaye alijaribu akashindwa. Lipumba amegombea mara ngapi? au ameshafanya kuwa hobby? What makes him different this time around?Then anaongea ujinga!!
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni aibu kubwa sana kwa JK na CCM kukimbia mdahalo. Ameona hata aibu kumjibu Dr Slaa kuhusu challenge hiyo ambayo ni very bold. Kwa aibu CCM wakamtuma Tambwe na Makamba kumjibu Dr Slaa sababu za kukimbia mdahalo. Nashangaa kwa nini Dr Slaa naye hakujibu "Nataka majibu kutoka kwa mgombea mwenzangu, na si hawa vikaragosi!'
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwenye red: Ni vigumu kuamini haya usemayo. Kwani ilikuwa ni lazima kwa Mtikila kuchukua fomu za kugombea urais? Si angekaa kimya tu na matokeo yake yangekuwa haya haya tu -- ya yeye kutogombea?

  Mi nadhani kapata pigo kubwa kukosa uteuzi kwa kuwa kakosa jukwaa la kujibiana na wagombea wengine (particularly Dr Slaa) on equal footing. Kama tumjuavyo Mtikila ni msema hovyo, asingejali kabisa sheria na kanuni za kampeni za ustaarabu.
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Ni chombo gani kina mamlaka ya kuandaa mdahalo kwa wagombea uraisi?
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama huna mambo ya maana ya kuandika si ukae kimya, Unaposema mtu kama Prof. Lipumba atamhujumu slaa kwani slaa ni nani mpaka hata Prof awe na haja ya kumfikirisha? slaa ni kwako kwangu mimi si lolote. You said anaongea ujinga, I think wewe ndo unaongea ujinga. wadanganyika safari hii said no. HAWADANGANYIKI.
   
 8. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,506
  Likes Received: 1,230
  Trophy Points: 280
  :mad2:mdahalo mdahalo unahitajika kupima uelewa wa wagombea wetu CCM waache uoga
   
 9. c

  chama JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2010
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hoja ya mwanahalisi ni ya kweli suala la kujiuliza watanzania je tunahitaji mabadiliko ya kiuchumi au mabadiliko ya kisiasa na tuendelee kufa njaa? CCM kilikuwa chama kipenzi cha watanzania kwa mvuto wa sera zake za kumkomboa mtanzania, leo hii CCM kimekuwa chama cha mafisadi na wezi. Kinachotuponza watanzania ni kukosa wapinzani wa kweli. Viongozi wengi wa upinzani wanaangalia maslahi yao binafsi. mwenyekiti wa kitaifa chadema Bw. Mbowe ni mfanyibiashara suala la kumuachia Dr. Slaa awe mgombea wauraisi si kwasababu Mbowe ni mwanademokrasia bali analinda maslahiya biashara zake. Ni rahisi sana kwa CCM kumnyamazisha Mbowe kwa kutumia vijana wao wa TRA. Kuhusu Mtikila suala lipo wazi huyu anadaiwa mamilioni ya shs kwa mkopo wa nyumba yake ya mikocheni hela za kulipa za kulipa hana sasa jee ataweza kuwa mpinzani wa kweli? Cheyo yupo kwenye mkumbo huo. Ukiangalia CUF hakina nguvu bara Lipumba inabidi akubali sera za CUF hata kama hakubaliani nazo, Je Seif Shariff ni mpinzani wa CCM? Jibu si kweli Hamadi yupo kwenye pay roll ya CCM analipwa kwa mwezi zaidi ya TSHS milioni 5, Mrema ni porojo tu naye anatafuta njia za kujipatia ulaji ndio maana anagombea ubunge. Watanzania amkeni
   
Loading...