Kikwete Afichua Kipigo cha Lipumba

Kikwete Afichua Kipigo cha Lipumba

uongozi wa jk ni mfano wa kuigwa kwa afrika na duniani kote safi sana jk tweenzetu.

ungeandika Hivi;rais Kikwete Ni Mfano Wa Kuigwa Kwa Ccm Na Familia Yake
 
Polisi na Maandamano na Mikutano ya hadhara:
Mtanzania yoyote ana haki ya kushiriki katika maandamano kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ibara hii inatoa haki kwa kila mtanzania kushiriki katika mikusanyiko/maandamano ya amani.

Hata hivyo kundi linalofanya mkusanyiko/maandamano hayo katika maeneo ya wazi linapaswa kutoa taarifa kwa polisi si chini ya saa 48 kabla ya mkusanyiko/maandamano hayo. Taarifa inatolewa kwa kiongozi wa polisi wa eneo ambalo mkusanyiko unapendekezwa kufanyika.

Iwapo kiongozi wa polisi anayepokea taarifa hiyo ana sababu ya msingi ya kuona kuwa mkutano unaopendekezwa unaweza kusababisha uvunjifu wa amani na usalama wa umma anaweza kuzuia mkutano huo kufanyika.

Kwa upande mmoja askari polisi wana wajibu wa kuhakikisha amani inakuwepo. Kwa upande mwingine wanapaswa kuwawezesha wananchi kutumia haki yao ya msingi ya kufanya mikutano ya hadhara kwa amani na utulivu.

Matumizi ya Nguvu dhidi ya Maandamano au Mkutano wa hadhara.
Polisi hawapo kwa ajili ya kuwaadhibu watu, bali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa watu wapo salama na sheria hazivunjwi.

Inapotokea kuwa polisi wanalazimika kudhibiti mkusanyiko wa watu, wanapaswa wahakikishe kuwa kila wakifanyacho wanatumia kiasi. Watalazimika kutumia nguvu kama suluhisho la mwisho baada ya hatua nyingine zote kushindikana. Hata hivyo, iwapo nguvu italazimika kutumika basi iwe ya kadiri na inayoendana na mazingira, na itumike kwa muda mfupi iwezekanavyo.

Matumizi ya Silaha za Moto dhidi ya Raia.
Kama ilivyosemwa hapo juu, polisi watatumia nguvu kubwa pale ambapo imelazimika tu, na ambapo njia nyingine zote za udhibiti zimejaribiwa na kushindikana.

Polisi anaweza kutumia bunduki katika mazingira yafuatayo:



  1. Dhidi ya mtu anayetoroka, au
  2. Dhidi ya mtu anayefanya jaribio la kutoroka toka kizuizini au
  3. Dhidi ya mtu anayefanya jaribio la kutoroka asikamatwe
  4. Dhidi ya mtu anayetumia nguvu kumwondoa mtu mwingine kutoka kizuizi halali
  5. Dhidi ya mtu anayetumia nguvu kuzuia ukamatwaji halali wa mtu mwingine.
  6. Dhidi ya kundi linaloharibu mali au kutishia usalama wa raia baada ya kuonya mara tatu



Lakini pale tu askari anapokuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hawezi kuzuia utoro huo kwa njia nyingine ana ametoa onyo kwa mtu huyo kuwa bunduki itatumika iwapo hatatii na mtu huyo hajali onyo lililotolewa. Pia endapo polisi watakuwa na sababu ya kuamini kuwa wao wenyewe wako hatarini kuumizwa vibaya.

Wanapolazimika kutumia bunduki dhidi ya kundi linalofanya uharibifu au kutishia usalama wa raia, risasi zinapaswa kulengwa chini na katika kundi linaloonekana ni tishio, lakini si kwa lengo la kusababisha mauaji bali kuwatawanya. Mara kundi linapoonyesha dalili la kutawanyika askari wanapaswa kusitisha upigaji risasi.

Polisi wanaolazimika kutumia risasi wanawajibika kutolea maelezo kila risasi waliyotumia kwa kuandika taarifa inayowekwa katika kumbukumbu.

Pale itakapothibitika kuwa polisi ametumia nguvu isiyohitajika atachukuliwa hatua za kinidhamu au kufunguliwa mashtaka kwa kosa la jinai.
 
Lipumba alisema atenda kuwashitaki polisi kwa rais kikwete kuwa walimpiga nadhani asipoteze mda kwenda huko atapigwa tena naona jk hataki ujinga kwa sasa.


images
Ha ha ha ha ha ha ..............!
 
uongozi wa jk ni mfano wa kuigwa kwa afrika na duniani kote safi sana jk tweenzetu.

JK ni muwazi kabisa. Amejibu swali ipasavyo

Kama utaiyangalia vizuri mwanzo hadi mwisho wa tukio hilo utagundua kuwa police wamevunja sheria za nchi na wametumika kisiasa, wametumia nguvu haliyakuwa uwezo wa kuvunja maandamano kwa njia ya usalama ulikuwapo,polisi walishindwa kutoa ushirikiano na kiongozi wa chama pro lipumba na badala yake kumuona kama kigaragosi na kumdhalilisha pamoja na wananchi.

Nyinyi naona mutakuwa na matatizo, kwani hamutaki kukubali ukweli na mushazowea kuendeshwa kipunda punda na ndio maana munashabikia police kwa furaha.
 
Hicho ni kiburi tu cha CCM kwa kulewa madaraka ............................. huko Kenya enzi za Kenyata kuna askari wa Kikuyu aliwahi kumpiga Moi bakora kwenye road block tena wakati akiwa makamu wa Rais. Imagine, nothing happened to him!! Baada ya Moi kuupata Urais jamaa ilibidi aachie ngazi mwenyewe .....................!!! There is always a payback time!!
 
ungeandika Hivi;rais Kikwete Ni Mfano Wa Kuigwa Kwa Ccm Na Familia Yake
Mkuu wewe sifuri kabisa kuliko hata mbowe unadhani akili ya kikwete mnaweza kumfikia hata kama mtajikusanya familia yenu yote?
 
Hicho ni kiburi tu cha CCM kwa kulewa madaraka ............................. huko Kenya enzi za Kenyata kuna askari wa Kikuyu aliwahi kumpiga Moi bakora kwenye road block tena wakati akiwa makamu wa Rais. Imagine, nothing happened to him!! Baada ya Moi kuupata Urais jamaa ilibidi aachie ngazi mwenyewe .....................!!! There is always a payback time!!
Tatizo lipumba hata huo uongozi hachaguliki labda awe rais wa chaneta au baraza la maganga wa jadi.
 
Tatizo lipumba hata huo uongozi hachaguliki labda awe rais wa chaneta au baraza la maganga wa jadi.

Inawezekana unachosema ni kweli ...................... hiyo haihalalishi yeye kupigwa. bado ana mchango mkubwa katika demokrasia ya nchi hata kama hatakuja kuwa Rais wa nchi hii. Mbona mambo yakizidi maji JK huwa anawaita Ikulu!!
 
Wana JF, naomba mnisaidie hili, Prof. Lipumba kulazimisha kufanya maadhimisho haramu, Polisi kanda maalumu waliyakataa tena mbele ya viongozi wa CUF, Pia Polisi Temeke hakuna barua iliyoandikwa, halafu Prof. akaamua kwenda kuazimisha, alipodjibitiwa akaamua kuwatumia wafuasivwake kama chambo ili kupata sifa ya kisiasa, je hii ni tabia sahihi inayofaa kufanywa na mtu kama Lipumba? Je ndiyo kuporomoka kisiasa? Naomba majibu badala ya matusi na kejeli.
 
Mbona una Wasiwasi wa matusi na kejeli? Unajua kabisa kwa ulichoandika lazima utakutana na hivyo vitu sio..........
 
Mkuu wewe sifuri kabisa kuliko hata mbowe unadhani akili ya kikwete mnaweza kumfikia hata kama mtajikusanya familia yenu yote?

Akili gani hizo matope Mbowe ana busara na hekima kuliko Jk
 
Kikwete akitoa mrejesho kwa polisi amesema anawapa hongera sn."hatuwezi kuvumilia watu kuvunja sheria za nchi". amenukuliwana magazeti ya Leo
my take
Lipumba ikulu unaenda kufata nn? umeshajibiwa labda km unataka statehouse juice and delicious lunch.
 
NITAFICHA WAPI USO WANGU KWA
ALIYOSEMA RAIS?????
Rais profesa Jakaya Mrisho Kikwete
ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa
kututawala na kutuletea maendeleo
wakati wa ukoloni.Akizungumza mbele ya
waandishi wa habari ikulu leo
alimuambia rais wa Ujerumani kwamba
wakati wanatutawala walitufanyia mambo
mengi sana mazuri ikiwemo kutujengea
jengo la ikulu.
Rais ameniumbua.Sijui nitaficha wapi
uso wangu.Tangu mwaka 2008 nimekuwa
nikiwafundisha wanafunzi wangu historia
huku nikiwaaminisha kwamba wakoloni
hawakuwa na nia njema.Niliwaambia
wakoloni walikuwa wakitunyonya,wa
kitukandamiza na kutudhalilisha.
Niliwaambia hata elimu waliyoitoa na
miundombinu waliyojenga ilikuwa ya
kuendeleza unyonyaji.
Niliwaambia wanafunzi wangu kuwa watu
waliowapinga wakoloni na kuwapiga vita
kama kina Mkwawa ndio mashujaa
wetu.Niliwasema vibaya wakoloni huku
nikitumia vitabu vya kina Walter Rodney
kama “HOW EUROPE UNDERDEVELOPED
AFRICA” na kunukuu sehemu ya “The Dar
es salaam School of thought” kuaminisha
wanafunzi wangu kwamba wakoloni
hawakutufaa.
Leo rais kaniumbua.Kama wanafunzi
wangu wamemsikiliza rais
nitakoma.Lazima watamuamini kwa
sababu rais wetu ni profesa.
 
Ndege wanaofanana huruka pamoja ulitegemea angewagombiza lakini huu uonevu una mwisho wake
 
Back
Top Bottom